IDARA YA HALI YA HEWA YATAHADHALISHA WAKAZI WA MABONDENI
Wakati matatizo ya awali yaliyowapata wananchi waishio mabondeni kutokana na mafuriko hayajapatiwa ufumbuzi , hasa wakazi wa Keko mwanga Magulumbasi A na B ,Mission kizinga msikitini ,Tabata Kisukuru na wengineo ,tahadhali imetoka katika idara ya hali ya hewa kwamba kutakuwepo na madhala makubwa kutokana na mvua za vuli zitakazonyesha kwa muda mfupi.Hii ni pamoja na kuwepo kwa magonjwa ya mlipuko kama maralia, kipindupindu na magonwa mengineyo,hivyo tunaomba hatua za haraka zichukuliwe ili familia hizo ziweze kunusurika na janga lililoko mbele yetu.
MAMBO TULIYOJUMUISHA KWA WIKI HII.
kwanza kabisa tunaishukuru serikali kwa kumaliza mgomo wa ma daktari uliodumu takribani wiki tatu.Hii imetufundisha kuwa katika kudai haki ni lazima uchukue hatua zinazokubalika ili chombo husika kiweze kutambua suala husika
tumeshuhudia watu walioathirika kwa kiasi kikubwa ni wanawake na watoto,kwani asilimia kubwa ya watoto wanaolazwa ni akina mama ndio wanao wajibika kuwauguza na akina baba wakiwa katika shughuli zao nyingine .Hivyo tunaiomba serikali kushughulikia migogoro mapema baina yake na makundi mbali mbali ili kunusuru akina mama na watoto.
Migomo ni dalili ya ukosefu wa haki na usawa wa mgawanyo wa rasilimali tulizonazo,kwa hali hiyo asasi za kijamii na wanaharakati mbali mbali wanatakiwa kufanya kazi ya kuelimisha wananchi na jamii kwa ujumla ili kufahamu haki na usawa wa rasilimali tulizonazo pamoja na mgawanyo wake uko vipi.
Tunaishukuru serikali na wadau mbalimbali ambao kwa pamoja wameweza kufanikisha zoezi la ujenzi wa maema ya familia takribani 289 katika eneo la Mabwepande lilotengwa kwa ajili ya wahanga wa mafuriko na kugawa viwanja kwa familia zilizokuwa hazijapatiwa ,hii imekamilishwa tarehe 6 februari 2012 . Vile vile kukamilisha ujenzi wa ghala la kuhifadhia chakula na misaada pia ujenzi wa shule kuendelea kwa kasi.
Wakati zoezi hili likiendeshwa kwa ufanisi ,bado tumeshuhudia familia nyingine zilizopata matatizo sawa na zile zilizopo Mabwepande ziikitelekezwa katika maeneo yake ya athari. Hii ni kutokana na kasumba iliyojengeka kuwa wilaya ya Kinondoni ni ya watu wa hali ya juu kuliko wilaya zingine ikifuatiwa na Ilala. Wilaya ya Temeke ikiwa ni ya mwisho katika mkoa wa Dar es salaam.Dhana hiyo imesababishia wahanga wa Keko, Mission Mbagala ambao ni wakazi wa wilaya ya Temeke kutofikiwa na vyombo vya habari ,hivyo kusahaulika katika zoezi hili ,na kubakia wakiendelea kuteseka katika maeneo yao. Kutokana na tatizo hili tunaomba serikali na wadau mbalimbali , mashirika ya kimataifa ,watu binafsi, makampuni na wasamalia wema kuingilia kati suala hili ili kunusuru maisha ya wananchi hao.
DHIMA YETU ni Kuwa na jamii yenye usawa na isiyobagua katika nyanja zote ,kiuchumi,kisiasa na kijamii na inayojumuisha makundi yote(kila raia )wa Tanzania.
DIRA YETU ni
Kutengeneza mikakati itakayoibua na kutetea haki za binadamu,wanawake na watoto kwa kuwajengea uwezo uhamasishaji mawasiliano , na kuwa na mahusiano na serikali na vyombo visivyo vya ki serikali kitaifa na kimataifa
Katika majumuisho ya wiki hii,tumugundua sababu kubwa zinazosababisha migogoro isiyoisha inayoikumba serikali yetu ya Tanzania.Hii ni kutokana na tabia za watanzania ambao wamezoea kulalamika bila kuchukua hatua,vile vile watanzania tuna kasumba ya kusahau.Kutokana na sababu hizi watanzania tuamke ,tuwajibike ,kwa kuchukua hatua kwa kufika mahali husika ,tupeleke ujumbe na hoja zetu kwa maandishi ili malalamiko yetu yawe na kumbukumbu ,kwani haki haipatikani bila kuipigania na hatima ya maisha yetu yapo mikononi mwetu wenyewe .
Wito wetu kwa asasi za kijamii ni kuwaomba tuwajibike kwa pamoja ili kuelimisha jamii {kuijengea uwezo jamii} kuanzia ngazi ya famili , mtaa n.k ili tuunde nguvu ya pamoja itakayoondoa mifumo mibovu ya uongoziwa wa nchi yetu ambayo insababisha matatizo yasiyo kwisha kwa kila sekta ,mfano elimu ,afya. na nyingine nyingi.Kwa kuwajengea uwezo wananchi watadhibiti siasa katika sehemu za utendakazi.
Dar es Salaam Flooding Community Survey
nguo za familia ya watu 7 zimepotea, ukuta wa nyumba umeathirika kwa maji yaliyo dumu kwa siku 20.pesa taslim laki mbili za karo ya shule ya mtoto wangu kupotea
Before flooding: masaa 2 | Now: masaa2 |