Base (Icyongereza) | English |
---|---|
Nashukuru kwa ujumbe wako mzuri ambao kwa kiwango kikubwa umenifunza mengi na kunionesha njia. Nikweli kabisa tatizo la vijana katika nchi yetu halitotatuliwa kwa propaganda za kisiasa ama maneno matupu bali linahitaji kujitoa mhanga na kuonesha moyo wa kipekee wa uzalendo wa kuwafunza/kuwaelimisha vijana na kuibadili mitazamo hasi ambayo ni mitazamo funge ya fikra na kupandikiza mitazamo chanya ambayo inazaa matunda ya heri na fanaka. Vijana wa tanzania wanahitaji msaada wa kifikra ambao utawaondoa pangoni na kuwaleta kwenye mwanga, tunahitaji kujitolea kwa hili na kuonesha ushirikiano na jamiii itatufuata baada ya kuona mafanikio. Sisi wana AUVITA tuko tiari kabisa kushiriki nanyi katika ukombozi huu wa vijana kwani ndiyo dhamira yetu kuanzisha asasi hii hivyo kwa hili tuko pamoja na wala hatutarudi nyuma. Pia umesema kuwa mumeshafanya mafunzo mbalimbali na matini munayo naomba utusaidie matini hayo ili tuyatumie pia kuwakomboa vijana wa mtwara ambao kweli dunia inaonesha kuwatupa mkono maana hofu waliyonayo vijana inahitaji jitihada kuwakomboa kifkra. Wako, Simba Mramba. 2014-06-11 15:36 GMT+03:00 Envaya : |
(Not translated) |
Kugirango ugire icyo uhindura kubyo wasemuye, ugomba kwinjira mu rubuga Injira · Iyandikishe