Base (Swahili) | Kiswahili | ||
---|---|---|---|
Mbunge mteule kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar,Mussa Khamis Silima, alipata ajali juzi katika eneo la Nzuguni, Dodoma, ambapo mkewe, Mwanaheri fahari, alifariki dunia na yeye na dereva wake kujeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospital ya Muhimbili kwa matibabu zaidi Mwili wa mke wa Mbunge Mussa Khamis Silima, Hayati Mwanaheri, ukiombewa dua na Wabunge n waombolezaji wengine baada ya kuwasili katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa mjini Dodoma leo kuswaliwa kabla ya kupelekwa Zanzibar kwa mazishi. Marehemu alifariki Jumapili jioni kwa ajali ya gari katika eneo la Nzuguni, nje kidogo ya mji wa Dodoma Mwili wa Marehemu ukiingizwa msikitini kuswaliwa kabla ya safari Gari la mafuta lililohusika katika ajali hiyo ambapo mfanyakazi wake anaonesha mahali ambapo gari dogo lililokuwa na marehemu na mumewe kugonga wakati likitaka kupita Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo akimweleza mbunge wa Mafia, Mh Shah, kilichotokea Mbunge wa Mafia Mh. Shah akiliangalia gari dogo la Mh. Silima lilivyoharibika baada ya ajali hiyo
|
(Not translated) |