Asili (Kiswahili) | Kiswahili |
---|---|
Jumuiya ya The Poultry Farmers Development Organization (POFADEO) ni jumuiya ya wafugaji iliyoanzishwa na wafugaji wakishirikiana na baadhi ya wataalamu wa mifugo. Jumuiya hii ilianzishwa kwa lengo la kuandaa mazingira bora ya ufugaji ili wafugaji hususan wa kuku na jamii za ndege waweze kuendeleza shughuli zao za ufugaji kwa ufanisi zaidi. Jumuiya ya POFADEO tangu kuasisiwa kwake miaka kumi iliyopita, imefanya kazi nzuri ya kuwashajiisha wafugaji kuendeleza shughuli za ufugaji kwa kuzingatia kanuni bora za ufugaji ili kuboresha uzalishaji katika mifugo yao. POFADEO inatumia wataalamu waliomo katika jumuiya hiyo kuawapatia taaluma wafugaji kuhusu umuhimu wa kuchanja mifugo yao, ulishaji bora wa kuku katika umri tofauti, utotoaji bora wa vifaranga, kujikinga na magongwa mbali mbali na mambo mengineo. MAFANIKIO YALIYOPATIKANA jumuiya ya POFADEO tangu kuasisiwa kwake imefanya mambo mabli mbali kama vile kutoa taaluma ya utawala bora kwa wajumbe wa kamti za masheha katika shehia mbali mbali za wilaya Wete, Chake chake, Micheweni na Mkoani (wilaya nne za kisiwa cha Pemba). Mradi huu uligharamiwa na shirika la The Foundation for Civil Society (FCS) ambapo jumla ya shilingi ishirini na moja, ishirini na nane elfu na mia mbili (21,028,200/=) zilitumika katika kufanikisha mradi huo. Miradi mingine iliyofadhiliwa na shirika la The Foundation For Civil Sciety ni mradi wa kuijengea uwezo jumuiya ya POFADEO kuhusu utawala bora ambapo jumuiya ilipata jumla ya shilingi milioni tano (5,000,000/=). POFADEO vile vile iliweza kutoa mafunzo kwa wafugaji kuhusu ufugaji bora wa kuku wa asili kutokana na ufadhili wa shirika la Tanzania Buisness Development Scheme, chini ya mpango wa Matching Grants Scheme. Shirika hili lilitoa jumla ya shilingi milioni nne, laki nane, mia tano na hamsini. Mbali na miradi hiyo jumuiya ya POFADEO inafanya miradi mbali mbali ya kuwafundisha wafugaji kwa kutumia nguvu na michango ya wanajumuiya na wataalmu waliomo ndani ya jumuiya hiyo. |
(Bila tafsiri) |
Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe