Envaya
Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

large.jpg

Mjumbe wa Baraza la AZAKi ndugu Shabani Nanyanga

large.jpg

Wajumbe wa Baraza la AZAKi la Lindi Mjini

Midahalo ya katiba iwe ni njia ya kujenga uwezo wa jamii katika kushiriki utungaji wa katiba mpya na kuonesha kuwa katiba ni zao la muafaka wa kitaifa na si mkataba wa watawala na watawaliwa kwani hakuna kundi la watawala katika nchi ya kidemokrasia kama Tanzania

FCS Narrative Report

Introduction

Lindi Non Governmental Organization Network
LINGONET
Kujenga Uwezo na Stadi za AZAKi za Ushawishi na Utetezi na Kuimarisha Ushiriki katika Sera na Maendeleo.
FCS/MG/3/08/95
Dates: 01 Septemba, 2011Quarter(s): 30 Novemba, 2011
Bw. Sharifu Maloya
S.L.P. 92
LINDI
Simu Mezani: +255 23 220 2630
Nukushi: +255 23 220 2630
Simu Kiganjani: +255 787 187 008
+255 712 316 141
+255 762 565 383
Barua Pepe: smaloya22@yahoo.com
smaloya@hotmail.co.uk

Project Description

Policy Engagement
Civil Society Capacity Strengthening
Mradi huu una malengo ya kujenga na kuongeza uwezo wa Asasi za Kiraia (AZAKi) za wilaya 5 za Mkoa wa Lindi za; Liwale, Ruangwa, Nachingwea, Kilwa na Lindi. Mradi unawezesha kujenga uwezo wa viongozi wa AZAKi katika uendeshaji na uendelezaji wa asasi zao kiufanisi kwa kufanya mafunzo kwa viongozi wa AZAKi kimuundo, kiutendaji na kiuendeshaji (Organizational Development). Mradi unawezesha viongozi kutambua dhana na dhima ya AZAKi kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya watu tangu wakati kabla ya ukoloni, wakati wa ukoloni, baada ya uhuru na hatimaye ndani ya mfumo wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa. Pia kuangalia Dira, Dhima, Malengo, Maadili na mambo mengine muhimu kwa ajili ya kuwezesha AZAKi kuendeshwa na kuendelezwa kwa ufanisi.

Vile vile mradi unalenga kuinua na kuboresha uelewa wa AZAKi na jamii kuhusu michakato mbalimbali ya kisera na maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa. Michakato hiyo ni pamoja na uandaaji wa mipango na bajeti za maendeleo, utungaji wa sheria ndogondogo na utoaji wa maamuzi mbalimbali. Imedhamiriwa na kukusudiwa kwamba kwa kufanya hivyo itawezesha kuongeza na kuboreka kwa uelewa na ushiriki wa AZAKi na jamii kiujumla katika michakato husika ya kisera, kisheria na maendeleo kiujumla. Pia kuimarisha na kuboresha ushirikiano na mahusiano baina ya AZAKi kwa upande mmoja na Serikali kwa upande mwingine ili kuhakikisha kwamba wananchi wakiwa walengwa wakuu wa michakato yote wanawezeshwa kupunguza umaskini uliokithiri na kujiletea maendeleo endelevu.

RegionDistrictWardVillagesTotal Beneficiaries
LindiLiwale - - 480
LindiLindi - - 480
LindiNachingwea - - 480
LindiKilwa - - 480
LindiRuangwa - - 480
 Direct BeneficiariesIndirect Beneficiaries
Female62141
Male78199
Total140340

Project Outputs and Activities

1. Wawakilishi 30 wa AZAKi toka wilaya ya Lindi wamejengewa uwezo na uelewa wa maarifa, mbinu na stadi za kufanya Ufuatiliaji Uwajibikaji Kijamii (SAM) katika miradi na shughuli za maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ifikapo Desemba, 2011.

2. Viongozi/watendaji 20 wa Halmashauri za Wilaya/Manispaa Lindi na wawakilishi 20 wa AZAKi wamejadiliana, kubadilishana habari na taarifa, ujuzi na uzoefu kuhusu uandaaji, utekelezaji, usimamizi na tathmini za miradi na shughuli za maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ifikapo Desemba, 2011.

3. Ushirikiano na mahusiano baina ya viongozi/watendaji wa Halmashauri 2 za wilaya/manispaa Lindi na wawakilishi wa AZAKi vimeimarika na kuboreka ifikapo Desemba, 2011.

4. Ushiriki wa walengwa/wadau katika ufuatiliaji wa maendeleo ya utekelezaji mradi umeongezeka na kuboreka katika Halmashauri za wilaya/manispaa Lindii ifikapo Desemba, 2011.
1. Kuendesha mafunzo kwa wawakilishi wa AZAKi 30 juu ya dhana ya Ufuatiliaji Uwajibikaji Kijamii (SAM) kwa siku 2 katika kila wilaya 5 za Mkoa wa Lindi ifikapo Desemba 2011.

2. Kufanya vikao vya siku 1 vya wadau 20 wa maendeleo kati ya viongozi/watendaji wa Halmashauri za Wilaya/Manispaa za Mkoa wa Lindi na wawakilishi wa AZAKi vya kubadilishana habari na taarifa, ujuzi na uzoefu kuhusu uandaaji mipango na bajeti za maendeleo, utekelezaji, usimamizi na tathmini za utekelezaji ifikapo Desemba, 2011.

3. Kufanya ufuatiliaji na tathmini shirikishi walengwa/wadau za maendeleo ya utekelezaji mradi katika Halmashauri za Wilaya/Manispaa 5 za Mkoa wa Lindi ifikapo Desemba, 2011.

1. Viongozi 30 wa AZAKi toka Halmashauri za wilaya/manispaa Lindi wamejengewa uwezo na kuongezewa maarifa, mbinu na stadi za kufanya Ufuatiliaji Uwajibikaji Kijamii (SAM) katika miradi na shughuli za maendeleo vinavyotekelezwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa yaliyofanyika Oktoba, 2011.

2. Kufanyika kwa kikao cha pamoja cha wadau 20 kati ya viongozi/ watendaji wa Halmashauri ya Wilaya Lindi na wawakilishi wa AZAKi kujadiliana na kubadilishana habari na taarifa, ujuzi na uzoefu tofauti kuhusu uandaaji, utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya mipango na bajeti za maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kilichofanyika Oktoba, 2011.

4.Kufanyika kwa kikao cha pamoja cha wadau 20 kati ya viongozi/watendaji wa Halmashauri ya Manispaa Lindi ili kujadiliana na kubadilishana habari na taarifa, ujuzi na uzoefu tofauti kuhusu uandaaji, utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini za mipango na bajeti za maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kilichofanyika Oktoba, 2011.

5. Kufanyika kwa ufuatiliaji na tathmini ya maendeleo ya utekelezaji wa mradi kwa kushirikisha walengwa/wadau 40 kwa idadi ya 20 toka kila halmashauri za wilaya na manispaa Lindi uliofanyika mnamo Novemba, 2011.
1. Ndiyo, tofauti iliyopo ni kubadilishwa kwa shughuli ya mradi kutoka ya Kuendesha mafunzo kwa wawakilishi wa AZAKi wa wilaya 5 za Mkoa wa Lindi juu ya Programu ya Maboresho ya Serikali za Mitaa (LGRP) na badala yake kuwa Mafunzo kwa wawakilishi wa AZAKi juu ya dhana ya Ufuatiliaji Uwajibikaji Kijamii (SAM). Hata hivyo kabla ya kufanyika kwa mabadiliko haya Mratibu wa Mradi aliwasiliana na Afisa Programu anayesimamia mradi huu katika FCS, Bi. Rose Kihulya na kutoa idhini ya kutekelezwa kwa shughuli hiyo pasipo kupoteza walengwa na mantiki ya mradi.
1. Mafunzo juu ya dhana ya SAM kwa AZAKi za wilaya ya Liwale na Ruangwa (TZS. 1,851,000/=)

2. Vikao vya wadau kati ya viongozi/watendaji wa Halmashauri na AZAKi katika wilaya za Liwale na Ruangwa (TZS. 3,080,000/=).

3. Kufanya ufuatiliaji na tathmini ya maendeleo ua utekelezaji mradi katika wilaya za Liwale na Ruangwa (TZS. 1,470,000/=)

4. Gharama za Utawala na Uendeshaji wa Mradi (TZS. 2,065,000/=).

Project Outcomes and Impact

1. Kuongezeka kwa Uwezo na uelewa wa kimaarifa, mbinu na stadi kwa AZAKi za kufanya Ufuatiliaji Uwajibikaji Kijamiii (SAM).

2. Kuimarika na kuboreka kwa Ushiriki wa AZAKi na jamii katika kufuatilia Uwajibikaji Kijamii (SAM) katika miradi na shughuli za maendeleo katika Halmashauri za wilaya/manispaa za Mkoa wa Lindi.

3. Kuboreka kwa Uwajibikaji wa viongozi katika utekelezaji na usimamizi wa miradi na shughuli za maendeleo katika Halmashauri za wilaya/manispaa za Mkoa wa Lindi.

4. Kuongezeka na kuboreka kwa Uwazi wa viongozi na watendaji wa Halmashauri katika utekelezaji wa miradi na shughuli za maendeleo katika Halmashauri za wilaya/manispaa za Mkoa wa Lindi.

5. Kuimarika na kuboreka kwa Ushirikiano na mahusiano baina ya viongozi/watendaji wa Halmshauri za Wilaya/manispaa za Mkoa wa Lindi na AZAKi.

6 Kuongezeka, kuimarika na kuboreka kwa Upashanaji na upatikanaji wa habari na taarifa za utekelezaji, usimamizi na ufanisi wa mipango na bajeti za maendeleo.
1. Kuongezeka kwa uwezo na uelewa wa AZAKi juu ya dhana ya SAM.

2. Kuongezeka na kuboreka kwa Ushiriki wa AZAKi na wananchi katika michakato ya Sera na maendeleo.

3. Kuimarika na kuboreka kwa Uwezo wa wananchi kufuatilia uwajibikaji wa kijamii kwa viongozi na watendaji wa Halmshauri za wilaya/manispaa husika.

4. Kuboreka kwa Ushirikiano na mahusiano baina na miongoni mwa wawakilishi wa AZAKi

5. Kuimarika na kuboreka kwa Mahusiano na ushirikiano baina ya viongozi/watendaji wa Halmashauri za wilaya/manispaa za Mkoa wa Lindi na Wawakilishi wa AZAKi katika michakato ya maendeleo.

1. Viongozi/watendaji wa Halmashauri za wilaya/manispaa wametambua kuwa maendeleo ya kweli hayawezi kupatikana pasipo kushirikishwa walengwa na wadau wa maendeleo husika.

2. AZAKi na wawanchi wamefahamu kwamba pasipo ushiriki wao kamilifu katika michakato ya mipango na bajeti za maendeleo itakuwa ni vigumu kufikiwa kwa maendeleo ya kweli na yaliyo endelevu.
Hakuna sababu zozote za tofauti katika mabadiliko yaliyotokana/kuletwa na mradi.

Lessons Learned

Explanation
Kuwepo kwa mahusiano na ushirikiano usioridhisha/ sio mzuri kati ya viongozi/watendaji wa Halmashauri za wilaya/manispaa na wawakilishi wa AZAKi na wananchi kiujumla kuhusu michakato ya sera na maendeleo.

Wananchi hawashirkishwi kikamilifu na ipasavyo katika michakato ya uandaaji wa mipango na bajeti za maendeleo katika ngazi ya vijiji.mitaa, vitongoji, kata na wilaya.
Mipango na miradi ya maendeleo katika Halmashauri za wilaya/Manispaa haitekelezwi kama ipasavyo na sawa na ilivyokusudiwa.
Kukosekana kwa uwazi wa kutosha na uwajibikaji duni kwa viongozi na watendaji wa Halmashauri za wilaya/manispaa za Mkoa wa Lindi.
Wananchi kukosa uelewa juu ya haki na wajibu wao katika michakato ya sera na maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na hivyo kupelekea kuwepo kwa ushiriki duni.
AZAKi nyingi hazina uwezo, maarifa wala mbinu za kufanya ushiwishi na uchechemuzi kuhusu haki na wajibu wa wananchi kushiriki/kushirikishwa katika hatua tofauti za michakato ya kisera na maendeleo kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Challenges

ChallengeHow it was overcome
Viongozi na watendaji wa Halmashauri za wilaya/manispaa kuwa na fikra mgando kwamba wao ndio wanaojua kila kitu na kwamba ndio serikali yenyewe.Kuelimishana na kupeana habari na taarifa kuhusu wajibu na majukumu ya viongozi na watendaji wa Halmshauri katika kuandaa, kutekeleza na kusimamia mipango na bajeti za maendeleo.
AZAKi kutotekeleza wajibu wao wa kuhamasisha na kuelimisha jamii ipasavyo kutambua nafasi, wajibu na haki zao katika michakato ya sera na maendeleo.Kuhamasisha AZAKi kutimiza wajibu wao wa kuelimisha na kuhamasisha jamii katika masuala tofauti ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.
AZAKi kukosa/kuwa na maarifa, mbinu na stadi visivyokidhi haja na mahitaji ya kufanya ushawishi na uchechemuzi kuhusu haki na wajibu wa wananchi kushiriki katika michakato ya sera na maendeleo.Kuelimisha na kuhamasisha AZAKi kujengeana uwezo na stadi za kufanya ushawishi na uchechemuzi wa kudai haki na wajibu wao na jamii katika michakato ya sera na maendeleo.
Kupanda kwa gharama za baadhi ya mahitaji na vifaa muhimu katika utekelezaji wa shughuli za mradi kiufanisi; mf. Vyakula, nauli kwa washiriki n.k.Kununua/kulipia vifaa na/au mahitaji ya utekelezaji wa mradi yanayoendana na bajeti iliyopo kwa kuzingatia ubora na hali halisi iliyopo.
Baadhi ya watendaji/viongozi wa AZAKi kutofahamu vyema malengo ya mradi na matokeo/mabadiliko yaliyokusudiwa na kutarajiwa.Kuelimishana na kuelekezana malengo ya mradi, matokeo/mabadiliko yaliyokusudiwa na kutarajiwa.

Linkages

StakeholderHow you worked with them
Halmashauri za Wilaya na Manispaa LindiKukubali kushiriki katika vikao vya majadiliano na kubadilishana habari na taarifa, ujuzi na uzoefu tofauti kuhusu michakato ya sera na maendeleo katika Hlamshauri ya wilaya husika.
Mkurugenzi Manispaa Lindi na Mkurugenzi Mtendaji - Halmashauri ya Wilaya LindiKufanya ufunguzi rasmi na kutoa nasaha katika vikao vya majadiliano na kubadilishana habari na taarifa, ujuzi na uzoefu tofauti kuhusu uandaaji, utekelezaji, usimamizi na tathmini ya utekelezaji mipango na bajeti za maendeleo za Halmshauri za Wilaya.
Idara za Mipango Halmashauri za Wilaya na Manispaa LindiKuandaa na kuwasilisha mada kuhusu wajibu wa Idata ya Mipango katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo katika wilaya kwa faida na manufaa ya wananchi.
Idara za Maendeleo ya Jamii - Halmashauri za Wilaya na Manispaa LindiKuandaa na kuwasilisha mada kuhusu wajibu wa Idara ya maendeleo ya jamii katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo katika wilaya kwa faida na manufaa ya wananchi.
Waandishi wa Habari na Wawakilishi wa asasi za KiraiaKushiriki mafunzo ya SAM na vikao vya majadiliano na kubadilishana habari na taarifa, ujuzi na uzoefu tofauti kuhusu michakato ya sera na maendeleo katika Halmashauri za wilaya na manispaa husika.

Future Plans

Activities Planned1st Month2nd Month3rd Month
Kuendesha mafunzo ya siku 2 kwa wawakilishi 30 wa AZAKi wa wilaya ya Kilwa juu ya dhana ya Ufuatiliaji Uwajibikaji Kijamii (SAM) ifikapo Desemba, 2011. XX XX
Kufanya ufuatiliaji na tathmini shirikishi ya maendeleo ya utekelezaji mradi katika wilaya ya Kilwa ifikapo Desemba, 2011. XX XX XX

Beneficiaries Reached

    Direct BeneficiariesIndirect Beneficiaries
WidowsFemale1330
Male1538
Total2868
People living with HIV/AIDSFemale918
Male1229
Total2147
ElderlyFemale1433
Male1847
Total3280
OrphansFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
ChildrenFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
DisabledFemale1021
Male1229
Total2250
YouthFemale1639
Male2156
Total3795
OtherFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total140340
(No Response)

Events Attended

Type of EventWhenLessonsActions Taken
Mafunzo ya Usimamizi wa Ruzuku (MYG) 2009Maarifa, mbinu na stadi za kusimamia utekelezaji wa mradi na matumizi ya fedha za ruzuku kwa ufanisi.Kutumia maarifa, mbinu na stadi zilizotolewa kusimamia utekelezaji wa mradi na matumizi ya fedha za ruzuku kiufanisi.
Mikutano ya Upashanaji Habari za Ruzuku toka FCS2005 na 2008Jinsi ya kuandaa na kuwasilisha maandiko miradi yenye sifa, vigezo na ubora unaohitajika na kukubalika na FCS na wadau wengine Kuendeleza jitihada za FCS kujenga uwezo wa AZAKi changa juu ya uandishi wa miradi yenye ubora na vigezo stahili.
Matamasha ya AZAKi 2009 na 2010Umuhimu wa kufanya kazi kwa umahiri na ubunifu mkubwa ili kupata ufanisi na kuleta mabadiliko chanya katika jamii.Kuhamasisha AZAKi kuwa wabunifu na kuchapa kazi kwa umahiri na ustadi mkubwa ili kupata mafanikio makubwa.
Maonesho ya AZAKi Bungeni2006,2007,2008,2009Umuhimu wa kufanya kazi karibu na wabunge ili kuwashawishi mabadiliko katika sera na sheria mbalimbaliKuwashawishi baadhi ya wabunge kuwa karibu na AZAKi ili wasaidiwe katika kutambua na kukabiliana na changamoto za maendeleo katika majimbo yao.
Mafunzo ya kubadilishana uzoefu wa kusimamia miradi ya ruzuku ya kati (MG)2011Kubadilishana maarifa na stadi, ujuzi na uzoefu tofauti katika kusimamia Fedha za Ruzuku ya Kati (MG), Mafanikio, Changamoto na mbinu za utatuzi zilizotumika.Kuwezesha asasi nyingine kupata maarifa na stadi, ujuzi na uzoefu katika kusimamia Fedha za Ruzuku ya Kati (MG)

Attachments

FCS Narrative Report

Introduction

Lindi Non Governmental Organization Network
LINGONET
Kujenga Uwezo na Stadi za AZAKi za Ushawishi na Utetezi na Kuimarisha Uashiriki katika Michakato ya Sera na Maendeleo.
FCS/MG/3/08/95
Dates: Machi 1, 2011 hadi Mei 31, 2011Quarter(s): Kwanza, Mwaka wa Pili
Sharifu Maloya
S.L.P. 92
LINDI
Simu: +255 23 220 2630
Nukushi: +255 23 220 2630
Kiganjani:+255 787 187 008 / +255 712 316 141
Barua Pepe: smaloya22@yahoo.com; smaloya@hotmail.co.uk

Project Description

Policy Engagement
Civil Society Capacity Strengthening
Mradi huu una malengo ya kujenga na kuongeza uwezo wa Asasi za Kiraia (AZAKi) za wilaya 5 za Mkoa wa Lindi za; Liwale, Ruangwa, Nachingwea, Kilwa na Lindi. Mradi unawezesha kujenga uwezo wa viongozi wa AZAKi katika uendeshaji na uendelezaji wa asasi zao kiufanisi kwa kufanya mafunzo kwa viongozi wa AZAKi kimuundo, kiutendaji na kiuendeshaji (Organizational Development). Mradi unawezesha viongozi kutambua dhana na dhima ya AZAKi kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya watu tangu wakati kabala ya ukoloni, wakati wa ukoloni, baada ya uhuru na hatimaye ndani ya mfumo wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa. Pia kuangalia Dira, Dhima, Malengo, Maadili na mambo mengine muhimu kwa ajili ya kuwezesha AZAKi kuendeshwa na kuendelezwa kwa ufanisi.

Vile vile mradi unalenga kuinua na kuboresha uelewa wa AZAKi na jamii kuhusu michakato mbalimbali ya kisera na maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa. Michakato hiyo ni pamoja na uandaaji wa mipango na bajeti za maendeleo, utungaji wa sheria ndogondogo na utoaji wa maamuzi mbalimbali. Imedhamiriwa na kukusudiwa kwamba kwa kufanya hivyo itawezesha kuongeza na kuboreka kwa uelewa na ushiriki wa AZAKi na jamii kiujumla katika michakato husika ya kisera, kisheria na maendeleo kiujumla. Pia kuimarisha na kuboresha ushirikiano na mahusiano baina ya AZAKi kwa upande mmoja na Serikali kwa upande mwingine ili kuhakikisha kwamba wananchi wakiwa walengwa wakuu wa michakato yote wanawezeshwa kupunguza umaskini uliokithiri na kujiletea maendeleo endelevu.
RegionDistrictWardVillagesTotal Beneficiaries
LindiLindi - -480
LindiLiwale - -480
LindiRuangwa - -480
LindiKilwa - -480
LindiNachingwea - -480
 Direct BeneficiariesIndirect Beneficiaries
Female62141
Male78199
Total140340

Project Outputs and Activities

1. Wawakilishi 60 wa AZAKi toka wilaya Liwale na Ruangwa za Mkoa wa Lindi wamejengewa uwezo na uelewa wa maarifa, mbinu na stadi za kufanya Ufuatiliaji Uwajibikaji Kijamii (SAM) katika miradi na shughuli za maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ifikapo Desemba, 2011.

2. Viongozi/watendaji 20 wa Halmashauri za Wilaya/Manispaa na wawakilishi 20 wa AZAKi toka Halmashauri za Wilaya za Liwale na Ruangwa za Mkoa wa Lindi wamejadiliana, kubadilishana habari na taarifa, ujuzi na uzoefu kuhusu uandaaji, utekelezaji, usimamizi na tathmini za miradi na shughuli za maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ifikapo Desemba, 2011.

3. Ushirikiano na mahusiano baina ya viongozi/watendaji wa Halmashauri 2 za wilaya za Liwale na Ruangwa za Mkoa wa Lindi na wawakilishi wa AZAKi vimeimarika na kuboreka ifikapo Desemba, 2011.

4. Ushiriki wa walengwa/wadau katika ufuatiliaji wa maendeleo ya utekelezaji mradi umeongezeka na kuboreka katika wilaya za Liwale na Ruangwa za Mkoa wa Lindii ifikapo Desemba, 2011.
1. Kuendesha mafunzo kwa wawakilishi wa AZAKi 30 juu ya dhana ya Ufuatiliaji Uwajibikaji Kijamii (SAM) kwa siku 2 katika kila wilaya 5 za Mkoa wa Lindi ifikapo Desemba 2011.

2. Kufanya vikao vya siku 1 vya wadau 20 wa maendeleo kati ya viongozi/watendaji wa Halmashauri za Wilaya/Manispaa za Mkoa wa Lindi na wawakilishi wa AZAKi vya kubadilishana habari na taarifa, ujuzi na uzoefu kuhusu uandaaji mipango na bajeti za maendeleo, utekelezaji, usimamizi na tahmini za utekelezaji ifikapo Desemba, 2011.

3. Kufanya ufuatiliaji na tathmini shirikishi walengwa/wadau za maendeleo ya utekelezaji mradi katika Halmashauri za Wilaya/Manispaa 5 za Mkoa wa Lindi ifikapo Desemba, 2011.
1. Viongozi 30 wa AZAKi za Wilaya ya Liwale wamejengewa uwezo na uelewa kuhusu maarifa, mbinu na stadi za kufanya Ufuatiliaji Uwajibikaji Kijamii (SAM) katika miradi na shughuli za maendeleo vinavyotekelezwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa yaliyofanyika mnamo Machi, 2011.

2. Kufanyika kwa kikao cha pamoja cha wadau 20 kati ya viongozi/ watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale na wawakilishi wa AZAKi kujadiliana na kubadilishana habari na taarifa, ujuzi na uzoefu tofauti kuhusu uandaaji, utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya mipango na bajeti za maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kilichofanyika mnamo Machi, 2011.

3. Viongozi 30 wa AZAKi za Wilaya ya Ruangwa wamejengewa uwezo kuhusu maarifa, mbinu na stadi za kufanya Ufuatiliaji Uwajibikaji Kijamii (SAM) katika miradi na shughuli za maendeleo vinavyotekelezwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa yaliyofanyika mnamo Machi, 2011.

4.Kufanyika kwa kikao cha pamoja cha wadau 20 kati ya viongozi/watendaji wa Halmashauri ya Wialya ya Ruangwa kujadiliana na kubadilishana habari na taarifa, ujuzi na uzoefu tofauti kuhusu uandaaji, utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini za mipango na bajeti za maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kilichofanyika mnamo Machi, 2011.

5. Kufanyika kwa ufuatiliaji na tathmini ya maendeleo ya utekelezaji wa mradi kwa kushirikisha walengwa/wadau 40 kwa idadi ya 20 toka kila wilaya za Liwale na Ruangwa uliofanyika mnamo mwezi Mei, 2011.
1. Ndiyo, tofauti iliyopo ni kubadilishwa kwa shughuli ya mradi kutoka ya Kuendesha mafunzo kwa wawakilishi wa AZAKi wa wilaya 5 za Mkoa wa Lindi juu ya Programu ya Maboresho ya Serikali za Mitaa (LGRP) na badala yake kuwa Mafunzo kwa wawakilishi wa AZAKi juu ya dhana ya Ufuatiliaji Uwajibikaji Kijamii (SAM). Hata hivyo kabla ya kufanyika kwa mabadiliko haya Mratibu wa Mradi aliwasiliana na Afisa Programu anayesimamia mradi huu katika FCS, Bi. Rose Kihulya na kutoa idhini ya kutekelezwa kwa shughuli hiyo pasipo kupoteza walengwa na mantiki ya mradi.

2. Katika uombaji fedha za ruzuku robo ya kwanza, mwaka wa pili kulifanyika makosa ya kiufundi kwa kuomba fedha zaidi ya kiasi kilichostahili kwa jumla ya shilingi (TZS.11,420,850/=) ikilinganishwa na shilingi (TSZ. 10,897,000/=) zilizostahili na hivyo kuwepo tofauti ya shilingi (TZS. 523,850/=) kama ziada ambazo zimebakia na zitapunguzwa toka kwenye uombaji wa fedha robo ya pili, mwaka wa pili wa utekelezaji wa mradi.
1. Mafunzo juu ya dhana ya SAM kwa AZAKi za wilaya ya Liwale na Ruangwa (TZS. 4,002,000/=)

2. Vikao vya wadau kati ya viongozi/watendaji wa Halmashauri na AZAKi katika wilaya za Liwale na Ruangwa (TZS. 3,080,000/=).

3. Kufanya ufuatiliaji na tathmini ya maendeleo ua utekelezaji mradi katika wilaya za Liwale na Ruangwa (TZS. 1,470,000/=)

4. Gharama za Utawala na Uendeshaji wa Mradi (TZS. 2,345,000/=).

Project Outcomes and Impact

1. Uwezo na uelewa wa kimaarifa, mbinu na stadi kwa AZAKi za kufanya Ufuatiliaji Uwajibikaji Kijamiii (SAM) umeongezeka.

2. Ushiriki wa AZAKi na jamii katika kufuatilia Uwajibikaji Kijamii (SAM) katika miradi na shughuli za maendeleo katika Halmashauri za wilaya/manispaa unaimarika na kuboreka.

3. Uwajibikaji wa viongozi katika utekelezaji na usimamizi wa miradi na shughuli za maendeleo katika Halmashauri za wilaya/manispaa unaboreka.

4. Uwazi wa viongozi na watendaji wa Halmashauri katika utekelezaji wa miradi na shughuli za maendeleo katika Halmashauri za wilaya/manispaa unaongezeka.

5. Ushirikiano na mahusiano baina ya viongozi/watendaji wa Hlamshauri za Wilaya/manispaa na AZAKi vinaboreka na kuimarika.

6 Upashanaji na upatikanaji wa habari na taarifa za utekelezaji, usimamizi na ufanisi wa mipango na bajeti za maendeleo unaongezeka, kuimarika na kuboreka.
1. Uwezo na uelewa wa AZAKi juu ya dhana ya SAM umeongezeka.

2. Ushiriki wa AZAKi na wananchi katika michakato ya maendeleo umeongezeka na kuboreka.

3. Uwezo wa wananchi kufuatilia uwajibikaji wa kijamii kwa viongozi na watendaji wa Halmshauri za wilaya/manispaa unaimarika na kuboreka.

4. Ushirikiano na mahusiano baina ya wawakilishi wa AZAKi umeboreka.

5. Mahusiano na ushirikiano baina ya viongozi/watendaji wa Halmashauri za wilaya/manispaa na Wawakilishi wa AZAKi katika michakato ya maendeleo vimeimarika na kuboreka.
1. Viongozi/watendaji wa Halmashauri za wilaya/manispaa wametambua kuwa maendeleo ya kweli hayawezi kupatikana pasipo kushirikishwa walengwa na wadau wa maendeleo husika.

2. AZAKi na wawanchi wamefahamu kwamba pasipo ushiriki wao kamilifu katika michakato ya mipango na bajeti za maendeleo itakuwa ni vigumu kufikiwa kwa maendeleo ya kweli na yaliyo endelevu.
Hakuna sababu zozote za tofauti katika mabadiliko yaliyotokana/kuletwa na mradi.

Lessons Learned

Explanation
Kutokuwepo kwa mahusiano na ushirikiano usioridhisha/ sio mzuri kati ya viongozi/watendaji wa Halmashauri za wilaya/manispaa na wawakilishi wa AZAKi na wananchi kiujumla kuhusu michakato ya sera na maendeleo.
Wananchi hawashirkishwi kikamilifu na ipasavyo katika michakato ya uandaaji wa mipango na bajeti za maendeleo katika ngazi ya vijiji.mitaa, vitongoji na kata.
Mipango na miradi ya maendeleo katika Halmashauri za wilaya/Manispaa haitekelezwi kama ipasavyo na sawa na ilivyokusudiwa.
Kukosekana kwa uwazi wa kutosha na uwajibikaji duni kwa viongozi na watendaji wa Halmashauri za wilaya/manispaa za Mkoa wa Lindi.
Wananchi kukosa uelewa juu ya haki na wajibu wao katika michakato ya sera na maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na hivyo kupelekea kuwepo kwa ushiriki duni.
AZAKi nyingi hazina uwezo, maarifa wala mbinu za kufanya ushiwishi na uchechemuzi kuhusu haki na wajibu wa wananchi kushiriki/kushirikishwa katika hatua tofauti za michakato ya kisera na maendeleo kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Challenges

ChallengeHow it was overcome
Viongozi na watendaji wa Halmashauri za wilaya/manispaa kuwa na fikra mgando kwamba wao ndio wanaojua kila kitu na kwamba ndio serikali yenyewe.Kuelimishana na kupeana habari na taarifa kuhusu wajibu na majukumu ya viongozi na watendaji wa Halmshauri katika kuandaa, kutekeleza na kusimamia mipango na bajeti za maendeleo.
AZAKi kutotekeleza wajibu wao wa kuhamasisha na kuelimisha jamii ipasavyo kutambua nafasi, wajibu na haki zao katika michakato ya sera na maendeleo.Kuhamasisha AZAKi kutimiza wajibu wao wa kuelimisha na kuhamasisha jamii katika masuala tofauti ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.
AZAKi kukosa/kuwa na maarifa, mbinu na stadi visivyokidhi haja na mahitaji ya kufanya ushawishi na uchechemuzi kuhusu haki na wajibu wa wananchi kushiriki katika michakato ya sera na maendeleo.Kuelimisha na kuhamasisha AZAKi kujengeana uwezo na stadi za kufanya ushawishi na uchechemuzi wa kudai haki na wajibu wao na jamii katika michakato ya sera na maendeleo.
Kupanda kwa gharama za baadhi ya mahitaji na vifaa muhimu katika utekelezaji wa shughuli za mradi kiufanisi; mf. Vyakula, nauli kwa washiriki n.k.Kununua/kulipia vifaa na/au mahitaji ya utekelezaji wa mradi yanayoendana na bajeti iliyopo kwa kuzingatia ubora na hali halisi iliyopo.
Baadhi ya watendaji/viongozi wa AZAKi kutofahamu vyema malengo ya mradi na matokeo/mabadiliko yaliyokusudiwa na kutarajiwa.Kuelimishana na kuelekezana malengo ya mradi, matokeo/mabadiliko yaliyokusudiwa na kutarajiwa.

Linkages

StakeholderHow you worked with them
Halmashauri za Wilaya za Liwale na RuangwaKukubali kushiriki katika vikao vya majadiliano na kubadilishana habari na taarifa, ujuzi na uzoefu tofauti kuhusu michakato ya sera na maendeleo katika Hlamshauri ya wilaya husika.
Ofisi ya Katibu Tawala (W) ya RuangwaKufanya ufunguzi rasmi na kutoa nasaha katika kikao cha majadiliano na kubadilishana habari na taarifa, ujuzi na uzoefu tofauti kuhusu uandaaji, utekelezaji, usimamizi na tathmini ya utekelezaji mipango na bajeti za maendeleo za Hlamshauri za Wilaya.
Ofisi ya Idara ya Mipango (W) za Liwale na RuangwaKuandaa na kuwasilisha mada kuhusu wajibu wa idata ya Mipango katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo katika wilaya kwa faida na manufaa ya wananchi.
Ofisi za Idara ya Maendeleo ya Jamii (W) za Liwale na Ruangwa.Kuandaa na kuwasilisha mada kuhusu wajibu wa idara ya maendeleo ya jamii katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo katika wilaya kwa faida na manufaa ya wananchi.
Mitandao ya AZAKi (W) za Liwale (ULIDINGO) na Ruangwa (RUANGONET)Kusambaza mialiko, kuandaa kumbi na mawasiliano ya moja kwa moja na walengwa/wadau wa mradi ikiwamo Serikali ngazi ya wilaya na Halmashauri kuhusu utekelezaji wa shughuli za mradi katika maeneo yao.

Future Plans

Activities Planned1st Month2nd Month3rd Month
Kuendesha mafunzo ya siku 2 kwa wawakilishi 30 wa AZAKi wa wilaya ya Lindi juu ya dhana ya Ufuatiliaji Uwajibikaji Kijamii (SAM) ifikapo Desemba, 2011.xxxxxxx
Kufanya vikao vya siku 1 kati ya viongozi/watendaji wa Halmashauri za Manispaa na Wilaya Lindi na wawakilishi wa AZAKi vya kujadiliana na kubadilishana habari na taarifa, ujuzi na uzoefu tofauti kuhusu michakato ya uandaaji, utekelezaji, usimamizi na tathmini za mipango na bajeti za maendeleo ifikapo Desemba, 2011.xxxxxxx
Kufanya ufuatiliaji na tathmini shirikishi ya maendeleo ya utekelezaji mradi katika wilaya ya Lindi ifikapo Desemba, 2011.xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Beneficiaries Reached

    Direct BeneficiariesIndirect Beneficiaries
WidowsFemale1330
Male1538
Total2868
People living with HIV/AIDSFemale918
Male1229
Total2147
ElderlyFemale1433
Male1847
Total3280
OrphansFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
ChildrenFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
DisabledFemale1021
Male1229
Total2250
YouthFemale1639
Male2156
Total3795
OtherFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total140340
(No Response)

Events Attended

Type of EventWhenLessonsActions Taken
Matamasha ya AZAKi2009 na 2010Umuhimu wa kufanya kazi kwa umahiri na ubunifu mkubwa ili kupata ufanisi na kuleta mabadiliko chanya katika jamii.Kuhamasisha AZAKi kuwa wabunifu na kuchapa kazi kwa umahiri na ustadi mkubwa ili kupata mafanikio makubwa.
Maonesho ya AZAKi Bungeni2006, 2007, 2008, 2009Umuhimu wa kufanya kazi karibu na wabunge ili kuwashawishi mabadiliko katika sera na sheria mbalimbaliKuwashawishi baadhi ya wabunge kuwa karibu na AZAKi ili wasaidiwe katika kutambua na kukabiliana na changamoto za maendeleo katika majimbo yao.
Mikutano ya Upashanaji habari za ruzuku toka FCS2005 na 2008Jinsi ya kuandaa na kuwasilisha maandiko miradi yenye sifa, vigezo na ubora unaohitajika na kukubalika na FCS na wadau wengine Kuendeleza jitihada za FCS kujenga uwezo wa AZAKi changa juu ya uandishi wa miradi yenye ubora na vigezo stahili.
Mkutano kuhusu Jukwaa la Katiba Tanzania2011Umuhimu wa kusoma Katiba ya Muungano na kuelewa marekebisho tofauti (14) yaliyokwisha kufanyikaKuhamasisha AZAKi kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uandaaji wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mafunzo ya Usimamizi wa Ruzuku (MYG)2009Maarifa, mbinu na stadi za kusimamia utekelezaji wa mradi na matumizi ya fedha za ruzuku kwa ufanisi.Kutumia maarifa, mbinu na stadi zilizotolewa kusimamia utekelezaji wa mradi na matumizi ya fedha za ruzuku kiufanisi.

Attachments

 

Email address: lingonetlindi@yahoo.co.uk
Phone number: +255 23 220 2630,0784860372
Street address: JENGO LA PRIDE,BARABARA YA JAMHURI,JIRANI NA BENKI YA CRDB,CHUMBA NAMBA 8&9

Mailing address: 

P.O.BOX 92 LINDI

Contact name:

KHAMIS CHILINGA
Contact title: KATIBU MTENDAJI

Lindi non governmental organisation network ilianzishwa kama Mtandao wa asasi za kiraia wa wilaya mwaka 2002 kufuatia warsha ya asasi za kiraia 13 za wilaya ili kubaini na kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazokabili sekta ya AZAKi katika kufikia malengo yao.kwa msaada mkubwa wa shirika la kigeni lijulikanalo kama THE CONCERN WORLDWIDE Lindi non governmental organisation network(LINGONET) ilianzishwa na kusajiliwa rasmi mwaka 2003 na kupata cheti cha ithibati(certicate of compliance) mwaka 2010

Saidi Kawanga, Mhasibu

                                                                            

 

 

 

 

 

                        Khamis Chilinga, Katibu Mtendaji

Bi Esha Salum ,Mwenyekiti wa LINGONET

.LINGONET inaendeshwa kwa taratibu za uanachama,asasi yoyote iliyosajiliwa katika sheria za NGOs inaweza  kuomba na kuingia uanachama wa LINGONET

malengo makubwa ya LINGONET ni kujenga uwezo wa asasi katika wilaya ya LINDI,kuratibu shughuli zao ili kuepuka muingiliano wa shughuli na kujenga uwezo wa jamii katika kuandaa,kupanga na kutekeleza miradi ya maendeleo na uchambuzi wa sera

LINGONET imefanya shughuli kadhaa katika kujenga sekta ya AZAKi katika wilaya ya Lindi tangu kuanzishwa kwake kwa ufadhili wa mashirika mbalimbali kama ifuatavyo;

(i) Mradi wa CODEP ambao ulilenga kujenga uwezo wa asasi za kiraia katika kushirikiana na kuboresha mahusiano na wadau wengine wakiwepo serikali kwa ufadhili wa THE CONCERN

(ii) Mradi wa kujenga mitandao ya wilaya katika mkoa wa Lindi mwaka 2006-2007 kwa ufadhili wa The Foundation for civil society

(iii) mradi wa kujenga uwezo wa AZAKi na wananchi katika ushawishi na utetezi juu ya     uchambuzi wa sera.mwaka 2009-2012 kwa ufadhili wa The Foundation for civil society

(iv) mradi wa haki na usawa wa kiuchumi unaofadhiliwa na SIDA kupitia kwa SAVE THE CHILDREN kwa miaka maradi ambao unalenga kujenga uwezo wa watoto katika kutambua na kudai haki zao kupitia mabaraza ya watoto yaliyoundwa katika kata na wilaya zote za wilaya za Kilwa ,Lindi  na Ruangwa mradi huu ni wa miaka minne

LINGONET inapata viongozi wake kupitia uchaguzi inaofanyika mara moja kila baada ya miaka mitatu ambapo viongozi wafuatao huchaguliwa

(1) Mwenyekiti

(2) Makamu mwenyekiti

(3) Katibu mtendaji

(4) Katibu msaidizi

(5) Mweka hazina

(6) Wajumbe saba(7)

LINGONET imeweza kuratibu uanzishwaji wa mtandao wa mkoa wa lindi LINDI ASSOCIATION OF NGOs(LANGO) kupitia mradi wake wa kujenga uwezo wa mitandao na kwa sasa inafanya kazi ya kujenga uwezo wa asasi ili ziweze kujiendesha kwa ufanisi na kufikia malengo yao katika kuhudumia jamii

LINGONET inaratibu mradi wa haki na usawa kiuchumi katika wilaya tatu za mkoa wa Lindi,mradi ambao unatekelezwa katika wilaya saba za Tanzania za Temeke,Kilwa,Ruangwa,Lindi,Same,Handeni na Arusha kwa ufadhili wa SIDA kupitia SAVE THE CHILDREN

Hadi hivi sasa LINGONET ina wanachama 23 na maombi kadhaa yanapitiwa kamati tendaji,LINGONET ni mtandao ambao umejijengea jina katika jamii.

Picha kubwa juu ni jengo ilipozaliwa LINGONET mwaka 2002,picha kubwa chini ni Mwenyekiti wa kwanza wa LINGONET Mr Said Kawanga,chini yake ni washiriki wa moja ya mafunzo ya LINGONET chini yake ni Mwenyekiti wa sasa wa LINGONET Bi Esha Salum na mwisho chini ni Katibu Mtendaji wa sasa wa LINGONET Mr Khamis Chilinga