Wasaidizi wa sheria(Emmanuel Alphonce na Samwel Joseph) wakimsikiliza Mwl.Mkuu wa shule ya Msingi Nyakato "C" iliyoko Manispaa ya Musoma wakati akito changamoto zinazowakabili wanafunzi katika shule yake ikiwa ni pamoja na wanafunzi kukosa malezi bora kutoka kwa wazazi/walezi wao katika suala la elimu.
Emmanuel Gervas, Mwanasheria(Kutoka Centre for Widows and Children Assiatance- CWCA) akitoa mafunzo juu ya sheria mbali mbali za nchi na utawala bora yaliyofanyika katika Manispaa ya Musoma kwa wasaidizi wa sheria kutoka katika Manispaa ya Musoma na Vijijini.
Emmanuel Alphonce(Msaidizi wa sheria kutoka MMPO) akitoa elimu ya sheria juu ya Haki za binadamu kwa watoto wa shule ya Msingi Nyarigamba "B" iliyoko katika Manispaa ya Musoma.
Mosi Mtatiro(Msaidizi wa sheria kutoka MMPO) akitoa elimu ya sheria juu ya Haki za binadamu kwa watoto wa shule ya Msingi Nyarigamba "A" iliyoko katika Manispaa ya Musoma.