Injira
The Foundation for Human Health Society.

The Foundation for Human Health Society.

KAHAMA, Tanzania

Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

TANZANIA KUWA KINARA WA UTOAJI WA HUDUMA ZA KIMAABARA AFRIKA MASHARIKI NA KATI



▪️Waziri Mavunde aweka jiwe la Msingi wa Ujenzi wa Maabara ya kisasa


▪️Ni maabara kubwa ya uchunguzi wa sampuli za madini Afrika Mashariki


▪️Kugharimu Tsh Bilioni 14.3


▪️Rais Samia atajwa kinara wa mageuzi sekta ya madini



📍 Kizota, Dodoma


Tanzania imeanza ujenzi wa maabara kubwa na ya kisasa ya uchunguzi wa sampuli za madini ambayo itakuwa ni kubwa kuliko zote kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati na ambayo itatoa huduma ya kimaabara kwa ubora na kwa uharaka kwa wadau wa sekta ya madini nchini.


Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa maabara ya kisasa ya uchunguzi wa sampuli za madini katika eneo la Kizota,Jijini Dodoma.


“Tunamshukuru Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa kuwa kinara wa mageuzi makubwa ya sekta ya madini na kwa kuandika historia ya ujenzi wa maabara hii ya kisasa miaka 100 baadaye tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa madini(GST) mwaka 1925.


Leo tunaandika historia kuanza kwa ujenzi wa maabara kubwa ambayo itafungwa mitambo na vifaa vya kisasa katika kutoa huduma za kimaabara ndani na nje ya nchi.


Huu ni ukombozi mkubwa kwa wadau wa sekta ya madini katika kupata taarifa sahihi za kimaabara kwa wakati na zenye ubora wa hali ya juu.


Ni imani yangu maabara hii itachochea ukuaji na maendeleo ya sekta ya madini”Alisema Mavunde


Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini(*GST*) Dkt. Notka Huruma Batenze amesema Maabara hiyo ya kisasa ya uchunguzi wa sampuli za madini utaleta tija kwa wadau wa sekta ya madini na kurahisisha upatikanaji wa huduma hii muhimu kwa maendeleo ya sekta ya madini.


Gharama za ujenzi wa maabara hii unatarajiwa kuwa Tsh Bilioni 14.3 na muda wa ujenzi wa kukamilika maabara ni siku 690.

CHEREHANI EMMANUEL ACHUKUA FOMU YA UTEUZI KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA USHETU KUPITIA CCM



1000746074.jpg
1000746075.jpg
1000746076.jpg
1000746077.jpg
1000746078.jpg

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ushetu, Wilaya ya Kahama, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Cherehani Emmanuel , leo Agosti 24, 2025, amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo.


Cherehani ambaye aliteuliwa na Kamati Kuu ya CCM Taifa kupeperusha bendera ya chama hicho amepokelewa na kukabidhiwa fomu hiyo na Afisa Uchaguzi katika Jimbo hilo Charles Mburu.


Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fomu, Cherehani amekishukuru Chama chake na wananchi kwa imani waliompa huku akisisitiza mshikamano ndani ya chama na kuondoa makundi ya makambi ili kujenga Ushetu yenye mshikamano na maendeleo kwa manufaa ya wananchi wote.

DC NKINDA AAGIZA WACHIMBAJI WADOGO WA DHAHABU MWIME WAREJESHEWE FEDHA ZAO

 .

1000745588.heic

DC Nkinda asisitiza makubaliano badala ya kutumia nguvu kwa makato ya wachimbaji
Aagiza wachimbaji wa Mwine warejeshewe zaidi ya milioni 7 walizokatwa kwa ajili ya ulinzi.
Aonya kuwa vitendo hivyo vinapunguza imani kwa serikali.
Ahimiza mazungumzo ya hiari kujenga mahusiano bora kazini.


Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Frank Nkinda, ametoa agizo kwa kampuni zinazojihusisha na uchimbaji wa dhahabu wilayani humo kuhakikisha hazitumii nguvu katika kufanya makato ya fedha kwa wachimbaji wadogo. Badala yake, amesisitiza umuhimu wa maelewano na elimu baina ya pande zote ili kuondoa malalamiko.

Akizungumza katika eneo la Mwine wakati wa kikao cha kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wadogo, Mhe. Nkinda ameagiza zaidi ya shilingi milioni saba (7,000,000) zilizokatwa kutoka kwenye malipo ya wachimbaji kwa ajili ya kulipia huduma za ulinzi wa mgodi, zirejeshwe kwa wachimbaji hao mara moja.

Ameeleza kuwa vitendo kama hivyo vinavunja imani ya wananchi kwa serikali, na kusisitiza umuhimu wa kuweka misingi ya maelewano nje ya mifumo rasmi ya kiserikali, ili kuimarisha uhusiano kazini na kuzuia migogoro kati ya waajiri na waajiriwa.

Mkuu huyo wa wilaya ameonyesha nia ya dhati ya kulinda maslahi ya wachimbaji wadogo na kuendeleza sekta ya madini kwa haki na usawa.



1000745587.heic
1000745585.heic
1000745584.heic
1000745586.heic

BENJAMIN LUKUBHA NGAYIWA AKABIDHIWA FOMU YA UTEUZI KUGOMBEA UBUNGE KAHAMA MJINI KUPITIA CCM

 1000746618.webp


Bw. Benjamin Lukubha Ngayiwa (Kushoto) mapema leo amekabidhiwa rasmi Fomu ya Uteuzi kugombea kiti cha Ubunge Jimbo la Kahama Mjini na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo hilo Bw. Sadick Kigaile kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

1000746620.webp
1000746619.webp
1000746619.webp


MKUTANO WA SABA WA KIMATAIFA SEKTA YA MADINI KUFANYIKA NOVEMBA, 2026

 1000745173.jpg

1000745121.jpg


*Yaelezwa Sababu ni kupisha maandalizi ya Maandalizi ya Uchaguzi Mkuu*


*Dodoma*


Wizara ya Madini imetangaza kusogeza mbele Mkutano wa Saba (7) wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini uliokuwa ufanyike mwezi Novemba 2025 na badala yake mkutano huo utafanyika tarehe 19 hadi 21 Novemba 2026, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar EsSalaam.


Taarifa iliyotelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Madini Eng. Yahya Samamba imeleza sababu za kusogezwa kwa mkutano huo kuwa ni kupisha maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa nchini uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba, 2025.


‘’Wizara ya Madini inaomba radhi kwa wadau wote wa ndani na nje ya nchi waliokuwa wanatarajia kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini ambao ulipangwa kufanyika Novemba 2025,’’ imeeleza taarifa hiyo.


Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini nchini unaofanyika kila mwaka tangu 2019 ukibebwa na kaulimbiu mbalimbali, hutumika kama jukwaa la kujadili kwa pamoja mstakabali wa Sekta ya Madini, kubadilishana ujuzi, maarifa na uzoefu pamoja na kuangazia fursa mpya zinazojitokeza katika Sekta ya Madini nchini.


Vilevile, mkutano huo hutumika kuimarisha mazingiraya uwekezaji, kuendelea kuvutia uwekezaji mpya kutoka ndani na nje ya nchi, wadau kupata fursa ya kujifunza Sera, Sheria na mikakati mipya ya Serikali na kujadili kwa pamoja masuala ya kisheria na uchumi yanayohusiana na Sekta ya Madini.


Mbali na hayo, kupitia hafla ya Usiku wa Madini ambayo huambatana na mkutano huo, hutumika kutoa tuzo kwa wadau waliofanya vizuri katika Sekta ya Madini kupitia vipengele mbalimbali ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wao kwa Sekta ya Madini nchini.


Aidha, mkutano huo huyakutanisha makundi mbalimbali wakiwemo mawaziri wa madini kutoka nchi nyingine za Afrika, watendaji wakuu wa kampuni kubwa za madini duniani waliowekeza nchini, watafiti, mabalozi wanao ziwakilisha nchi zao hapa chini na nje ya tanzania, mashirika ya kimataifa.


Makundi mengine ambayo hushiriki mkutano huo ni pamoja na wachimbaji, wafanyabiashara wa madini, taasisi za fedha, vyuo vikuu na vya kati, taasisi za umma, taasisi binafsi zinazojishughulisha na madini, viongozi mbalimbali kutoka wizara, taasisi za umma, mikoa na halmashauri ambazo shughuli za madini zinafanyika.



#Vision 2030:


*Madini ni Maisha na Utajiri*

HAYA HAPA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE CCM UCHAGUZI MKUU 2025 MKOA SHINYANGA

 




Mkoa wa Shinyanga :


Patribas Katambi- Shinyanga Mjini


Benjamin Lukubha Ngayiwa -Kahama Mjini


Mabula J. Magangila - Msalala


Ahmed Salum - Solwa


Azza Hillal Hamad - Itwangi


Emmanuel Cherehani - Ushetu


Lucy Mayenga - Kishapu

SEKTA YA MADINI YAENDELEA KUNG’ARA SINGIDA, SERIKALI YATENGA BILIONI 115 KWA UTAFITI WA KINA

 



Na Neema Nkumbi – Iramba, Singida


Wachimbaji wadogo wa madini mkoani Singida wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa hatua madhubuti za Serikali ya Awamu ya Sita katika kuimarisha sekta ya madini, zikiwemo ugawaji wa leseni mpya na kuondoa vikwazo vilivyokwamisha maendeleo ya wachimbaji wadogo.

Pongezi hizo zimetolewa Agosti 23, 2025, katika Kongamano la Wachimbaji Wadogo wa Madini wa Kanda ya Kati lililofanyika Sekenke One, Shelui Wilaya ya Iramba, ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde.



Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde amesema Serikali imejipanga kuongeza kiwango cha utafiti wa kina wa madini kutoka asilimia 16 hadi kufikia asilimia 50 ifikapo mwaka 2030, kupitia mkakati wa Vision 2030: Madini ni Maisha na Utajiri.

Kwa ajili ya utekelezaji wa mkakati huo, Serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni 115, ikiwa ni pamoja na ununuzi wa helikopta maalum kwa ajili ya upigaji picha za anga na ujenzi wa maabara za kisasa zitakazosaidia wachimbaji wadogo kufanya uchambuzi wa madini kwa ufanisi.

"Hatutaki tena kuuza mawe ghafi. Tunalenga kutoka kusafirisha mawe kwenda kuuza bidhaa za madini zilizoongezewa thamani, Hii ni kwa faida ya wachimbaji wadogo, vijana, wanawake na taifa kwa ujumla,” amesema Mavunde.

Waziri Mavunde ameongeza kuwa kampuni kubwa za madini zimeonesha nia ya kuwekeza katika mgodi mkubwa wa dhahabu utakaokuwa katika mikoa ya Singida na Dodoma, hatua ambayo inatarajiwa kuongeza ajira, mapato ya Serikali na kuchochea ukuaji wa uchumi wa kitaifa kupitia sekta ya madini.


Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego amesema kuwa sekta ya madini ndiyo inayoongoza kwa kasi ya ukuaji wa uchumi mkoani humo, ambapo kwa mwaka wa fedha 2024/25, Singida imekusanya zaidi ya shilingi bilioni 26, ikizidi lengo la awali la bilioni 24.


“Zaidi ya tani 2.7 za dhahabu huzalishwa kila mwaka, ambapo tani 1.5 zinatoka kwa wachimbaji wadogo. Huu ni ushahidi kuwa sekta hii imekuwa mkombozi wa wananchi wetu,” amesema Dendego.


Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida, Mhandisi Sabai Nyansiri, amesema mafanikio hayo yamechangiwa na mazingira rafiki yaliyowekwa kwa wachimbaji wadogo pamoja na usimamizi madhubuti wa shughuli za uchimbaji.

Nyansiri amebainisha kuwa uzalishaji wa madini mkoani Singida umeongezeka mwaka hadi mwaka na kwa sasa sekta hiyo inachangia zaidi ya shilingi bilioni 6 kwa mapato ya Serikali kwa mwaka.

Kwa mujibu wa wachimbaji hao, hatua ya Serikali kufuta leseni 2,648 ambazo zilikuwa hazitumiki na kuzigawa upya kwa wachimbaji wadogo kumesaidia kupunguza migogoro ya maeneo na uchimbaji holela, hivyo kufungua ukurasa mpya wa tija na uwajibikaji katika sekta hiyo muhimu.


Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA), Bw. John Bina, amesema zaidi ya wachimbaji wadogo milioni 6 wanashiriki kikamilifu katika shughuli za madini nchini na kuchangia takriban asilimia 40 ya mapato ya sekta hiyo.

“Tunatambua dhamira ya dhati ya Rais Samia katika kuwatambua na kuwawezesha wachimbaji wadogo, Hii ni heshima kubwa kwetu, na ndiyo maana leo tunasherehekea mafanikio haya,” amesema Bina.

Bw. Bina, ametoa rai kwa serikali kutumia fursa ya amani na utulivu nchini kujenga soko kubwa la madini ndani ya Tanzania.


“Tunaamini tunaweza kupata Dubai yetu hapa nyumbani Tukijenga soko hapa, wachimbaji watanufaika zaidi na kodi zitabaki nyumbani,” amesema Bina.

1000743325.jpg
1000743328.jpg
1000743336.jpg
1000743335.jpg
1000743323.jpg
1000743322.jpg
1000743321.jpg
1000743320.jpg
1000743319.jpg
1000743318.jpg
1000743317.jpg

WACHIMBAJI MKOA WA SINGIDA WAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA MAFANIKIO MAKUBWA SEKTA YA MADINI

1000743318.jpg



▪️Wapongeza ugawaji wa Leseni kwa wachimbaji wadogo Singida




▪️Singida wavuka malengo ya ukusanyaji wa maduhuli




▪️Waziri Mavunde aeleza mkakati wa kuongeza eneo la utafiti wa kina madini nchini




▪️Kampuni za madini zajipanga kuanzisha Mgodi Mkubwa wa Dhahabu kanda ya Kati (Dodoma & Singida)




📍 Iramba – Singida.




Wachimbaji Wadogo wa Madini Mkoa wa Singida wamepongeza jitihada kubwa za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika sekta ya madini, ikiwemo kugawiwa leseni na kuwekewa mazingira bora ya kufanya kazi zao kwa amani.




Pongezi hizo zimetolewa leo Agosti 23, 2025 wakati wa Kongamano la Wachimbaji Wadogo wa Madini wa Mkoa wa Singida na Kanda ya Kati, lililofanyika katika eneo la Sekenke One, Shelui – Wilaya ya Iramba, ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde.




Wachimbaji hao wameleza kuwa, hatua ya Serikali kufuta na kurudisha Serikalini leseni na maombi 2,648 ambayo hayakuwa yakifanyiwa kazi, kisha kugawiwa upya kwa wachimbaji wadogo, imekuwa suluhisho la muda mrefu kwa changamoto ya kuvamia maeneo na kuchimba bila leseni.




Akizungumza katika Kongamano hilo, Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amesema mpango wa Serikali ni kuongeza kiwango cha utafiti wa kina wa madini kutoka asilimia 16 kilichopo sasa hadi kufikia asilimia 50 ifikapo mwaka 2030, kupitia maono ya Vision 2030; Madini ni Maisha na Utajiri.




Amesema kuwa, Serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni 115 kwa ajili ya utafiti wa madini nchini, ikiwa ni pamoja na kununua helikopta maalum yenye vifaa vya kisasa kwa ajili ya upigaji picha na utafiti wa anga, sambamba na ujenzi wa maabara za kisasa za uchambuzi wa madini zitakazotumika na wachimbaji wadogo.




Wakati huohuo, Waziri Mavunde amebainisha kuwa Kampuni kubwa za madini zimeanza kujipanga kuwekeza katika Mgodi mkubwa wa dhahabu katika Kanda ya Kati (katika mikoa ya Dodoma na Singida), hatua inayotarajiwa kuongeza zaidi fursa za ajira, mapato ya Serikali na mchango wa sekta ya madini katika uchumi wa taifa.




Kwa upande wake, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA), Bw. John Bina, alisema zaidi ya wachimbaji wadogo milioni 6 wanashiriki kikamilifu katika shughuli za madini na wamefanikisha sekta hiyo kuchangia hadi asilimia 40 ya mapato yote ya madini nchini.




“Tunampongeza Rais Samia kwa maono yake ya kuendelea kuithamini sekta ya wachimbaji wadogo. Hii ni heshima kubwa kwetu na ndiyo maana leo tunasherehekea mafanikio haya,” alisema Bina.




Naye, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego, alisema sekta ya madini ndiyo inayoongoza kwa kasi ya ukuaji kiuchumi ndani ya mkoa huo na imewezesha Singida kuvuka malengo ya ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali.




“Madini ndiyo injini ya uchumi wa Singida, na kwa sasa mchango mkubwa unatoka kwa wachimbaji wadogo waliowekewa mazingira bora ya kufanikisha kazi zao,” amesema.




Awali, akizungumza katika kongamano hilo, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida, Mhandisi Sabai Nyansiri, amesema mkoa huo umefanikiwa kuvuka malengo ya ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali yatokanayo na sekta ya madini katika mwaka wa fedha 2024/25, baada ya kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 26 dhidi ya lengo la shilingi bilioni 24.


1000743325.jpg
1000743328.jpg
1000743336.jpg
1000743335.jpg
1000743323.jpg
1000743322.jpg
1000743321.jpg
1000743320.jpg
1000743319.jpg
1000743318.jpg
1000743317.jpg

WAZIRI LUKUVI ATOA MAAGIZO YA RAIS SAMIA AJALI YA MGODI NYANDOLWA


8bcd5e9d-6290-4eba-bdca-53321d7ed828.jpe

Waziri wa nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo kwa viongozi wa Serikali waliopo maeneo ya ajali ya mgodini kushiriki taratibu zote za mazishi kwa walifariki ajali ya mgodini na kuwakilisha rambirambi zake kwa wahusika huku akisihii kuendelea kuratibu vyema shughuli ya uokoaji inayoendelea.
dd8251f7-dbe1-4ee7-8cb8-6032f5768901.jpe

Ameyasema hayo wakati wa kikao na viongozi pamoja na ndugu wa waathirika wa ajali ya mgodini katika eneo la tukio la ajali ya mgodi unaomilikiwa na Kikundi cha Wachapakazi katika machimbo ya Nyandolwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
209b61f1-7e9f-4fff-b08a-53d135a32d95.jpe

“Rais Samia kaniagiza kuwafikishia salamu za pole na rambirambi pia kanituma kuleta maagizo kwa viongozi wa serikali waliopo eneo hili kuhakikisha wanahudhuria misiba yote ya watu waliopoteza maisha katika ajali hii na kuwakilisha rambirambi alizotoa katika familia hizo” amesema Lukuvi.
6454bab8-ec39-47c2-a920-3ed31f6929d7.jpe

Agosti 16, 2025 Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro alitoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Dk. Kalekwa Kasanga kufanya utaratibu wa kuweka ofisi ya muda ya mtendaji wa kijiji katika eneo la tukio la ajali ambayo itatumika kuwasajili wageni waliokuja kusubiri ndugu zao kwa ajili ya kuhudumiwa na serikali.
30605410-7ead-477f-9168-c8200a5e6213.jpe

Mnamo Agosti 18, 2025 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita alitoa maelekezo kwa familia zilizokuja kusubiri ndugu zao, kuchagua wawakilishi wawili au watatu ambao watabaki ili iwe rahisi kwa serikali kuhudumia familia hizo na kupewa mahitaji muhimu.
06fba4bf-2b77-488d-8245-7b321618804e.jpe

Aidha, Agosti 11, mwaka huu watu 25 walifukiwa na Mgodi wa Kikundi cha Wachapakazi katika Machimbo ya Nyandolwa na hadi sasa watu 11 wametolewa huku watatu wakiwa hai na nane wakiwa wamefariki, na juhudi za kuendelea kuwatoa wengine 14 zinaendelea kwa kasi kwa kutumia mashine za utambuzi wa ardhini kujua maeneo waliopo.