Andulile Raphael
Mwenyekiti.
Wasifu wake: Ni Mtakwimu Mwandamizi ambaye ametumikia katika nyadhifa mbalimbali za utumishi wa umma kwenye Wizara, Idara na wakala wa serikali. Ni mhamasishaji stadi.
Adam Gwankaja
Katibu Mkuu.
Ni mwalimu na mwanaharakati wa maendeleo ya binadamu. Ametumikia katika nafasi mbalimbali akiwa mwalimu, mkuu wa shule, hadi kufikia kuwa mchambuzi wa sera na mtumishi mwandamizi kwenye mashirika ya kitaifa na ya kimataifa. Ni mwandishi habari, mtafiti, mhariri na mhakiki wa kazi za fasihi.
Adam Exavery
Mweka Hazina.
Ni mhitimu na mtumishi mzoefu katika masuala ya uhasibu. Ametumikia na amejipatia uzoefu katika kusimamia fedha za miradi toka kwa wafadhili kwenye mashirika ya kitaifa na kimataifa.
Edson Mwaibanje
Mratibu wa Programu
Ni kiongozi na mhamasishaji jamii mzoefu. Kabla ya kujiunga katika sekta ya maendeleo, Mwaibanje ametumikia katika nafasi mbali mbali za kisiasa (chama na serikali). Kwenye mashirika yasiyo ya kiserikali, ametumikia katika nafasi mbali mbali za uongozi ikiwemo kuwa mwenyekiti wa mtandao wa asasi zisizo za kiserikali mkoani Mbeya (MBENGONET)