Injira
MWELA THEATRE GROUP DAR-ES-SALAAM

MWELA THEATRE GROUP DAR-ES-SALAAM

TEMEKE,DSM,Tanzania

Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

MAJUKUMU YA SERIKALI ZA MITAA.

 

Halmashauri za Manispaa zimeanzishwa chini ya sheria za Mamlaka za Miji (Local Government Urban Authorities Act. 1982).
Majukumu makuu ya Serikali za Mitaa yaliyofafanuliwa na sheria hiyo ni kama ifuatavyo:-

  • Kusimamia na kudumisha amani ulinzi na usalama katika maeneo ya mipaka yake.
  • Kuhamasisha/kuendeleza na kuwapatia huduma bora za kijamii na kiuchumi wananchi walio katika eneo la mipaka ya Halmashauri.
  • Kusimamia sera za maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika maeneo yao.
  • Kuchukua hatua madhubuti za kuhifadhi na kuendeleza mazingira.
  • Kusimamia utawala, fedha, mambo yote ya uendeshaji katika ngazi mbalimbali zilizo ndani ya mamlaka ya Halmashauri ya Manispaa/Jiji.
  • Kusimamia na kuhakikisha demokrasia inadumishwa katika jamii.
  • Kukusanya mapato yatakayowezesha mamlaka ya serikali ya mtaa kuendesha shughuli zake pamoja na kutoa taarifa za matumizi kupitia kamati mbalimbali.
  • Kutoa huduma mbalimbali za kiuchumi na kijamii pamoja na kutekeleza shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
  • Kuzingatia na kutambua masuala mtambuka kama vile Jinsia (accord due recognition to and, promote, gender awareness).
  • 10. Kuendeleza na kusimamia kanuni za biashara, viwanda, kilimo n.k.
  • 11. Kusimamia na kuendeleza huduma za Afya, Elimu, Maji, Utamaduni na masuala ya burudani katika jamii.
  • 12. Kubuni mikakati ya kupambana na umaskini pamoja na mbinu za kusaidia kuboresha maisha ya vijana, wazee, walemavu n.k.

 

Utawala bora ni swala linalotekelezwa na halmashauri zote katika nyanja za:

•  Demokrasia

•  Ushirikishwaji

•  Utawala wa sheria

•  Uadilifu wa viongozi na wafanyakazi wa Serikali za mitaa

•  Uwazi na Uwajibikaji

•  Ufanisi katika utendaji kazi

•  Mchakato wa kijinsia

•  Upangaji mipango

•  Ujuzi wa upangaji Mipango kwa kutumia Rasilimali zilizopo

3 Nzeli, 2011
« Inyuma Ahakurikira »

Tanga igitekerezo

Izina ryawe:
Aho uherereye
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.