Mojawapo ya Darasa lililogharimiwa na mfuko wa maendeleo ya elimu ya msingi kata ya mwandiga
Wajumbe wakisikiliza maelezo kutoka kwa mratibu wa mradi ndugu Edward ambaye hayupo pichani hapo. Huu ni wakati wa mafunzo yaliyoendeshwa na KIOO kwa ufadhiri wa The Foundation For Civil Society.
Wajumbe wa mkutano wa utambulisho wa mradi wakiwa wanamsikiliza mwezeshaji wa mafunzo hayo.
Katika kufanya ufuatiliaji wa mradi na tathimini ya ndani ya mradi ambao umefadhiriwa na The Foundation For Civili Sciety viongozi wa asasi yetu ya KIOO wakifuatilia matokeo ya mradi wa ufuatiliaji wa matumizi ya umma ikiwa ni pamoja namna wanajamii wanavyoshiriki katika kupanga mipango na namna wanavyofanya maamuzi juu ya hatima ya vijiji vyao. Katika kile ambacho hakikutazamiwa na wafuatiliaji hawa wa mradi ni kule kupatikana kwa maelezo juu ya namna ambavyo mabaraza ya kata na vijiji yanayohusika na utatuzi wa migogoro kijijini ambavyo wametumia mwanya huo kujinufaisha kimapato.
Wakitolea mfano wananchi waliohojiwa na wafuatiliaji wetu walipopata habari hiyo wakiwa katika kijiji cha Mwandiga waliambiwa kuwa mabaraza hayo yamekuwa yakitoza hadi elfu hamsini (50,000) kwa kila mdaawa yaani mlalamikaji na mlalamikiwa jambo ambalo linaonesha kwamba barza hilo la kata lilikuwa limepokea migogoro 40 ambayo ni sawa na shilingi 4,000,000/= zilizopatikana kutokana na migogoro hiyo lakini hakuna karatasi wala faili katika ofisi hiyo na mara zote wananungunika kukosekana kwa vitendea kazi.
Alipoulizwa juu ya hilo mtendaji wa kata hiyo Ndugu Mandari alikiri kuwapo kwa tukio hilo na kusema kwamba hii imetokana na ukweli kwamba watendaji wengi wakiwamo hao wanaotoza hela hizo hawana uelewa juu ya hilo.
Wakati huo huo pia wafuatiliaji wetu waligundua kuwa Halmashauri ya wilaya ya Kigoma ilikuwa imeanza kutekeleza wito wake kwa vitendo kwa kusambaza taarifa mbalimbali zikiwamo zile za mapato na matumizi kama zilivyokutwa kwenye mbao za matangazo katika kata mbalimbali zinazounda Halmashauri hii. Hatua hii kwa mradi wetu imekuja muda mwafaka na inatia matumaini na wito wetu katika hili ni kuendeleza juhudi hizi kila mwaka.
Wananchi wa kijiji cha Nyamhoza wamemshikiria mwenyekiti wao wa kijiji kwa tuhuma za kula fedha za pemebeo za kilimo ambapo alishirikiana na kamati ya vocha ya kijiji kula fedha hizo.Aidha mtendaji wa kijiji hicho ameshatoroka na hadi sasa hajulikani aliko. Juhudi hizi zimefanyika kupitia mradi wetu wa ufuatiliaji wa matmizi ya umma.
Habari nyingine tulizozipata wakati wa ufuatiliaji na tathimini ya mradi kutoka kijiji cha Kirando mwenyekiti wa kijiji hicho amepigiwa kura ya kutokuwa na imani naye hasa baada ya kubainika kwamba alitumia milioni 9 za kijiji kununua mashine yake ya kusoza jambo ambalo lilibainika wakati wa zoezi la ufuatiliaji wa matumizi ya umma katika kijiji hicho.
Wakati hayo yakiendelea katika vijiji hivyo huko Sunuka wananchi walichukua hatua za kumhoji mheshimiwa diwani juu ya taarifa za ujenzi wa hosteli katika shule yao ya kata kwa thamani ya shilingi 220,000,000/= ambapo hadi sasa msingi haujachimbwa kabisa licha ya kuwa mwaka wa fedha kwa ajili ya kazi hiyo unakwisha june mwaka huu. Aidha Diwani huyo alikiri kuwepo kwa bajeti hiyo katika mwaka huu wa fedha na kueleza kuwa muda si mrefu mkandarasi ataanza kufanya kazi hiyo. Lakini kama si kufanyika kwa mradi huu hakuna aliyekuwa na taarifa juu ya ujenzi huo.