Envaya

large.jpg

Mheshimiwa Freeman Mbowe(kiongozi wa kambi rasimi ya upinzani Bungeni),akisaini daftari la wageni mbele ya mkurugenzi mtendaji Ndg Meshack Masanja na Chrispine Ferdinand(Program Officer,Mzeituni Foundation) katika banda la Mzeituni Foundation wakati wa maonesho ya ASASI ZA KIRAIA,bungeni Dodoma mwezi May/2013.Maonesho ambayo yalifunguliwa rasimi na Mh;Anna Makinda Spika wa Bunge la Jamhuri th 28/05/2013 na kufungwa na naibu waziri wa Maendeleo ya jamii th 30/05/2013

large.jpg

Ndugu Martine Mziba,afisa wa Idara ya maji akifungua kikao kifupi na kuwatambulisha wageni kutoka wizara ya maji  na ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI walipokuwa katika kitongoji cha KIZULE kata ya Ngoma jana 14/06/2013 eneo ambalo Mzeituni Foundation kwa kushirikiana na idara ya maji wamekuwa wakitekeleza zoezi la usajili wa vyombo vya watumiaji maji. Jumuiya ya watumiaji maji KIZULE wamekuwa mfano mzuri kwani kwa pamoja na kwa kushirikiana na wananchi wameweza kujiwekea kanuni na taratibu za chombo chao.

large.jpg

Hapa ni Engineer Maganga kutoka SNV-Mwanza aliyekuwa ameambatana na timu kutoka Wizara ya maji na Ofisi ya waziri mkuu serikali za mitaa  iliyofika wilayani Ukerewe katika kuona mafanikio ya jumuiya za watumiaji maji zilizoanzishwa na kusajiliwa kwa mujibu wa sera na sheria ya Maji. Timu ya Maji na usafi wa mazingira ya halimashauri ya wilaya ya Ukerewe wamewezesha baadhi ya vyombo vya watumiaji maji kuanzishwa. Tukio hili lilifanyika Ijumaa ya tarehe 14/06/2013 katika kitongoji cha KIZULE kata ya Ngoma.

large.jpg

Team ya Mzeituni Foundation ikijiandaa kwa maonesho asubuhi ya siku ya pili(29th may 2013),katika viwanja vya Bungeni,mjini Dodoma.

large.jpg

Mkurugenzi Mtendaji wa Mzeituni Foundation bwana Meshack Masanja akifurahia kitu na Chrispine F.Mabwenga wote kutoka Mzeituni,walipokuwa wakihudhuria kikao mjini dodoma,siku moja kabla ya Ufunguzi wa Maonyesho ya AZAKI,wakipata maelekezo na utaratibu namna watavyoendesha shughuri zao kesho yake,maelezo haya yakitolewa na mmoja wa watumishi wa Ofisi ya Spika.

large.jpg

Hii ni meza kuu ikiwa tayali kumsubili mgeni rasimi Mh.Anne Makinda(Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania),katika hotuba ya ufunguzi wa MAONESHO YA ASASI ZA KIRAIA(AZAKI),bungeni DODOMA yaliyofanyika tarehe 28-30/may/2013 katika viwanja vya bunge.

large.jpg

Washiriki mbalimbali wa MAONESHO YA AZAKI BUNGENI DODOMA,wakipita katika mabanda ya wenzao kuona na kujifunza kupitia kazi zinazofanywa na Asasi hizo.

Muda wa siku tatu za maonesho ulikuwa wa kufana maana kupitia kuwaonesha wabunge wa Bunge letu la Jamhuri ya muungano kazi zetu tumezidi kuwaonesha ni namna gani sisi kama AZAKI tunao mchango mkubwa katika kuleta MAENDELEO ya Taifa letu la Tanzania.

large.jpg

Baadhi wa wanakamati wa kamati ya ufuatiliaji wa rasilimali za umma kata ya muriti wakiwa katika mkutano wa kuelezea shughuli zao siku walipotembelewa na uongozi wa Forum Syd Tanzania Tarehe 27/07/2011

large.jpg

Bw:Godfrey Wawa Country Program Manager wa Forum Syd Tazania akiwa na Afisa mradi wa social accountabili ukerewe Mwanza pamoja na Afisa ufuatiliaji na tathimini wa forum syd Miss Marta kwenye ufuatiliaji wa mradi wa SAPT (Social Accountability Program Tanzania)Tarehe 27/07/2011

large.jpg

Mwalimu Kondola wa shule ya msingi Nansio akiwa anatoa maelekezo kwa wanafunzi wake wenye ulemavu wa mtindio wa ubongo na wasioona siku hiyo ambayo uongozi wa Mzeituni ulikwenda kuwakabidhi madawati .Tarehe 19/7/2011