Envaya
Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Icyongereza. Edit translations

watoto  wakiwa kituoni 

afisa habari wa shirika na mratibu wa mafunzo akihojiana na mmoja wa washiliki waliofanikiwa kuhuzulia mafunzo ya ukatili wa kijisia na kingono 

UKATILI WA KIJINSIA

Maana

Ni aina ya ukatili unaohushisha mwanaume na mwanamke, unaotokana na jinsi wanavyohusiana na hali ya kutokuwepo kwa uwiano kati yao. Ukatili huu hufanywa kwa mtu kwa sababu tu ya jinsi yake.

Ukatili wa kijinsia huathiri wanawake zaidi kuliko wanaume.

AINA ZA UKATILI WA KIJINSIA

a)       Ukatili wa kimwili

Ni kitendo anachofanyiwa mtu kinachohusisha kuumizwa mwili na huweza kuonekana moja kwa moja au mwathirika kuhisi maumivu bila watu wengine kutambua kitendo hicho. Mifano ya ukatili wa kimwili ni vipigo, shambulio la mwili, kuchomwa mwili moto, matumizi ya silaha, kuvuta nywele, kusukuma, kunyonga mkono au mguu, kumpiga kichwa ukutani/sakafuni na kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu yoyote ya mwili

b)      Ukatili wa kisaikolojia

Ni ukatili ambao mtu anatendewa na unamsababishia maumivu kiakili/kihisia ambapo mtu mwingine hawezi kutambua kuwa mwenzake ametendewa ukatili hadi mazingira yatakapojitokeza na mtendewa akajieleza. Mifano ya ukatili wa kisaikolojia ni matusi kwa njia ya maneno au ishara yenye lengo la kudhalilisha, vitisho na kutishia kufanya fujo, maneno ya kufedhehesha, kudharauliwa hadharani, kutishia kutoa siri, kuingiliwa faragha, kutishiwa kuuawa, wivu wa kupindukia, kunyang’anywa watoto kwa makusudi.

c)       Ukatili katika uhusiano wa kingono

Ukatili huu huambatana na vitendo vinavyohusiana na masuala ya ngono. Mfano unyanyasaji/bughudha za kijinsia, kujamiiana kwa maharimu, ubakaji ndaniya ndoa, ulawiti,utekaji na usafirishaji wa wanaume au wanawake na watoto kwa ajili ya ngono, utumwa wa kingono, mashambulio na kuingiza vitu vigumu kwenye sehemu za siri.  

d)      Ukatili wa kiuchumi

Ni aina ya ukatili ambao unamnyima fursa za kiuchumi mwanamke au mwanaume katika kujiongeza kipato na kuchangia katika maendeleo. Aina hii ya ukatili huwapata wanawake kutokana na hali yao ya kuwa tegemezi kwa wenzi wao . Mifano ya ukatili huu ni kunyang’anywa mali, ubaguzi katika fursa za kiuchumi na umilikiwa mali, ubaguzi katika fursa za kujipatia mahitaji muhimu ya chakula, malazi na mavazi, kunyimwa haki za kurithi, elimu duni na mianya finyu ya fursa za kujielimisha, kunyimwa sehemu ya mapato ambayo ni jasho lako na kukatazwa kufanya kazi.  

 

      

e)      Ukatili unaotokana na tamaduni au mila potofu

Huu unatokana na mila na desturi za jamii zetu ambazo zinakinzana na haki za binadamu hivyo kuchangia kuwepo kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia. Kwa mfano ndoa za kushurutisha, ndoa za utotoni, kutakasa wajane, kurithi wajane, ukeketaji, matambiko ya kingono kwa watoto, ndoa za maharimu, kufungiwa au kuwekwa ndani kwa shuruti, ndoa za ushirika, miiko ya chakula na ukatili utokanao na mahari

 

ATHARI ZA UKATILI WA KIJINSIA

a)       Athari kwa mtu binafsi

  1. Athari ya kisaikolojia
  2. Athari ya kimwili

b)      Athari katika ngazi ya familia

Ukatili wa kijinsia unaweza kusababisha madhara mengi katika familia. Baadhi yake ni kupotea kwa amani na upendo, kujenga uhamasa kati ya wanafamilia, watoto kutoroka nyumbani, kupoteza pato la familia kwa kutibu majeraha yanayotokana na vitendo vya ukatili, kupoteza wazazi au watoto. c) Athari katika ngazi ya jamii

Kupoteza nguvu kazi ya jamii, muda na mali katika kushughulikia maswala ya ukatili wa kijinsia, ongezeko la watoto wa mitaani, migogoro na umaskini.

d) Athari katika ngazi ya taifa

Madhara ya ukatili wa kijinsia hapa ni pamoja na kupoteza nguvukazi ya taifa, ongezeko la watoto mitaani, ongezeko la uhalifu, maendeleo duni, kupoteza rasilimali na kuongezeka kwa umaskini. Taarifa juu ya ukatili wa kijinsia inaweza kutolewa katika

-Afisa Ustawi wa Jamii

-Afisa maendeleo ya jamii

-Polisi dawati la jinsia

-Afisa mtendaji kata

-Paralegal

 

we open trainnig for prayer 

enjoyment we need to happen for the children all days

                             Lunch at the trannig of sexual harrasment