Envaya

TAMA

Discussions

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

TOA MAONI: KATIBA TUITAKAYO TANZANIA

Tanzania Agricultural Modernization Association (Bukoba)
July 2, 2012 at 10:32 PM EAT (edited July 2, 2012 at 10:39 PM EAT)

Salaam ndugu zangu wana Kagera na Watanzania kwa ujumla.

Kuanzia tarehe 2.7.2012, mkoa wa Kagera hasa Wilaya ya Biharamulo, wananchi wilayani humo wameanza kutoa maoni yao katika kata ya Kalenge na Movata katika Mchakato wa Katiba Mpya. Tume ya Mabadiliko ya Katiba itaendelea kukusanya maoni ya wana Kagera katika wilaya ya Ngara (6.7.2012), Karagwe (9.7.2012), Kyerwa (12.7.2012), Misenyi (16.7.2012), Bukoba DC (19-21/7/2012), Bukoba MC (22-25/7/2012) na Muleba (26-29/7/2012). Kila Wilaya Tume itatumia wastani wa siku 4 na watafanya mikutano na wananchi katika wastani wa kata 6-8. Katika Manispaa ya Bukoba, mikutano itafanyika kata/maeneo ya Rwamishenye, Bilele, Nyanga, Kahororo, Hamugembe, Nyamkazi, Bakoba na Kibeta.

Kazi hii inaendelea kufanyika si tu Mkoani humu bali nchi nzima kwa mfumo huu.

RAI YANGU
Kwa niaba ya Asasi ya Kijamii ninayoisimamia ya Tanzania Agricultural Modernization Association (TAMA) ambayo moja ya malengo yake ni ushawishi na utetezi wa haki za kiraia na utawala bora miongoni mwa jamii ya watanzania, nachukua fursa hii kukaribisha maoni na mawazo yenu juu ya KATIBA TUITAKAYO. Maoni haya kwa niaba ya wana Kagera na Watanzania kwa ujumla tutafanyia kazi na hata kuyawasilisha kwa Wajumbe wa Tume kama Asasi ili yachambuliwe, yatathminiwe na kutumiwa kama maoni huru ya wanakagera na watanzania katika kuandaa Katiba Mpya tuitakayo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, nichukue fursa hii kuwaombeni Asasi zetu kuhamasisha wananchi kushiriki mikutano hiyo ili kutoa maoni yao moja kwa moja kwa wajumbe wa Tume.

Ahsanteni na Karibuni sana.

Imetolewa na, Paschal M. Paschal Nchunda KATIBU MTENDAJI - TAMA.
02.07.2012


Add New Message

Invite people to participate