Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

ONGEZEKO LA MAAMBUKIZI YA VVU/UKIMWI

Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (Geita)
January 19, 2013 at 6:41 PM EAT

 Kwa nini maambukizi ya VVU/UKIMWI kwa nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara yanazidi kuongezeka kila kuchapo ingawa kuna juhudi kedekede zinazofanywa na serikali pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali?

Tukutane (Geita)
January 19, 2013 at 11:21 PM EAT
Maambukizi ya VVU/UKIMWI yanazidi kuongezeka kila kuchapo kwa sababu:- 1: Umaskini. 2: Elimu ya namna ya kuzuia na kujikinga haijawakolea wadau. 3: Mila na desturi potofu zinachangia kwa kiasi fulani mfano ukeketaji, kurithi wake nk. 4: Uwepo wa mazingira hatarishi yanayoamsha na kuchochea ari ya kufanya mapenzi, mfano kumbi za starehe, migodi nk.
Mjamaa (mwanza)
March 5, 2013 at 11:50 AM EAT

kuna sababu moja mimi naiona kuba sana.USIRI wa ukimwi unaowekwa na muusika wa umimwi na nchi mana ikumbukwe kwamba siku za hivi karibuni vijana wengi wamekuwa wakijiua mara tu wanapojua ni waasirika lakini swali linakuja kwanini wanaamua kujiua?Mimi nasema ni kwasababu ya mazingira magumu ya usiri yanayowekwa yaliyomfanya yeye kwanza kuupata ukimwi.Hakutegemea mpenzi wake ni muasirika ndio mana akalala nae hali iliyompa naye ukimwi.Je,ni haki kuendelea kufanya ukimwi siri ya mwenye nao na daktari hali tunajua madhara yanayoletwa na kufanywa hivyo mfano kwa mafataki,mashuleni nk.Lakini ni kweli kwamba mtu akijulikana ana ukimwi hatakubalika katika jamii?na hatapendwa kama wengine?Mimi nasema hapana ,yote hayo ni uongo.Ukimwi usiwe jambo la siri tenaaaa!


Add New Message (Hide)

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.