Envaya

Wananchi wa kijiji cha Nyamhoza wamemshikiria mwenyekiti wao wa kijiji kwa tuhuma za kula fedha za pemebeo za kilimo ambapo alishirikiana na kamati ya vocha ya kijiji kula fedha hizo.Aidha mtendaji wa kijiji hicho ameshatoroka na hadi sasa hajulikani aliko. Juhudi hizi zimefanyika kupitia mradi wetu wa ufuatiliaji wa matmizi ya umma.

Habari nyingine tulizozipata wakati wa ufuatiliaji na tathimini ya mradi kutoka kijiji cha Kirando mwenyekiti wa kijiji hicho amepigiwa kura ya kutokuwa na imani naye hasa baada ya kubainika kwamba alitumia milioni 9 za kijiji kununua mashine yake ya kusoza jambo ambalo lilibainika wakati wa zoezi la ufuatiliaji wa matumizi ya umma katika kijiji hicho.

Wakati hayo yakiendelea katika vijiji hivyo huko Sunuka wananchi walichukua hatua za kumhoji mheshimiwa diwani juu ya taarifa za ujenzi wa hosteli katika shule yao ya kata kwa thamani ya shilingi 220,000,000/= ambapo hadi sasa msingi haujachimbwa kabisa licha ya kuwa mwaka wa fedha kwa ajili ya kazi hiyo unakwisha june mwaka huu. Aidha Diwani huyo alikiri kuwepo kwa bajeti hiyo katika mwaka huu wa fedha na kueleza kuwa muda si mrefu mkandarasi ataanza kufanya kazi hiyo. Lakini kama si kufanyika kwa mradi huu hakuna aliyekuwa na taarifa juu ya ujenzi huo.

14 Februari, 2011
Ifuatayo »

Maoni (1)

(Afahamiki) alisema:
Baada ya changamoto zilizotolewa na maradi huu wa ufuatiliaji wa uwajibikaji kijamii sasa halmashauri ya wilaya ya Kigoma imeanza kubandika kwenye mbao za matangazo taarifa za mapato na matumizi ikiwa ni pamoja na bajeti za kila mwaka kwenye kila kata.Hii imeonekana katika kata ya Mwandiga na mtendaji wa kata hiyo amekiri kwamba taarifa hizo zimeletwa siku mbili zilizopita kwani ilionekana wakaguzi kutoka ofisi ya CAG na wale wa maboresho ya serikali za mitaa walikuwa mbioni kuja kukagua namna ambavyo wananchi wanashirikishwa katika kufanya maamuzi.
5 Machi, 2011

Ongeza maoni

Jina lako:
Mahali ulipo:
Email yako:
(sio lazima)
Anwani yako ya email haitachapishwa.