Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

FAMILIA NNE(4) ZAKOSA MAHALI PAKUISHI.

kufuatia mvua kubwa  iliyonyesha tarehe 11 .04 .2012 jijini Dar es salaam imesababisha maafa makubwa katika maeneo mbalimbali ya jiji ikiwemo wakazi wa Mission Msikitini Mbagala  wilaya ya Temeke kukosa makazi baada ya nyumba zao kubomoka kutokana na mvua hizo.Tawa imethibitisha hali hii baada ya kutembelea eneo hili na kujionea tafalani kubwa zilizosababishwa na maji.Wakazi hawa wanailalamikia serikali kwa kutowafikia na kuwapa msaada kwani hata maafa ya mafuriko ya kwanza yaliwakumba na hakuna aliyewapa msaada wakazi hawa wa Mission Msikitini.Pamoja na kuwatembelea wakazi hao wakati wa maafa ya mafuriko ya mwanzo na kuainisha matatizo yao hakuna hatua iliyochukuliwa , hivyo tunaomba taasisi binafsi ,mashirika mbalimbali ,kitengo cha maafa na watu binafsi kwa pamoja kusaidiana ili maisha ya familia hizi yaweze kunusurika.

Picha hapo chini  zinaonyesha matukio mbalimbali yaliyotokea siku ya wanawake duniani,huu ni mkutano uliojumuisha wanachama wa asasi yetu ili kujadili maedeleo ya kazi za asasi kwa ujumla.Vilevile tulikuwa na taarifa mbalimbali za ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto wa kike.