Asasi yetu ya Epa-ukimwi inakusudia kuzitumia sherehe za krismasi na mwaka mpya kama sehemu ya kufikisha ujumbe mpya wa kuitaka jamii kujitathmini toka kipindi cha sherehe zilizopita 2011 hadi sasa. Hii itasaidia jamii kuweza kuona ni kwa jinsi gani imeweza kushiriki katika mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya ukimwi. Sambamba na hilo kipindi hiki pia kitatumika kwa kutoa elimu kwa mangariba na manyakanga wanaosimamia taratibu na mila za tohara na unyago kwani kipindi hiki cha uvunaji wa korosho shughuli hizo hufanyika kwa kiwango kikubwa. Misaada mbalimbali toka kwa wadau wa asasi itahitajika katika kusukuma mbele jukumu hilo muhimu. Pia suala la kupitia katiba ya Tanzania linafanywa na wana asasi ili kutoa maoni yao na kuchangia katika mchakato wa marekebisho ya katiba unaoendelea hapa nchini.
17 Ukuboza, 2012