Envaya
Maeneo ya ukurasa huu ni kwa Kiingereza. Hariri tafsiri

large.jpg

Mwakilisha wa matokeo ya ufuatiliaji wa rasilimali za umma akiwasilisha taarifa kama ilivyokusanywa na watafiti kwenye kata mbalimbali zinazotekeleza mradi.

large.jpg

Darasa hili ni lililojengwa kwa fedha kutoka mguko wa maendeleo ya elimu nchini MMEM linapatikana katika kijiji cha Sunuka lakini cha ajabu ni kuwa liko katika hali hii. Darasa hili lina muda wa miaka miwili tu lakini linaonekana kama lenye miaka 6. Hii inatokana na ukweli kwamba wananch hawakushiriki katika utekelezaji wa ujenzi huu.

large.jpg

Washiriki wakijadiliana nje ya ukumbi wakijadiliana juu ya taarifa zilizowasilishwa kwenye mdahalo huu wakihusianisha na taarifa za wanasiasa ambazo huzitoa wakati wa kampeni na vikao mbalimbali vya kisiasa.

large.jpg

Hawa nao ni baadhi ya washiriki waliofurika kujisikilizia wenyewe juu ya hali halisi ya namna rasilimali zao hasa fedha zinavyotumika wakati wa midahalo hii katika halmashauri ya Kigoma

large.jpg

Mojawapo ya mikutano ya mdahalo iliyoendeshwa na shirika la KIOO katika Halmashauri ya wililaya ya Kigoma kujadiliana juu ya changamoto juu ya upangaji wa mipango ambao umeperekea matumizi mapaya ya rasilimali za umma hasa fedha. Mfano Katika kijiji cha Ilagala barabara iendayo sambala haikutengenezwa kabisa licha ya kuoneshwa kwenye taarifa kuwa imetengenezwa.

Mwezeshaji akiwezesha kwenye mojawapo ya semina za KIOO

Mzee huyu ni miongoni mwa wadau ambao wanawahamasisha wanajamii kushiriki kwenye mikutano mbalimbali ya kijiji na hapa alikutwa kwenye moja ya mikutano katika kijiji cha malagalasi wilaya Kigoma katika Tarafa ya Nguruka.

Uwakilishi wa wananchi upo nchini kisheria na wawakirishi hao hupatikana kwa njia ya kura halali ambazo hupigwa na wananchi kote nchini.Madiwani hawa wameonekana kuwa chachu ya mijadala katika halmashuari mara baada ya kushiriki mafunzo ya KIOO ya ufuatiliaji na uwajibikaji kijamii ambayo kwao waliyaona kama yamewafungua macho na kuanza kufuatilia kila kitu kwa ukaribu zaidi. Moyo huu waliouonesha tunawaomba wauendeleze kwa ajili ya maendeleo ya waliowachagua.

Hili ni boti lililotumika kubebea mbolea ya ruzuku ambayo iliuzwa na viongozi wa kijiji cha Nyahoza katika halmashauri ya wilaya ya Kigoma.Hii ilithibitika baada ya timu ya ufuatiliaji kuwahoji wananchi na kutokana na mwamko walioupata wakafichua kila kitu ndipo picha hizi zilipopatikana.

Baadhi ya washiriki wa semina ya wadau wa kupinga unyanyasaji kwa watu wenye ulemavu wa ngozi nchini.Mradi huu umetekelezwa na KIOO kwa ufadhiri toka Japan