Vijana Wanachuo cha Victory wakiwa kwenye sherehe za ufunguzi wa wiki ya elimu zilizo fanyika makao makuu ya shirika la VIYOSO-MOROGORO
Wanachuo wa victory wakigonga grasi zao kuashiria ufunguzi wa wiki ya elimu
wanachuo wa victory wakicheza kwaito katika ufunguzi wa wiki ya elimu morogoro
vijana kutoka chuo cha victory Morogoro kilichopo chini ya Asasi ya Vijana ya VIYOSO wakicheza
Baadhi ya wanamichezo vijana kutoka chuo cha Victory kilichopo chini ya taasisi ya VIYOSO wakiamasisha michezo kwa jamii
SHIRIKA LA VIYOSO LATOA SEMINA KWA VIJANA MKOANI MOROGORO
Shirika la VIYOSO kwa kushirikiana na shirika la YES IDO yameendesha semina ya ujasiliamali kwa vijana zaidi ya 63 kutoka kata 29 za manispaa ya Morogoro.
Semina hiyo ilikuwa na lengo la kuwajengea uwezo vijana juu ya kujitambua na jinsi ya kuwa mjasiliamali hili kuinua kipata na kuchangia maendeleo ya Taifa.
Mkurugenzi wa Asasi ya vijana VIYOSO mkoani Morogoro Bw. Freddy Ng'atigwa akifungua semina ya ujasiliamali kwa vijana wa manispaa ya morogoro semina iliyoandaliwa kwa ushirikiana wa asasi ya viyoso pamoja na YES IDO kutoka marekani.
mwezeshaji Bi Ashura kutoka ofisa za Manispaa Morogoro Kitengo cha Biashara akitoa mada juu ya fulsa za wajasiliamali vijana kupata leseni katika kuanzisha shughuli zao