Challenges facing millennium development goals.
Tanzania’s leadership is struggling to promote gender equality to meet the requirements of the Millennium Development Goals. Success of the MDG number 3 and target number 4 are all intended to be portrayed by four major indicators. The goal is to promote gender equality and empower women, while the target is to eliminate gender disparity in primary and secondary education by 2005 and in all levels of education not later than 2015.
The four indicators are: Ratio of girls to boys in primary, secondary and tertiary education to be equal as well as ratio of literate females to males among 15 – 24 years. Two other indicators are:- share of women in wage employment in the non agricultural sector, to be the same as that of men and proportion of seats held by women in the national parliament to be 50%.
Gender equality can simply be preached and lived; enrolment of children in pre and primary schools has always been done without discrimination among children of both sexes in our country. Nevertheless, the ratio has never been as required.
In 2007, the number of boys enrolled was 4,215,171 while that of girls was 4,101,754. Moreover pregnancy further lowered the number of girls by raising the number of girls’ school drop-out. The men responsible with the pregnancies have been going unpunished, even though the law states that 30 years’ imprisonment is what they deserve for so doing.
What happens is that, a parent who happens to sue a man for impregnating his/her daughter is required to go to court. Going to court takes time, and sometimes bus fare where the court is some distance away. The magistrate may postpone the case three our four times, leaving the parent tired and broke. Without bus fare, the parent will not be able to report again to the court.
Without complainant, the magistrate will not be able to go on with the case. So the accused walks away to ply his trade. Postponement of such cases may be intentional, although some magistrates may give excuses which cannot be denied as genuine.
In some communities, girls are given into marriage at a young age, sometimes as young as 12 or 13 years. Although the law says that any person under 13 years is a child and children are not given into marriage, the same law says that a girl of 14 can be given into marriage at the consent of the parents.
Even if this law is amended, to prohibit such girls of tender age to be given into marriage, yet some culprits will break that law and the principle will again protect such law-breakers; cases will be postponed till complainants lose hope and decide to work in their fields instead of wasting time by going to court where justice is not expected to be dispensed. Again none will be convicted.
The number three indicator which is equal share of women in wage employment in the non agricultural sector cannot be implemented without adequate education being considered. It will not be proper to pick a woman from the streets and employ her in an office, just to balance the number of women against that of men in offices.
The same applies to indicator number four. The proportion of seats held by women in the national parliament will depend on the academic qualifications of the women. When women candidates cannot compete with men academically, voters may vote for them at their peril. Even the president may nominate some of the kind, but such members of parliament will be a burden to the house.
These are only challenges rooted from education. There are more when we consider other aspects. For example, when empowering of women is being considered, land ownership should not be excluded. However, land is acquired through inheritance or acquisition, which is by paying money to buy it. Inheritance can be given by parents to their children. Parents themselves give away their possessions to children according to certain criteria. In some societies, a girl who marries becomes part of the husband’s family. Some parents do not consider such daughters in their wills.
In case they die, what they will inherit will be the deceased mothers’ clothes and maybe jewelry (unfortunately very few women in our culture have jewelry) but not land. Some fathers bequest their possessions to children after weighing what such children are worth. A daughter who had had no income, who had not brought even a half kilogramme of sugar to her father is not likely to get something valuable from such a father, who is the sole owner of land in the family.
As in the case of acquisition, one has to pay money to buy land. A woman who had had no learning, no employment will not be able to buy land. Moreover, money lenders need security for their money. Without security, an ordinary woman is not likely to get a loan from our banks. Some money-lenders who have more lax rules are those who take loans from our banks and lend it in small amounts to their customers, especially “mama-lishes”, who cannot make any development because the rates of interest are high. The lenders have to charge much to pay back their creditors and leave some to pay for their own survival.
In order to meet the MDGs requirements, education obstacles to girls must be dealt with accordingly. The law intended to safeguard children (Education law 25/1978) must be in operation. The Swahili language newspaper, Uhuru of November 20, 2006 reported that 47 girls failed to complete standard seven in Kilombero district because they got pregnant and some of the men responsible with the malady had been dealt with, but others were living with the girls as their wives.
This was an Area Commissioner’s report to his senior, the Regional commissioner. One wonders why these others were given a green light, to live with the pregnant pupils, while the law states plainly that they should be punished.
Sometimes the chains that prevent us from being free are more mental than physical...
ELIMU DUNI YA FEDHA INAWAATHIRI WANAKOPAJI BENKI…
October 10 hadi 13 mwaka huu, ilikuwa ni wiki ya huduma za kifedhana uwekezaji, iliyofanyika jijini Dar es salaam.
Katika maonyesho hayo hakuwepo kwa taarifa maalumu ya kuonyesha idadi ya washiriki, lakini ilionekana kuwa na washiriki wengi katika wiki hiyo.
Inawezekana idadi kubwa ya washiriki ilikuwepo kutokana na kutokuwepo kiingilio,pia na kutolewa bure kwa elimu iyo ya ujasiria mali kwenye mabanda zaidi ya matatu kwnye viwanja hivyo.
“nimejua mengi kuhusu namna gani naweza kupata mikopo na jinsi ya kusimamia biashara yangu katika hali ambayo itanipa ufanisi wa kudumu”.
“mimi n mjane,nina watoto wa tatu ambao nawatunza na nimekuwa nahangaika kupata mkopo, nafuga kuku, ambao nafikiri sasa nahitaji mkopo ili nikuze mtaji wangu” anasema Muro.
Anasema ipo haja ya wiki ya huduma za fedha zikaendeshwa katika maeneo mengine nchini ili kuwasaidia watanzania wengi zaidi ambao tafiti zinaonyesha kwamba hawana ujuzi wa kusimamia fedha zao kwa ufasaha.
ELIMU DUNI NI CHANZO CHA WAKOPAJI KUTOREJESHA MIKOPO.
Muro anasema kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu elimu ya fedha, kumesababisha watu wengi kushindwa kulipa madeni wanaokpa benki.
“nilichogundua kwenye wiki hii ya fedha ni kwamba taasisi nyingi za mikopo nchini zimekuwa hazitoi elimu nzuri ya mikopo , na taasisi hizo zinafanya hivyo kwa lengo la kuwadhulumu hasa katika marejesho na kupitia riba za mkopo, lakini hakupewa elimu jinsi atakavyoendesha biashara yakeau kusimamia fedha yake sawasawa..”
MAMBO MUHIMU KABLA YA KUKOPA MKOPO..
Taarifa ya taasisi ya Bogach Finance Co.Ltd inaeleza kwamba ni lazima mkopaji awe na sababu ya uhakika ya kuchukua mkopo huo, kabla ya kuamua kufanya hivyo.
Bogach Finance Co. Ltd imekwa ikitoa mikopo kwa ajili ya watakaotaka kujiendeleza kielimu, kulipia pango la nyumba,kununua viwanja na huduma za mikopo kwa vikundi.
Kampuni hiyo imebainisha kwamba siri moja ya kuw a na mafanikio mazuri yatokanayo na mkopo ni kutimiza malengo ambayo muombaji anakuwa amejiwekea kabla ya kuamua kukopa.
Baadhi ya wakopaji wamebaini kwamba zipo taasisi ambazo zinatoa mikopo bila kubainisha aina ya riba wanatozwa katika mikopo wanayotaka.
Mfanyabiashara wa soko l kariakoo Jonathan Kihaule , ambaye alikwenda kwenye wiki ya huduma ya fedha , alisema kuna benki zimekuwa zikifurahia wakopaji kutokuwa na elimu ya mikopo.
“nilichogundua baada ya mafunzo, kutokuwa na elimu ya kifedha kunasababisha matatizomengi katika maisha. Kwa mfano mtu anaeza kukimbilia riba ya asilimia mbili kwa mwezi, ambayo ukichanganua ni sawa na asilimia 24 kwa mwaka na kuacha riba ya asilimia 10 kwa mwakaambayo ni nafuu”
Anasema kihaule.
Mfanyabiashara huyo amewashauri watanzania kujua muda wa marejesho ya mkopo, masharti ya riba kabla ya kukimbilia kukopa kwa kuwa kadri muda wa kurejesha mkopo unapokuwa mrefu riba pia inakuwa kubwa.
Kwa mfano, mkopo wa sh5 milion unatozwa riba ya 24% kwa mwaka ukitaka ukatwe ndani ya miaka mitatu riba itakuwa 964,000 lakini watu wengi hawana ufahamu kuhusu hilo.
NI KOSA LA TAASISI ZA FEDHA KUTOA SIRI.
Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wakopaji kwamba baadhi ya taasisi zimekuwa zikiwatangaza watu wanaokopa mikopo katika taasisi hizo jambo ambalo kampuni ya huduma ya fedha ya Finscope Survey imeonya tabia hiyo.
Finscope Survey inakiri kwamba watoa mikopo wamekuwa wakitangaza taarifa za wateja wao kwa watu wengine na kukiukasheria za mikopo ya Benki Kuu ya Tanzania( BOT Act2007).
Taarifa za mkopaji zinatakiwa kuwa siri kati ya ofisi ya mkopo na mteja wake kwani kutoa siri ya mtu mwingine ni kinyume cha sheria.
TAFAKARI DHAMANA YA KUWEKA KABLA YA KUKOPA.
Mchambuzi wa maswala ya uchumi kutoka Zanzibar, Hawa Maljuni, anasema mkopaji yoyote anatakiwa kuwaza kwa makini kuhusu dhamana ya kuweka hasa kwa mikopo inayotaka mkopaji kuweka nyumba, gari au biashara kama dhamana kabla ya kupewa mkopo.
“kuna watu wengine wamepoteza gari, nyumba baada ya kuweka dhamana ili wapate mkopo. Ukweli ni kwamba unatakiwa kuweka gari au nyumba yako iwapo tu una uhakika kwamba una uwezo mkubwa wa kurudisha deni kwa wakati” anasema Hawa.
Kama una wasiwasi kuhusu kurejesha mkopo usikubali kuweka dhamana ya gari au nyumba. Pia imebainika asilimia 21 tu ya wakazi wajiji la dare s salaam na vitongoji vyake wana elimu ya usimamizi wa fedha huku asilimia 48 wana ufahamu wa kuweka akiba, hii ni kwa mujibu wa utafiti uliyofanywa na taasisi ya kifedha ya Finscope .
Kwa mujibu wa ofisa mmoja wa taasisi hiyo, Ally Goronya, karibu asilimia 80 ya wananchi wote jijini dar es salaam hawana ufahamu kuhusu maswala ya mkopo.
Utafiti unabahinisha, asilimia 54 ya wanawake wote jijini dare s salaam wanaochukua mkopo wengi wao wameishia kunyang’anywa dhamana wanazoweka ili kufidia fedha wanazokopa.
Kwa mfano, vyombo vya ndani, kama friji na mali nyinginezimekuwa zikichukuliwana taasisi za fedha kutokana na wakoaji kuwa na elimu duni ya kutunza fedha na kurudisha kwa wakati.
Utafiti huo ulifanyika mwaka 2009 na kubaini kuwa kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu fedha kumesababisha watanzania wengi kushindwa kufikia malengo ambayo wameweka kabla ya kuchukua mkopo.
Wateja wengi wanachukua mikopo wamekuwa wakidhulumiwa haki zao kwa sababu hawana elimu ya kutosha kuhusu fedha.
Mratibu wa wiki ya huduma za fedha, Godfrey Kivamba,anasema zaidi ya wajasiria mali 1600 walihudhuria na kupatiwa mafunzo, na jitihada zinafanyika kuhakikisha watu wengi wanapatiwa elimu.
Anasema lengo la mpango huo ni kutoa elimu kuhusumatumizi bora ya taasisi za fedha hasa suala la mkopo kwa kuwa wananchi wengi nchini hawana elimu ya kutosha, ukilinganisha na nchi kama Kenya, Uganda, Rwanda, na nyingine nyingi za Afrika.
Mafunzo yaliyotolewa na pamoja na kutambua jinsi ya kufungua kampuni, mikopo na biashara.
Ofisa mikopo wa wajasiriamali wadogo katika benki ya CRDB, Frank Peter, anasema wajasiriamali wanakabiliwa na matatizo ya mitaji na kukosa elimu sahihi kuhusu jinsi ya kukopa katika taasisi za fedha.
Chanzo: Mwananchi, oct 18 2012