Juu ya ukurasa wa Hariri Tovuti ( ) ni sehemu ya Andika Habari, ambayo inakuruhusu kwa urahisi kuchapisha taarifa mpya za shirika lako za habari, picha, na hati katika ukurasa wa Habari wa tovuti yako kwenye Envaya.
Kuandika taarifa ya habari, chapa habari ambayo ungependa kuichapisha katika boksi kubwa nyeupe. Unaweza pia kwa urahisi "copy and paste" maandiko kutoka kutoka mahali pengine, kama vile hati ya Microsoft Word.
Kama ungependa kuchapisha picha au faili za hati zozote katika taarifa yako ya habari, bonyeza Fungia picha au Fungia hati na kufuata maelekezo ili kuchagua picha au faili kutoka kwenye kompyuta yako.
Ambapo wewe ni tayari kuchapisha habari yako kwenye tovuti yako, bonyeza kitufe cha Chapisha.
Ifuatayo: Kuhariri Kurasa kwenye Tovuti yako
Iliyotangulia: Kuhariri Tovuti Yako