Mkuu wa Wilaya ya Kyela Bib Magreth Malenga akiwa katika sherehe ya wazee iliyofanyika katika Kata ya Busale kijiji cha Lema wilayani Kyela
Mkurugenzi wa Asasi ya SWOLO akiwa na wajumbe wa Baraza la wazee katika kijiji cha masoko wilayani Kyela hadi sasa mabaraza ya wazee katika vijiji 103 kwa ngazi ya vijiji na mabaraza 10 kwa ngazi ya kata yameundwa ikiwa ni pamoja na takwimu za wazee wote kwa majina zimeandaliwa. Shughuli yote hii imewezeshwa kwa msaada mkubwa wa The Foundation for Civil Society Tanzania
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la wazee kata ya Matema Wilayani Kyela wakiwa kwenye picha ya pamoja
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Asasi ya SWOLO wakiwa na viongozi wa Asasi hiyo.
Wazee wa Baraza la ushauri wakiwa katika Mkutano uliondaliwa na Asasi ya SWOLO ili kujadili haki zao
Mkurugenzi wa Asasi ya SWOLO akitoa maelezo kuhusu sera ya taifa ya wazee ya mwaka 2003 kwa wazee wa kijiji cha Kyijila wilayani Kyela.
Wazee katika kijiji cha Fubu wilayani Kyela wakiwa kwenye mkutano ulioendeshwa na Asasi ya SWOLO.