Fungua
MWELA THEATRE GROUP DAR-ES-SALAAM

MWELA THEATRE GROUP DAR-ES-SALAAM

TEMEKE,DSM,Tanzania

MAJUKUMU YA SERIKALI ZA MITAA.

 

Halmashauri za Manispaa zimeanzishwa chini ya sheria za Mamlaka za Miji (Local Government Urban Authorities Act. 1982).
Majukumu makuu ya Serikali za Mitaa yaliyofafanuliwa na sheria hiyo ni kama ifuatavyo:-

  • Kusimamia na kudumisha amani ulinzi na usalama katika maeneo ya mipaka yake.
  • Kuhamasisha/kuendeleza na kuwapatia huduma bora za kijamii na kiuchumi wananchi walio katika eneo la mipaka ya Halmashauri.
  • Kusimamia sera za maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika maeneo yao.
  • Kuchukua hatua madhubuti za kuhifadhi na kuendeleza mazingira.
  • Kusimamia utawala, fedha, mambo yote ya uendeshaji katika ngazi mbalimbali zilizo ndani ya mamlaka ya Halmashauri ya Manispaa/Jiji.
  • Kusimamia na kuhakikisha demokrasia inadumishwa katika jamii.
  • Kukusanya mapato yatakayowezesha mamlaka ya serikali ya mtaa kuendesha shughuli zake pamoja na kutoa taarifa za matumizi kupitia kamati mbalimbali.
  • Kutoa huduma mbalimbali za kiuchumi na kijamii pamoja na kutekeleza shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
  • Kuzingatia na kutambua masuala mtambuka kama vile Jinsia (accord due recognition to and, promote, gender awareness).
  • 10. Kuendeleza na kusimamia kanuni za biashara, viwanda, kilimo n.k.
  • 11. Kusimamia na kuendeleza huduma za Afya, Elimu, Maji, Utamaduni na masuala ya burudani katika jamii.
  • 12. Kubuni mikakati ya kupambana na umaskini pamoja na mbinu za kusaidia kuboresha maisha ya vijana, wazee, walemavu n.k.

 

Utawala bora ni swala linalotekelezwa na halmashauri zote katika nyanja za:

•  Demokrasia

•  Ushirikishwaji

•  Utawala wa sheria

•  Uadilifu wa viongozi na wafanyakazi wa Serikali za mitaa

•  Uwazi na Uwajibikaji

•  Ufanisi katika utendaji kazi

•  Mchakato wa kijinsia

•  Upangaji mipango

•  Ujuzi wa upangaji Mipango kwa kutumia Rasilimali zilizopo

large.jpg

hiki ni cheti cha mwenyekiti wa mwela fikiri m mvugaro alipo udhulia semina ya jinsi ya kutengeneza muziki mafunzo yalioandaliwa na Music Crssroads

large.jpg

mwenyekiti wa mwela theatre na mwanakijiji mmoja na mwandishi wa habari wakipigwa picha ya pamoja katika ofisi za mwela theatre jijini dar-es-salaam

large.jpg

mjumbe wa mwela theatre na waandishi wa habari wa japan katika picha ya pamoja katika ofisi za mwela theatre jijini dar-es-saalaam

large.jpg

mjumbe wa mwela theatre katika picha ya pamoja na mwandishi wa habari wa japan katika ofisi za mwela theatre group jijini dar-es-salaam

large.jpg

mwenyekiti wa mwela theatre akiwasindikiza waandishi wa habari kutoka kwenye ofisi za mwela theatre group.kuelekea katika shughuli zingine za kulijenga taifa

large.jpg

mwenyekiti wa mwela theatre akiwa na mwandishi wa habari wa japan wakipiga picha ya pamoja kwa furaha ya ujio wao katika ofisi za mwela theatre group nchini tanzania.

large.jpg

mwenyekiti wa mwela theatre na waandishi wa habari wa japan pamoja na watoto katika picha ya pamoja inje ya ofisi za mwela theatre group nchini tanzania.

large.jpg

mwenyekiti wa mwela theatre group akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari wa japan kabla ya kuondoka nchini mwao huko japan.

large.jpg

mjumbe wa mwela theatre group akiwa katika semina iliyoaandaliwa na taasisi nchini tanzania.