Envaya
Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Icyongereza. Edit translations

Kwa miaka mingi, saratani imekuwa ni gonjwa ambalo limewatesa wengi na kusababisha vifo vingi nchini.

Sababu hasa ni asilimia kubwa ya Watanzania kutokuwa na uelewa hasa wa gonjwa hili, pamoja na namna ya kupunguza uwezekano wa kulipata na kwamba likigundulika mapema, linaweza kutibika.

Sababu nyingine ni kutokuwepo na idadi ya kutosha ya wataalamu wa kutosha kutoa elimu hii, pamoja na serikali kutoyapa kipaumbele mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukizwa kwa muda mrefu hapo awali.

Tanzanian Cancer Society inaundwa kwa kiasi kikubwa na wataalam wa tiba ya saratani ambao wamejitolea kuhakikisha Watanzania wanaelewa nini maana ya Saratani na njia zote za kuiepuka, na hata atakayelipata gonjwa hili, apate elimu na huduma za kutosha kuboresha afya yake kadiri inavyowezekana.