Injira
JUMUIYA YA WANAFUNZI WALIOSOMA SKULI ZA JIMBO LA UZINI (JUWASSU)

JUMUIYA YA WANAFUNZI WALIOSOMA SKULI ZA JIMBO LA UZINI (JUWASSU)

Zanzibar, Tanzania

Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

How can we improve the education sector at Uzini?

JUMUIYA YA WANAFUNZI WALIOSOMA SKULI ZA JIMBO LA UZINI (JUWASSU)
27 Gashyantare, 2012 at 13:45 EAT
  • To improve and facilitate uzinis community for making the higher standards of education and other development corner.
  •  To support primary and secondary student during preparation time, examination and fields period schools at uzini area.
  • Reduce and stop the transmission of HIV/AIDs, MALARIA, T.B, CHOLERA and stand by giving out FREE CARE CLINIC for Zanzibar new generation.
  • Educate and eliminate there duties, rights and responsibilities.
  • To establish the project strategy, policy and support small business union and  private sector.
  • To prepare and participate in the workshop, seminar, short-course class, vocational training and field in a work-place.
  • Making co-ordination and friendship of the government, non-government organization, parastatal, institution, donors and other sponsors/supports either by individual or by group.
  • Contract, advice and consult the community and supporters within or outside the country in built the educational center and other infrastructure.
  • To have an competent nursery, primary and secondary schools by quality and quantity with comfortable environment
JUMUIYA YA WANAFUNZI WALIOSOMA SKULI ZA JIMBO LA UZINI (JUWASSU)
27 Gashyantare, 2012 at 21:29 EAT

kwa nini sisi wazaliwa wa jimbo la uzini tunashindwa kufanya mageuzi ya elimu ndani ya jimbo letu la uzini wakati tunaweza kufanya mageuzi ya kisiasa na kuitwa jimbo mama kisiasa lakini tunaitwa jimbo tasa kielimu

MZALIWA JIMBO LA UZINI (JIMBO LA UZINI )
27 Gashyantare, 2012 at 22:22 EAT

mageuzi ya kielimu tutaweza kufanya kwa kuiunga mkono juwassu kwani vijana wamejitolea kwa ajili ya maendeleo ya elimu ndani ya uzini.kwani huko nyuma hatukuweza kufanya mageuzi kwakua hatukua na chombo kinachoweza kutuunganisha lakini sasa tuna juwassu ambayo inaweza kutuunganisha na kuleta mabadiliko cha muhimu hapa nikuunganisha nguvuzetu wanauzini popote tulipo kwani umoja ninguvu hongereni juwassu na msichoke kwani safari ya meli 1000 inaanza na hatua moja. hata ROME haikujengwa kwa siku moja pia mbuyu ulianza kama mchicha.@JUMUIYA YA WANAFUNZI WALIOSOMA SKULI ZA JIMBO LA UZINI (JUWASSU): 

Madu wa maendeleo (Uzini)
28 Gashyantare, 2012 at 04:37 EAT

MDAU WA MAENDELEAO UZINI.

Kwa muda mrefu sasa jimbo la uzini limekuwa nyuma katika suala la ELIMU,licha ya kwamba Jimbo hilo lina skuli iliyojengwa zamani tokea enzi za ukoloni kama sikosei shule hiyo ya UZINI imejengwa 1936.Ni skuli chache zilizojengwa katika miaka hiyo ikiwa ni pamoja na Ndijani kwa Wilaya ya kati,Makunduchi na Muyuni kwa Kusini Unguja.

Skuli ya Uzini imebahatika kutoa wasomi wengi ambao wamehudumu katika nafasi mbali mbali katika Serikali ya SMZ na SMT.Hata hivyo kwa kipindi kirefu sasa kada ya Elimu jimbo la uzini kwa imekuwa inasuwasuwa licha ya kuongezeka kwa skuli nyingi ikiwa ni pamoja na KIBOJE,BAMBI,UMBUJI,MPAPA,MCHANGANI NA GHANA.Skuli ambazo ni msingi na sekondari hadi sekondari ya juu.Hata hivyo sekta hiyo haina mafanikio kwa sasa kwani watoto wengi wamekuwa wakiishia kidato cha pili ambayo ndiyo elimu ya lazima na baada ya hapo vijana wengi imekuwa hawana la kufanya na matokeo yake kuwa wanazurura tu.

Nimefarajika kuona kuna JUMUIYA HII YA JUWASSU ambayo inajishughulisha na maendeleo ya ELIMU kwa vijana wa Uzini,pengine Jumuiya hii inaweza ikawa chachu ya maendeleo ya ELIMU UZINI.Inaweza kutoa mchango mkubwa katika kuleta mapinduzi ya ELIMU Uzini.

Hata hivyo najuwa jumuiya hii najuwa inachangamoto nyingi sana .Kwanza ni suala la "Recognition".Hapa nakusudia ili jumuiya iweze kufanya kazi ni lazima iwe imekubalika kwa walengwa na hapo ndipo itakapopata"LEGITIMACY" ya kufanya kazi zake sawa.Suala jengine ni Uwezo wa kujiendesha kwa jumuiya hii,hapa namaana uwezo wa kifedha wa jumuiya kwani bila ya fedha hakuna kinakachofanyika.Suala jengine ni Moyo wa kujitolea kwa wahusika pamoja na jamii inayohudumiwa .Vilevile suala la kuungwa mkono na jamii inayohudumiwa ni muhimu sana kwani bila ya hilo kazi hiyo haitakuwa na mafanikio kwani lengo ni kuwasaidia vijana hivyo jamii ya vijana hao lazima ikubali.

Ombi langu kwa wanauzini,nikwamba kuikubali jumuiya hiyo kwa kuiunga mkono ili iweze kufanya kazi zake kama ilivyokusudia.Pia kutafuta mbinu za kuiwezesha kifadha ili kazi zilizokusudiwa zisikwame.Vile tuwe tayari kuhimiza vjana wetu na kuhimizana wenyewe kwa wenyewe ili kuhakikisha tunaiwezesha jamuiya kufanya kazi ya kuwasaidia vijana hao katika sekta hiyo ya elimu .Vijana tuwe tayari kushiriki kikamilifu katika mikakati ya jumuiya hiyo ili malengo yaweze kufikiwa hasa ukitilia maanani kuwa sisi ndio walengwa.

MWISHO NISEME UZINI ITAJENGWA NA WANA UZINI,HATUJACHELEWA,TOA  MCHANGO WAKO ILI KUFIKIA MLENGO.

HEKO JUWASSU,MSIKUBALI KURUDI NYUMA.

 

 

Machano (Zanzibar)
23 Mutarama, 2014 at 15:49 EAT

@JUMUIYA YA WANAFUNZI WALIOSOMA SKULI ZA JIMBO LA UZINI (JUWASSU): 


Andika ubutumwa

Tumira abandi mu kiganiro