Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

1.Tosa inafanya kampeni za vita dhidi ya malaria kwa kutoa elimu kwaenye shule za msingi na sekondari ,zahanati ,vituo vya afya na jamii kwa kushirikiana na wahudumu wa afya wa kujitolea (wakala wa mabadiliko ya tabia ) katika kata zote wilayani nyamagana kwa kushirikiana na madiwani.watendaji wa kata,watendaji wa mitaa,waalimu na wafanyakazi wa idara ya afya kwenye zahanati na vituo vya kutolea huduma.

2.Tosa inahamasisha wajawazito kuwahi kilinki mapema wanapojijua wana mimba ili kupata huduma na vipimo kama inavyoonyeshwa kwenye kadi ili kupunguza vifo vya wajawazito.

3.tosa inatoa sare na karo za shule kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

4.Tosa inatoa elimu ya ujasiriamali kwa wajane

 

 

tosa inafanya kazi katika shule za msingi kwa kushirikiana na waalimu na viongozi wa mitaa ili kupata habari sahihi kuhusu watoto wanaohitaji kufadhiliwa na shirika letu

tosa pia inafanya uchunguzi ili kujua wahitaji walio na hali ngumu zaidi na kuwapa kipaumbele.pia inafatilia afya za watoto hao kwa karibu na  mahitaji ya chakula inapotokea uhitaji huu.

tosa inatajia kuwasiliana na RITA ili watoto yatima  na wanaoishi kwenye mazingira hatarishi wasajiliwe ili wapewe vyeti vya kuzaliwa.

kuendelea na kampeni za malaria kwa kufanya matamasha katika shule za msingi na kugawa vyandarua kwa wajane,watoto yatima na jamii zenye kipato kidogo

kuendelea kuwaelimisha jamii juu ya haki za wajane  na watototo yatima kwa kupitia

vipeperushi,mikutano,makongamano na vyombo vya habari.