Fungua
Chanika Tuamke Youth Organization (CTYO)

Chanika Tuamke Youth Organization (CTYO)

Ilala Dar Es Salaam, Tanzania

large.jpg

Uelimishaji wa vijana kwa njia ya sanaa shirikishi.

large.jpg

Harakati za kuelimisha jamii bado zina endelea ili kufikia malengo

large.jpg

Mafunzo ya Afya ya Uzazi kwa vijana yaliofanyika Iringa yalio Endeshwa na AMREF

large.jpg

Baadhi ya Semina za Afya ya Uzazi kwa vijana zilizo fanywa na Chanika Tuamke Youth Organization (CTYO)

large.jpg

Baadhi ya Matamasha ya Afya ya Uzazi kwa vijana yaliofanywa na Chanika Tuwmke Youth Organization (CTYO)

large.jpg

hizi ni baadhi ya shughuli za Chanika Tuamke Youth Organization (CTYO)

large.jpg

hizi ni baadhi ya shughuli za Chanika Tuamke Youth Organization (CTYO)

large.jpg

Katika kuhakikisha kuwa tuna kuwa na vijana bora wenye uwezo wa kupanga mipango kuisimamia na kuitekeleza ili kujiletea maendeleo chanya. Mikakati mbalimbali inafanyika kupitia Chanika Tuamke Youth Organization (CTYO) ili kuhakikisha vijana wanapata haki zao za msingi.

Pia Chanika Tuamke Youth Organization (CTYO) Imeanza mkakati wa kutaka kuanzisha Mfuko wa Maendeleo ya vijana CTYO Mfuko huu una malengo mbalimbali yakiwemo kuwa saidia vijana mbalimbaili nao kama:

1.Vijana waliofeli kidato cha nne na darasa la saba

2.Vijana na watoto waishio katika mazingira hatarishi

3.Vijana na watoto waathirika na Unyanyasaji wa jinsia

4.Watoto wenye watoto yani (Children mother)

5.Vijana na watoto waathirika na virusi vya UKIMWI na vijana kwa ujumla. Mfuko utalenga kuwapatia vijana mafunzo yafutayo:

1.Welding

2.Aluminum

3.Computer application

4.Cherehani

 5.Ujasiliamali BAADHI YA MAJUKUMU YA MFUKO yatakuwa ni

1.Kutafuta wadau wa kufadhili shughuli za CTYO

2.Kuunda miradi midogomidogo na kutoa ajira kwa vijana

3.Kuendelea kutoa Elimu ya Afya ya Uzazi kwa vijana

4.Kuendeleza shughuli za ushawishi na Utetezi kuhakikisha kuwa kuna kuwa na vijana bora wanaoweza kupanga mipango kusimamia na kuitekeleza ili kujiletea maendeleo chanya.

5.Kuendeleza shughuli za Ushawishi na Utetezi kuhakikisha vijana wanapata Afya,Maadili,Malezi na huduma bora ya rafiki kwa vijana katika jamii na serikali kwa ujumla na kuchambua sera mbalimbali za vijana na kuhakikisha sera hizo zinakwenda na wakati na zinafanyiwa kazi.

MWISHO

Chanika Tuamke Youth Organization (CTYO) Inakushukuru wewe kwa kutufuatilia kwa karibu Pia CTYO ina vijana Makini,Malidadi,Wanaojiamini,Wanaoweza kupanga mipango kusimamia na kuitekeleza ili kuleta maendeleo katika jamii. Shukrani sana.