MAJUKUMU YA SERIKALI ZA MITAA.
|
|
Halmashauri za Manispaa zimeanzishwa chini ya sheria za Mamlaka za Miji (Local Government Urban Authorities Act. 1982). Majukumu makuu ya Serikali za Mitaa yaliyofafanuliwa na sheria hiyo ni kama ifuatavyo:-
- Kusimamia na kudumisha amani ulinzi na usalama katika maeneo ya mipaka yake.
- Kuhamasisha/kuendeleza na kuwapatia huduma bora za kijamii na kiuchumi wananchi walio katika eneo la mipaka ya Halmashauri.
- Kusimamia sera za maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika maeneo yao.
- Kuchukua hatua madhubuti za kuhifadhi na kuendeleza mazingira.
- Kusimamia utawala, fedha, mambo yote ya uendeshaji katika ngazi mbalimbali zilizo ndani ya mamlaka ya Halmashauri ya Manispaa/Jiji.
- Kusimamia na kuhakikisha demokrasia inadumishwa katika jamii.
- Kukusanya mapato yatakayowezesha mamlaka ya serikali ya mtaa kuendesha shughuli zake pamoja na kutoa taarifa za matumizi kupitia kamati mbalimbali.
- Kutoa huduma mbalimbali za kiuchumi na kijamii pamoja na kutekeleza shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
- Kuzingatia na kutambua masuala mtambuka kama vile Jinsia (accord due recognition to and, promote, gender awareness).
- 10. Kuendeleza na kusimamia kanuni za biashara, viwanda, kilimo n.k.
- 11. Kusimamia na kuendeleza huduma za Afya, Elimu, Maji, Utamaduni na masuala ya burudani katika jamii.
- 12. Kubuni mikakati ya kupambana na umaskini pamoja na mbinu za kusaidia kuboresha maisha ya vijana, wazee, walemavu n.k.
|
Utawala bora ni swala linalotekelezwa na halmashauri zote katika nyanja za:
• Demokrasia
• Ushirikishwaji
• Utawala wa sheria
• Uadilifu wa viongozi na wafanyakazi wa Serikali za mitaa
• Uwazi na Uwajibikaji
• Ufanisi katika utendaji kazi
• Mchakato wa kijinsia
• Upangaji mipango
• Ujuzi wa upangaji Mipango kwa kutumia Rasilimali zilizopo
3 Nzeli, 2011