NURU CLUB
TAARIFA YA MAFUNZO YA YA UJASILIA MALI
May 2010
YALIYOMO
1. Utangulizi
2 Lengo kuu la mradi
3 Madhumuni
4 Walengwa.
5 Utambuzi wa washiriki.
6. Mada zilizofundishwa
7 . Wawezeshaji
8. Mafanikio.
9 . Matatizo yaliyoibuka /changamoto.
10 Mambo tuliyojifunza/kugundua.
11. Matarajio.
12 Mabadiliko yaliyojitokeza
NURU
NURU CLUB
.
MRADI WA HAKI YA MWANANCHI
TAARIFA YA YA MAFUNZO YA UJASILIA MALI
KWA WATU 35 YALIYOFANYIKA KIWALANI
MAY 2010
Utangulizi
NURU CLUB ni asasi ya watu wanaoishi na VVU/UKIMWI,asasi hii ni mdau kwenye kutekeleza mradi wa haki za mwananchi unaoisimamiwa na shirika la AMREF chini ya ufadhili wa shirika la nchini Uingereza lijulikanalo kama DFID.
Mradi huu unafanyika katika kata tatu ambazo ni Kiwalani iliyopo Ilala , Tandale na Manzese zilizopo katika wilaya ya Kinondoni.
Mafunzo haya ni mwendelezo wa mafunzo yaliyofanyika mwaka jana ambapo tulitakiwa kutoa mafunzo kwa watu 75 lakini hatukuweza kufikia idadi hiyo kwa sababu fedha iliyokuwa imetengwa kwenye shughuli hiyo ilikuja pungufu haikutosheleza hivyo ilitubidi kutoa maafunzo kwa watu 45 na wale waliobaki 35 ndio tumewapatia mafunzo kwenye robo ya mwisho na kufikia idadi ya waliofikiwa kuwa 80.
LENGO KUU LA MRADI WA HAKI ZA MWANANCHI:
Ni kuboresha upatikanaji wa huduma za afya ,matibabu pamoja na matunzo kwa watu wanaoishi na VVUna UKIMWI na wale wanaoathiriwa wa UKIMWI hasa wanawake ,viziwi pamoja na wale wanaofanya biashara za ngono.
Katika kutekeleza mradi huu asasi ya NURU iliendesha mafunzo ya siku mbili ya ya ujasilia mali kwa watu 35. Mafunzo haya yalifanyika katika kata KIWALANI ambapo washiriki walitoka kwenye kata husika.Tuliweza kufundisha wanawake 25 na wanaume 20
LENGO KUU LA MAFUNZO YA UJASILIAMALI-
Kuwajengea waviu uwezo wa kusimamia na kuendesha biashara ndogondogo kwa lengo la kuwasaidia kujikwamua kiuchumi kwa kutumia rasilimaili na fursa zinazopatikana kwa mfano mikopo midomidogo. Lengo lingine ni kuwajengea uwezo ili waweze kuwa na mbinu za kubuni na kuanzish na kuisimamia miradi yao.
MADHUMUNI YA MAFUNZO;
Kuwajengea WAVIU uwezo na mbinu mbalimbali za kuweza kuibua,kubuni na kuzisimamia biashara zao kitaalamu.
WALENGWA
Ni watu wanaoishi na VVU na UKIMWI kutoka katika kata 3 za Tandale, Manzese na Kiwalani ambako ndiko mradi unakotekelezwa.Uchaguzi wa washiriki wa mafunzo haya uliwalenga zaidi wale waliokuwa na biashara zao ndogondogo,ili waweze kupata mafunzo na waweze kuendesha biashara zao kwa ufanisi zaidi.
UTAMBUZI WA WASHIRIKI ULIVYOFANYIKA.
NURU CLUB kushirikiana na viongozi wa PTCs ndogondogo 12 tuliweza kuchambua kutoka kwenye daftari la majina ya wanachama wa asasi yetu na kufanikiwa kupata majina ya washiriki wote kwa uwiano sawa kulingana na sehemu mradi ulikolenga.Utaratibu huu tunao siku nyingi na umekuwa ukitoa mafanikio mazuri sana Register yetu ina jina la kila mwanachama ,namba yake ya simu,kata aliyotoka na wilaya.
MAFUNZO YALIYOFANYIKA.
NURUCLUB iliandaa mafunzo ya ujasilia mali kwa siku mbili na tulifundisha watu 35, wakiwemo wanawake 20 na wanaume 15.
MADA ZILIZOFUNDISHWA.
1.Jasilia mali ni nani?
Hapa tuliwawezesha wanawarsha kuweza kuelewa wajasilia mali ni akina nani ambapo tuliona kuwa neno ujasiliamali kiujumla lina maanisha kujitolea,kukubali kuanzisha shughuli mpya ambazo ni za kibunifu na kivumbuzi.
2.Kwa nini watu huwa wajasilia mali?
Tuliwawezesha kujua sababu zinazopelekea watu kuwa wajasilia mali ambapo tuliona ni ili kuinua vipato na kuondokana na hali duni ya maisha
.
3.Jinsi gani ya kuwa mjasilia mali hapa tuliwaelimisha kuhusu tabia wajasilia mali ambapo tabia hizo ni kujiamini wenyewe,kuwa na msimamo,wabunifu na wavumbuzi,wenye bidii na wenye uwezo wa kubadilisha mipango na malengon
4 .Dhana au wazo zuri la ujasilia mali
Waliwezeshwa namna ya kutambua na kubuni mbinu mbalimbali za kiujasiliamali
5.Hatua za kufuata ili mtu kuwa mjasilia mali. Hapa waliwezesha kutambua hatua mbalimbali za kufuata ili kuwa wajasilia mali
WAWEZESHAJI WA MAFUNZO
Mafunzo haya yaliwezeshwa na wafuatao:-
1 Elizabeth sangu Mshauri /TOT
2. Fortunata Lyuki Mshauri/TOT
Wawezeshaji hawa wamepatiwa mafunzo mbalimbali kupitia program za AMREF ,PASADA na chuo cha biashara (CBE) ambapo hawa ni TOTs kwenye mambo ya HIV/AIDS.
MAFANIKIO
Watu 35 wamepatiwa elimu ya ujasiliamali ambayo itawasaidia katika kubuni biashara na kuziendesha na kuzisimamia kitaalam.
Mafanikio mengine tuliyoyapata baada ya mafunzo ya awali ni kwamba wanachama wa NURUCLUB wamepata mwamko na wameanza kuomba tufanye utaratibu wa kuanzisha mfuko wa vicoba.
MATATIZO YALIYOJITOKEZA
Wenzetu wa wilaya ya Temeke waliweza kudai kushiriki kwenye mafunzo kwani wote ni wanachama wa NURU..
MAMBO TULIYOGUNDUA.
Tuligundua kwamba watu wengi wanaendesha biashara zao bila utaalamu kitu ambacho kinapelekea biashara nyingi kutokuwa endelevu au kuyumba yumba.
Pia tumegundua watu wanategemea kupata mitaji mikubwa ili waweze kuendesha biashara,kumbe biashara huweza kuanza kwa mtaji mdogo na kuendelea kukua hadi mtaji uwe mkubwa
Vilevile tumebaini ya kwamba wengi hawana mitaji kwa ajili ya biashara, wengi wanabangaiza ,kutokana na mafunzo haya tumegundua kwamba wakiwezeshwa wataweza kuendesha biashara kitaalamu zaidi.
MATARAJIO YETU;
Kuona kwamba watu wanaoishi na VVU/UKUMWI wanakuwa na uwezo wa kuanzisha na kusimamia biashara zao kwa lengo la kupunguza umaskini ambapo hali hiyo itachangia kupunguza hali ya utegemezi ambayo mara nyingi husababisha unyanyapaa.
Vilevile tunatarajia kwamba watu wanaotumia ARVs watakuwa na uwezo wa kupajipatia chakula cha kutosha ambapo kitasaidia katika kutumia dawa vizuri na kuimarisha afya zao,watakuwa wafuasi wazuri wa dawa kutokana na elimu waliyopata. Na pia nguvu kazi ya Taifa itaongezeka.
Pia tunatarajia kwamba elimu tuliyofundisha itawasaidia kwenda kutafuta mikopo sehemu mbalimbaali kwa lengo la kuimarisha mitaji yao na kuweza kuisimamia vizuri, biashara zao
Pia tunatarajia kuanzisha mfumo wa benki ya Jamii VICOBA kwa lengo la kusaidia kuondokana na ugumu wa upatikanaji wa mikopo kutoka kwenye mabenki mengine ambayo yana masharti magumu.
MABADILIKO YALIYOJITOKEZA.
Mwanzoni tulikuwa tumelenga kutoa mafunzo kwa watu 75,lakini kutokana na sababu tulizozieleza hapo mwanzo hatukufikia idadi hiyo, hivyo tulifanikiwa kufikia watu 45,na wale waliobakia 35 ndio tumewapatia mafunzo sasa.

Maoni (1)
MRADI WA HAKI ZA MWANANCHI
NURU CLUB
TAARIFA YA TAMASHA LA UELIMISHAJI JAMII `JUU YA UPIMAJI WA HIARI , UNYANYAPAA,UNYANYASAJI PAMOJA NA HAKI ZA WATU WAISHIO NA VVU/ UKIMWI
MAY 2010
YALIYOMO uk:
1. Utangulizi……………………….…3
2 Lengo kuu la mradi…………….…3
3 Madhumuni………………………4
4 Walengwa. ………….……………4
5 Shughuli zilifanyika… …….……..4
6 . Mbinu zilizotumika………..…..…5
8. Waelimishaji……………….……..5
9 Mafanikio………………….……..6
10 Matatizo………………………..…7
11. Mambo tuliyojifunza ………...….8
12 Matarajio…………..……………8
NURU CLUB
MRADI WA HAKI YA MWANANCHI
TAARIFA YA TAMASHA LA UELIMISHAJI JAMII JUU YA UPIMAJI WA HIARI , UNYANYAPAA,UNYANYASAJI PAMOJA NA HAKI ZA WATU WAISHIO NA VVU/ UKIMWI. MAY 2010.

Ni kuboresha upatikanaji wa huduma za afya ,matibabu pamoja na matunzo kwa watu wanaoishi na VVUna UKIMWI na wale wanaoathiriwa na UKIMWI hasa wanawake ,viziwi pamoja na wale wanaofanya biashara za ngono.
Katika kutekeleza mradi huu asasi ya NURU iliendesha mafunzo ya siku mbili ya jinsi ya kuishi kwa matumaini kwa watu 75. Mafunzo haya yalifanyika katika kata tatu ambapo mradi unalenga.Tuliweza kuwafundisha wanawake 53 na wanaume 22.
LENGO LA MATAMASHA YALIYO FANYIKA:.
Kwanza kabisa ni kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa kupima afya hasa tukilenga upimaji wa hiari wa VVU.
Pili kuelimisha jamii juu ya athari na madhara yanayoweza kusababishwa na unyanyapaa na unyanyasaji wa aina yeyote kwa mtu yeyote lakini tukitia msisitizo zaidi kwa watu wanaoishi na VVU/UKIMWI ,
Tatu kuelimisha juu ya haki na wajibu kwa jamii juu ya suala la ukimwi pia kuwafahamisha juu ya sheria mpya ya UKIMWI ya mwaka 2008
MADHUMUNI YA TAMASHA:-
Kuchangia Kuondoa / kupunguza / kutokomeza unyanyapaa na ubaguzi miongoni mwa wanajamii ili kuboresha upatikanaji wa haki hasa kwa watu wanaoishi na VVU NA UKIMWI.
WALENGWA
Wananchi wa kata za Kiwalani ,Manzese na Tandale pamoja na watu wanaoishi na VVU na UKIMWI waliopo katika eneo la mradi.
SHUGHULI ZILIZOFANYIKA:-
A.Kutoa elimu kwa jamii
MADA ZILIZOFUNDISHWA.
1.Umuhimu wa kupima VVU, hapa tulielezea faida na hasara zake.
Hapa mafunzo yalilenga zaidi ukweli kuhusu swala zima la ugonjwa wa ukimwi kuanzia njia za maambukizi,njia za kujikinga,tulifundisha haya ili kumpa mtu nafasi ya kufanya maamuzi yaliyo sahihi
2.Madhara ya unyanyapaa /unyanyasaji.
Hapa tuelezea maana ya unyanyapaa pamoja na aina za unyanyapaa.
3. Tulizungumzia suala la haki na wajibu kwa jamii pamoja na kwa watu wanaoishi na VVU/UKIMWI.
Hapa tulifundisha haki za msingi za watu wanaoishi na VVU / UKIMWI,tulieleza kwamba kupata maambukizi ya VVU hakuzuii haki za msingi kwa binadamu yoyote.
Tunaposema haki za binadamu ni pamoja na haki ya kuishi, kuheshimiwa , kupata watoto , kuoa na kuolewa,kumiliki mali,kwenda kokote unakota,kuishi popote,haki ya kupata matibabu, pamoja na kushiriki kwenye mambo yote yanayohusu jamii bila kubaguliwa au kuvunja sheria.
4. Tuliangalia sheria ya UKIMWI ya mwaka 2008 sehemu ya 7 na ya 8 sehemu ambazo zinazungumzia juu ya unyanyapaa pamoja na haki na wajibu kwa jamii pamoja na watu wanaoishi na VVU/UKIMWI.
Mbinu zilizotumika kufundishia ;
1. Kuwezesha, kuelezea mada
2. Kuuliza na kuulizwa maswali.
3. Mashindano ya kucheza kiduku ambapo yalivutia watu wengi sana.
4. Watu wanaoishi na VVU kutoa shuhuda kuelezea historia zao tangia walipotambua afya zao.
Waelimishaji kwenye tamasha
1. Elizabeth sangu Mshauri /TOT
2. Msafiri thomas Mshauri /TOT
Wawezeshaji hawa wamepatiwa mafunzo mbalimbali kupitia program za AMREF,PASADA, HPI(health policy initiative) ambapo hawa ni TOTs kwenye mambo ya HIV/AIDS.
B. Upimaji wa VVU wa hiari.
Tulifanya matamasha mawili makubwa moja katika Wilaya ya Ilala kata ya Kiwalani na tamasha lingine lifanyikia Wilaya ya Kinondoni likihusisa kata za Tandale na Manzese. Shuguli hii ilitoa mafanikio yafuatayo hapa chini:-
Kiwalani tulitoa elimu kwa watu wapatao 1000.
Waliopima ni watu 232, Wanawake 92 na Wanaume 140.
Waliokutwa wana maambukizi ya VVU ni wanawake 11 na wanaume 12 ambapo idadi yao ni watu23.
Tandale na Manzese tulitoa elimu kwa watu takriban 1500 na kati yao 206 walipima VVU ambapo wanaume walikua 127 na wanawake 79.Maambukizi ya VVU yalikuwa kama ifuatavyo :-Wanawake 7 na wanaume 6 walioonekana wana maambukizi ya VVUna kufanya idadi ya wenye maambukizi kuwa 13.
Kwa ujumla kwenye matamasha yote mawili tulitoa elimu kwa watu 2500. Waliopima ni 438 wakiwemo wanawake 171 na wanaume 267. Waliokutwa wana maambukizi ni 36 wakiwemo wanawake 18 na wanaume 18.
WALIOKUWA WANATOA HUDUMA YA UPIMAJI NI :-
Washauri nasaha wawili kutoka Angaza Zaidi wakishirikiana na washauri wawili kutoka NURUCLUB ambao ni :-Elizabeth Sangu na Fortunatha Lyuki.
Mafanikio / Changamoto / matatizo
MAFANIKIO
1.Kwa Kupitia matamasha haya tumeweza kuamsha hisia za wengi ambao walikuwa hawaelewi lolote kuhusu haki na wajibu walionao katika jamii,hivyo wameweza kujitokeza na kuuliza maswali mengi na hatimaye kufikia maamuzi ya kwenda kupima afya zao.
2.Mafanikio mengine ni pamoja na mwitikio wa watu kuja kupima ambapo kwa matamasha yote mawili tuliweza kutoa elimu kwa watu 2500 ambapo waliopima ni 438 wakiwemo wanawake 171 na wanaume 267. Waliokutwa wana maambukizi ni 36 wakiwemo wanawake 18 na wanaume 18.
3.Watu waliohudhuria walipata elimu mbalimbali iliyotolewa hivyo wakaweza kutambua mambo ambayo hawakuwa wanayaelewa ikiwemo haki na wajibu wa jamii ,unyanyapaa na unyanyasaji kuhusiana na masuala ya ukimwi.
4.kiongozi wa serikali ya mtaa wa Yombo Kiwalani Ndugu Ignas Maembe alipata nafasi ya kuzungumza na wananchi na kuwaasa kuhusu kuzingatia elimu iliyotolewa pia akawaomba wajitunze kwani hali ya maambukizi inazidi kuongezeka.Pia aliwaonya wale ambao wanawaambukiza wenzao kwa makusudi waache tabia hiyo mara moja kwani kufanya hivyo ni kurudisha nyuma harakati za mapambano dhidi ya UKIMWI.
MATATIZO YALIYOJITOKEZA
1.Wenzetu wa wilaya ya Temeke waliweza kudai kushiriki kwenye mafunzo kwani wote ni wanachama wa NURU.
2.Tulishindwa kufanya shughuli kulingana na mpango kazi kutokana na kucheleweshewa fedha na mfadhili
3.Kulikuwa na mfumuko wa bei hivyo kulitikisa kidogo bajeti yetu.
4.Baadhi ya washauri nasaha wa Angaza zaidi walikataa kusaidiana na NURUCLUB kwenye zoezi la upimaji kwa sababu malipo yalikuwa ni madogo.
4.Baadhi ya viongozi wa serikali hawakutoa ushirikiano wa kutosha hata baada ya kuwapatia taarifa rasmi ya shughuli zilizokuwa zinatekelezwa ndani ya mitaa yao kuhusu mradi wa haki za mwananchi..
MAMBO TULIYOJIFUNZA / KUGUNDUA.
1.Tumegundua kwamba katika eneo la Kiwalani,Manzese na Tandale kuna watu wanaofanya biashara ya ngono na wasenge.
2.Tumegundua kwamba jamii ikipelekewa huduma ya elimu na upimaji wa VVU karibu hujitokeza kwa wingi zaidi kuliko kufuatilia huduma hiyo kwenye vitu maalumu.
3.Masuala ya imani za dini zinakwamisha harakati za mapambano dhidi ya UKIMWI.
MATARAJIO YETU/MAPENDEKEZO.
Kutokana na uzoefu tulioupata tungependa kurudia baadhi ya shughuli tulizotekeleza kwenye mradi mwaka huu kwenye mwaka ujao kutokana matokeo yake kuwa na manufaa makubwa na wanajamii kuomba turudi tena kwa ajili ya huduma kama hiyo.

TUNAENDESHA TAMASHA LA KUHAMASISHA JUU YA HAKI ZA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI PAMOJA NA UKIMWI KATIKA KATA TATU KWENYE WILAYA MBILI ZA ILALA NA KINONDONI, AMBAPO KINONDONI TUPO VIWANJA VYA BAARESA, NA ILALA TUPO VIWANJA VYA RELINI KWA ALLY MBOA. VILEVILE TUNAENDESHA MAFUNZO YA UJASILIAMALI KWA WATU WANAOISHI NA VVU/UKIMWI KATIKA KATA YA KIWALANI KWA SIKU TATU.