Injira
LAKE ZONE ARTS GROUP (NZOGWI)

LAKE ZONE ARTS GROUP (NZOGWI)

Mwanza, Tanzania

Lengo kuu la shirika langu ni kusaidia na kuelimisha vijana ambao wameathirika  kwa ugonjwa wa ukimwi. Tunawasaidia kwa kutoa elimu kwa njia shirikishi, kwa sanaa za mikono na sanaa za maonyesho.  Pia tunatoa elimu ya kujikinga na maambukizi dhidi ya ukimwi.Lake zone art group  pia tunatoa  elimu ya upambaji yani ( art decoration) kwa vijana tunao wahudumia , kwa ajili ya kupambana na umasikini  ili vijana wasiokuwa ajira wapate kujiajiri wenyewe. Pia katika mradi wetu uliomalizika hivi karibuni Lake zone art group tuliweza kuwasaidia vijana wapatao kumi, wa kike watatu na wakiume saba kwa kuwapeleka katika vyuo mbalimbali kwa kuwapatia masomo.Tumewaghalamikia ada na mahitaji yote ya shule kama vifaa,mavazi n.k . Wakike tuliwapeleka katika Chuo cha mafunzo ya Ualimu Mara.  Pia wakiume tuliwapeleka veta na wote wamehitimu na wanaajira. Shughuli zetu tunazifanyia katika Kata ya Pamba Wilaya Nyamagana Mkoa Mwanza. Tunawakaribisha wote  mtutembelee katika Ofisi zetu zilizopo Bugando. Na tunakaribisha maoni ,ushauli n.k    .

 

Wenu Passion P. Kemikimba         

 

Amakuru agezweho
LAKE ZONE ARTS GROUP (NZOGWI) yasanze Envaya.
3 Werurwe, 2011
Ibyiciro
Aho uherereye
Mwanza, Tanzaniya
Reba ibigo mwegeranye