Asasi kwa kushirikiana na wanaasasi wae imeandaa mafunzo ya sheria ya malezi ya mtoto
kwa wanajamii wa kata ya Mpeta. Mafunzo hayo yamelengwa kuwasaidia wanajamii kuweza kufahamu umuhimu wa malezi kwaa mtoto na sheria zinazohusu masuala hayo. Mafunzo hayo
yatafanyika kati tarehe 10-14 za mwezi wa Septemba mwaka huu wa 2105 kwenye zahanati ya Mpeta. Wawezeshaji watakuwa ni Yakobo Mchopa, Mwanaafa Malenga, Anjelina Saidia na Thecla Mbawala.
Ni matumaini yetu kuwa wananchi wa kata hiyo na vijiji jirani wataweza kuhudhuria na kupata elimu hiyo itakayotolewa bure.
Washema imeendelea na shughuli zake za kutoa huduma za usaidizi wa kisheria na haki za binadamu. Wanachama wake wamesaidia jamii kwa kutoa elimu juu yamasuala ya kisheria katika kata za Nanganga, Chiungutwa, Mchauru, Namalenga, Mkomaindo na Lukuledi. Aidha kwa sasa inafanya utafiti wa kubaini makundi ya wanawake, vijana na walemavu ambao wanakosa fursa ya kugombea katika chaguzi mbalimbali. Utafiti na uibuaji huo umelenga kata za Chiungutwa, Nanganga na maeneo ya Mji wa Masasi. Baada ya utafiti huo kutaandaliwa mpango mkakati wa kuwezesha walengwa hao kujengewa uwezo ili waweze kushiriki na kugombea nafasi za uongozi wa serikali za mitaa Dec 2014 na udiwani na ubunge kwenye uchaguzi mkuu wa 2015 na kuongeza idadi ya wale wachache waliopo. Katika mradi huo Washema itahusisha asasi zingine zinazoshiriki katika masuala ya kujengea uwezo na utoaji wa elimu ya uraia.