Siku ya mjadala wa utoaji maoni ya rasimu ya katiba mpya katika hoteli ya DABUYA tarehe 3-4/8/2013. Mjadala huu uliandaliwa kwa ushirikiano wa Mzeituni Foundation na CHAWATA Mkoa wa Mwanza,na kuwaleta pamoja wawakilishi wa walemavu kutoka makundi mbalimbali katika wilaya za Magu,Ukerewe,Karagwe,Ilemela na Nyamagana. Mjadala ulifunguliwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Walemavu Tanzania Mkoa wa Mwanza.Katika ufunguzi wake mwenyekiti aliwahimiza na kusisistiza washiriki kutazama swala la Katiba kwa upana na kuepuka kuzungumzia ulemavu binafsi au kulalamika.Aidha aliongeza kuwa ni vyema kuwawakilisha kikamilifu maelfu ya kundi la walemavu ambao hawakupata muda wa kushiriki katika mkutano huo. Mwenyekiti alitoa angalizo kuwa katika mjadala ni muhimu wote kuweka pembeni itikadi binafsi za kisiasa au kidini na kila mshiriki atambue amehudhuria kwa hali yake ya ulemavu na si vinginevyo. Washiriki walipata fursa ya kujitambulisha kwa majina,taasisi ,mahali wanapotokea na hali yao ya ulemavu. HIYO NI PICHA YA BAADHI YA WASHIRIKI WAKISHIRIKI KATIKA MJADALA.
7 Kanama, 2013