Injira
Africa Upendo Group

Africa Upendo Group

Shighatini,Mwanga,Kilimanjaro, Tanzania

Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

Vijana wa Africa Upendo Group wamekuwa wakikutana mara kwa mara kujadiliana maswala mbalimbali yanayohusu vijana.

kutokana na wimbi la vijana wengi ambao wanamaliza vyuo vikuu lakini kutokana na mashirika na serikali kung'ang'ania kuwa vijana hawa wawe na uzoefu katika kazi na kwa kuzingatia kuwa vijana hawa ndio kwanza wanatoka kwenye vyuo wamekuwa katika kuhangaika sana.

Katika asasi yetu ya Africa Upendo Group tumekuwa na kitengo maalum cha kuwasaidia vijana kama hawa kwa kuwapatia mafunzo mbalimbali na kwa pamoja kwa njia ya kujitolea tumeweza kuwa na mikutano ya mara kwa mara.Ili kubaini njia mbadala katika kuona kuwa vijana wanapokuwa bado wapo mashuleni na baada ya kutoka wanaweza kujiajiri wenyewe kwa kufanya mambo mbalimbali yakiwemo tafiti mbalimbali.Katika kuliona hili vijana hawa wametengeneza tovuti ambayo itajulikana kama www.ICT4TD.co.tz ambayo itakuwa na shughuli mbalimbali zikiwemo vijana wengi kujitolea kufundisha masomo mbalimbali kama lugha ya kijerumani,kifaransa,Kiingereza,masomo ya Teknohama watakuwa wanajitolea zaidi katika maswala yanayohusu jamii kama usafi na utunzaji wa mazingira,Makazi au kaya,vijana walioathiriwa au wako katika hatari ya kuambukizwa UKIMWI na madawa ya kulevya n.k kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali ikiwemo Envaya,DTBI,Restless,Global Exchange,VSO wizara ya habari utamaduni na maendeleo ya vijana .

Katika kutekeleza majukumu yao mbalimbali vijana wamekuwa na makongamano mbalimbali kama siku ya kujitolea duniani ambapo vijana waliweza kubadilishana uzoefu na mambo mbalimbali pia waliweza kuhudhuria mkutano ambao ulihudumiwa wa DTBI,na kwa pamoja walikutana na vijana kutoka chuo kikuu cha MIT kutoka Marekani na kubadilishana mawazo na wamekuwa wakifanya mambo mbalimbali ya mifano ya hayo.

Pia wameunda Stearing commitee ambayo itakuwa na majukumu mbalimbali kwa makundi mbalimbali.Ili kuboresha zaidi na kuhakikisha kuwa vijana wanapata taarifa za msingi kutoka nje na ndani ya nchi yao.Website hii imemalizika na iko katika hatua ya kuzinduliwa karibuni.

Hapa chini utaona moja ya kamati ambayo inashughulika na kuratibu makundi mbalimbali chini ya mwenyekiti wake Albert.Huyu ni kijana aliyemaliza mafunzo ya Teknohama kwenye chuo kikuu cha Dodoma na Moderator akiwa ni Neatness Msemo ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji katika Asasi hii.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

kwa kukuona picha nyingi zaidi bonyeza link hapo chini:

http://ict4td.webs.com/apps/photos/album?albumid=12923434

13 Gashyantare, 2012
« Inyuma Ahakurikira »

Ibitekerezo (5)

Africa Upendo Group (Makuburi - Kinondoni Dar es salaam) bavuzeko

Asasi yetu ina mambo mengi inayofanya kuona kuwa wale ambao wapo katika asasi hii wanapata shughuli mbalimbali za kufanya.Kama ambavyo tulishaeleza kuwa tuna projects mbalimbali tunazoendesha na nyingi ya projects hizo ni pamoja na Training na mafunzo kivitendo.Tuliamua kutafuta eneo kule Matipwili kwa ajili ya ufugaji wa samaki wa maji baridi kwa kutumia mto Wami lakini pia tuna eneo la ufugaji wa samaki wa Bahari.Huko Kilwa na hapa ni baadhi ya picha ambazo tulizipiga tukiwa na Mkutano na wanavijiji wa huko.

13 Gashyantare, 2012 (edited 13 Gashyantare, 2012)
Africa Upendo Group (Makuburi - Kinondoni Dar es salaam) bavuzeko

Pamoja na mikutano na wanakijiji wa Singino kule Kilwa lakini tulipata bahati ya kutembelea wajasiriamali ambao wanapata kipato chao kwa njia ya uvuvi wa Maliasili za bahari.Wako duni sana hawana vifaa vya kuvulia na ili kuwatoa huko ni kwa kuwafundisha njia hii ya ufugaji wa samaki wa maji chumvi kwa njia ya kitaalamu zaidi ndio maana tumechukua eneo kwa kushirikiana nao basi tuache mazalia ya bahari yasiharibiwe ovyo kwa vifaa duni na badala yake tutumia njia mbadala ya kufuga kwa maji chumvi lakini kwenye mabwawa.angalia wavuvi hawa

Hawa ni samaki wa baharini wanaopatikana huko Kilwa.Tulipata bahati ya kuwala kwa wingi na ni watamu ajabu.

Wavuvi wana vifaa duni vya kuvulia Samaki.Tunawasaidiaje jamani

Vijana wamechoka na wanarudi bila Samaki kwani wangekuwa na Mashua na vifaa vizuri wasingeonekana katika hali hii

Hiki ni kijiji cha Singino Kilwa tulipofanyia mikutano yetu na wana kijiji.

Hapa tunasubiri kuuziwa Samaki wa baharini mwangalie mzee huyu anasema yupo hapa miaka mingi na anafanya kazi hii wakati wote

Hapa ni kwenye mnada wa Samaki wajasiriamali wanakuja kununua samaki

Mama huyu mjasiriamali akikaanga samaki zetu tulizonunua

Kaka yuko Busy akiwaparura samaki tulionunua kweli ni Utalii wa nguvu

Hapa ni Darasani kwenye ofisi za asasi watu mbalimbali wamekusanyika kumsikiliza mkufunzi kutoka Chuo cha Uvuvi Mbegani Bwana Kissai akiwafundisha njia bora na za kisasa za ufugaji wa samaki kwa kutumia mabwawa.

Hapa wanasemina wakishauriana jambo ambalo lilionekana kutokueleweka na mkufunzi msadizi anawaelimisha.

13 Gashyantare, 2012 (edited 13 Gashyantare, 2012)
steven s. yohana (kilwa kivinje) bavuzeko
kwa jina naitwa Steven S. yohana,ni Afisa uvuvi kilwa kivinje,nimefulahi sana kuona kwamba mnaendelea kutoa elimu inayohusu ufugaji wa samaki. Ni kweli kwamba samaki wamekua wakitegemewa na jamii nyingi Duniani kwa ajili ya chakula na kipato.Kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya samaki pamoja na mazao yake na kukua kwa teknolojia ya uvuvi.shughuli za uvuvi katika maji ya asili zimeongezeka kwa kiwango kikubwa ,hali hii imesababisha kupungua kwa kiwango kikubwa cha rasilimali za uvuvi hususani kwenye Bahari.Kwahiyo mbinu kubwa ya kutatua tatizo hilo ni ufugaji wa samaki,ili kuweza kupunguza fishing effort baharini.kingine ambacho cha muhimu sana ni ubora wa kitoweo cha samaki kwamba hakina madhala yoyote ukilinganisha na nyama za mbuzi,kuku,ngombe ambazo hukua kwa madawa mengi.wito wangu karibuni sana kilwa,na msituchoke kututembelea,lakini kingine ni kwamba kuna kikundi cha wavuvi ambao wapo tayari katika maswala ya ufugaji,kikundi kipo kijiji cha mgongeni kilwa kivinje,karibuni sana.
6 Nzeli, 2012
robert ottaru (makuburi dar es salaam) bavuzeko

Ni vipi watu kama sisi ambao tunataka kupata elimu kuhusu ufugaji wa samaki 2tajuaje wakati nyie mmefundishwa 2naona picha pia mmefundishwa na bwana kissai kwani hamuwezi kuandika hicho
mlichojifunza na mimi nijifunze
14 Gicurasi, 2013
Neatness (via email) bavuzeko
14 Gicurasi, 2013

Tanga igitekerezo

Izina ryawe:
Aho uherereye
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.