FCS Narrative Report
Utangulizi
Tarehe: Januari 25-Aprili 25, 2011 | Kipindi cha Robo mwaka: Robo ya kwanza 2011 |
TWSEDHRO
S.L.P 579
Kigoma Tanzania
Maelezo ya Mradi
Mkoa | Wilaya | Kata | Vijiji | Idadi ya Wanufaika |
---|---|---|---|---|
Kigoma | Kigoma (Vijijini) | Kagongo | 30 | |
Mukigo | 30 | |||
Nguruka | 30 | |||
Kasulu | Kasulu Mjini | 40 | ||
Kasangezi | 48 | |||
Nyakitonto | 47 |
Walengwa wa moja kwa moja | Walengwa wasio wa moja kwa moja | |
---|---|---|
Wanawake | 79 | 36,800 |
Wanaume | 146 | 31,200 |
Jumla | 225 | 98,000 |
Shughuli na Matokeo ya Mradi
- Mikutano ya utetezi na ushawishi ngazi ya Kata/Wilaya imefanyika na mikakati juu ya ufuatiliaji wake imeandaliwa.
-
2. Kutengeneza vipeperushi na mabngo ( Posters) yenye tafsiri rahisi ya sera ya maendeleo ya wanawake na jinsia na kuvisambaza kwa wingi katika maeneo ya vijijini ili wananchi waweze kuielewa sera na kufuatilia utekelezaji wake.
3. Kuunda vikosi vya ufuatiliaji wa masuala ya unyanyasaji wa wanawake vijijini ( Gender Violance Monitoring Group) na kuripoti na pia kutafuta mfumo bora wa kuripoti matukio hayo.
4. Kuendesha mikutano majukwaa ya utetezi na ushawishi ambapo wahanga wa matukio ya unyanyasaji wataalikwa kutoa changamoto walizopitia na mikakati ya pamoja kuandaliwa.
- Kuandaa vipeperushi 2,000 na mabango 1,000(Posters) na kuyasambaza katika kata zote sita yaani: Kagongo, Mukigo, Nguruka, Kasulu Mjini, Kasangezi/Kigembe, na Nyakitonto.
- Kuendesha mikutano sita katika kata sita ambapo mkutano uliendeshwa kwa muda wa siku mbili kama ilivyo pangwa kwa kila kata, jumla ya washiriki 30 walihudhulia kwa kila kata ambapo kwa ujumla jumla ya washiriki 180 walihudhulia mkutano huo.
Mkutano huo wa ufafanuzi wa sera na wajibu wa viongozi katika kutekeleza sera ya maendeleo ya wanawake na jinsia ya mwaka 2000, ulitekelezwa katika kata sita ambazo ni: kwa Kigoma Vijijini):- Kagongo, Mukigo, na Nguruka. Kwa Kasulu ni: Kata za kasulu Mjini, Kigembe/Kasangezi na Nyakitonto.
Masuala yaliyoshughulikiwa ni pamoja na haya yafuatayo;
- Ufafanuzi kuhusu Sera ya Maendeleo ya wanawake na jinsia ya mwaka 2000
- Wajibu wa Viongozi katika kutekeleza Sera ya maendeleo ya wanawake na Jinsia ya mwaka
2000.
- Hali ya vyombo vya kusimamia, kutekeleza na kutoa haki kwa wanawake katika kata husika.
( hii ilikuwa ni kwa siku ya Kwanza)
Siku ya Pili:- tulishughulikia haya:
- Ushiriki wa jamii haswa wanaume na wanawake katika shughuli za kiuchumi/maendeleo.
- Aidha tulifanya majadiliano kuhusu changamoto juu ya wajibu wa viongozi katika kutekeleza sera ya MWJ ya mwaka 2000 na nini kifanyike ili kukabiliana na changamoto hizo.
Wapi:- katika kata sita za mradi kama ilivyotajwa huko nyuma. Maswala haya yaliwahusu viongozi wa mabaraza ya Kata na wawakilishi wa wananchi katika kata sita za mradi.
Idadi kwa kila kata ilikuwa washiriki 30, ambapo jumla ya washiriki 180 walinufaika na mafunzo hayo.
Mafanikio ya jumla.
1. ushirikiano mzuri kati ya watendaji wa Kata na shirika letu na hatimaye kufanikiwa kufanyika kwa mikutano yote 12( kwa kata sita kila Kata siku mbili) kama ilivyopangwa.
2. kupokelewa vizuri kwa sera na kueleweka miongoni mwa viongozi washiriki wa mikutano hiyo.
3.Viongozi kutambua changamoto zinazowakabili na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto hizo.
4. Ujembe wa sera kuwafikia/kuifikia jamii kwa urahisi kupitia vipeperushi na mabango yenye ujumbe murua/mwepesi.
6. jamii kutambua haki zao za msingi kama Sera inavyofafanua.
7. Kuanza kuripotiwa kwa matukio ya unyanyasaji kijinsia kupitia ofisi zetu za kigoma na Kasulu.
8. Shirika letu ikiwa ni pamoja na FCS kuendelea kufahamika miongoni mwa jamii haswa ngazi ya vijiji na Wilaya.
9. Ushiriki wa vyombo vya habari katika shughuli zetu kama vile: ITV, RFA, Radio Kwizera, Star TV, channel Ten, na vyombo vya magazeti kama Uhuru, Habari leo n.k.
10. Shirika kufanikiwa kupata usafiri wa Pikipiki, pamoja na vitendea kazi kama vile Scanner machine na mtando wa internet na Printer.
Shuguli ya Kwanza: Kuandaa mikutano sita katika ngazi ya kata kwa kila kata yenye lengo la kuwakutanisha wajumbe wa mabaraza ya kata na wawakilishi wa wananchi ili kutoa ufafanuzi juu ya sera ya maendeleo ya wanawake na jinsia na pia kueleza nafasi yao katika kutekeleza sera hiyo. (Siku mbili kila Kata)
1. Chakula kwa washiriki 30@ 5000 x 30 x 2 x kata 6 = 1,800,000
2. soda/maji kwa washiriki 30@1000 x 30 x siku 2 x Kata 6 = 720,000
3. Chai washiriki 30@ 1000 x 30 x 2 x kata 6= 360,000
4. Ununuzi wa limu kwa ajili barua za mialiko limu 4@ 10,000 x 4= 40,000
5. Ununuzi wa Bahasha 190@50x 190= 9,500
6. Note Book 180@1000 x 180= 180,000
7. Flip chart 5@ 8000 x 5= 40,000
8. marker Pen Box 5@ 7000x 5= 35,000
9.Maskin Tape 15@500 x 15= 7500
10.nauli kwa wawezeshaji na watendaji wa asasi @ 15000 x 3 x 2 x6 540,000
11. Ukumbi 100000 x 2 x Kata 1(Kasulu mjini) 200,000
12. Gharama za wawezeshaji 50000 x wawezeshaji 2 x 2x siku 12= 1,200,000
13. Malazi na chakula cha usiku kwa wawezeshaji 2+ Mratibu 540,000
Jumla kwa shughuli ya kwanza (zilizotumika) ni 5,672,000
2. shughuli ya Pili: Kutengeneza vipeperushi na mabango yenye tafsiri rahisi ya sera ya maendeleo ya wanawake na jinsia na kivisambaza kwa wingi katika maeneo ya vijijini ili wananchi waweze kuielewa sera na kufuatilia utekelezaji wake.
1.2.1 Kutengeneza vipeperushi 2000@ 1000 x 2000 2,000,000
1.2.2 kutengeneza Mabango Posters 1000@ 1000 x 1000 1,000,000
1.2.3 Gharama za usambazaji kwa kata 6.@ 10,000x6 60,000
Jumla ya ndogo (Matumizi) 3,060,000
3. Shughuli ya Tatu: Kuendesha Mikutano /Jukwaa la utetezi na ushawishi ambapo wahanga wa matukio ya unyanyasaji walialikwa kutoa changamoto walizopitia na mikakati kuandaliwa.
( Wilaya ya Kasulu). mkutano/Jukwaa mmoja ( robo ya kwanza)
3.1. Gharama za ukumbi kwa siku 1@ 100,000 x 1 100,000
3.2. Gharama za mwezeshaji 1@ 100,000 x siku moja 100,000
3.3. Gharama za chai washiriki 50 @2000 x 50 x siku moja 100,000
3.4. Chakula cha mchana kwa washiriki 50 @ 5000 x 50 x 1 250,000
3.5. Malazi washiriki (toka Vijijini 40 @10,000 x 40 x 1 400,000
3.6. Usafiri wa wawakilishi toka vijijini 40@ 15,000 x 40 x siku 1 600,000
3.7. Note Book kwa washiriki 50@ 1000 x 50 50,000
3.8. Chakula cha usiku kwa washiriki 40 toka vijijini @ 5000 x 40 x 1. 200,000
Jumla ya Matumizi (kwa Wilaya ya Kasulu) 1,800,000
4. shughuli ya Nne: Ufuatiliaji na Tathimini Ufuatiliaji kufanyika angalau mara moja kwa mwezi ili kuona jinsi watendaji wa kata wanavyotekeleza Sera katika kata husika.
4.1. Ununuzi wa Petrol ya Pikipiki ( Ufuatiliaji) lita 61.25 @ 2000 x 61.25 122,500
4.2. Ununuzi wa limu A4 kwa ajili ya fomu za tathimini. @ 10,000 x 4 38,000
4.3. Chakula na malazi siku 2 kila kata @15000 x siku 2 x kata 3 90,000
4.4. Mwezeshaji wa tathimini siku 3 kwa kata 3@ 100,000 x3 300,000
4.5. Nauli watendaji 3@ 10,000 x 4 x siku 3 120,000
4.6. Chakula na malazi wakati wa tathimini watu 4@ 15,000x 4 x 3 180,000
Jumla ya matumizi sughuli ya nne: 978,000
Gharama za utawala.
6.1. Posho ya mratibu miezi mitatu @200,000 x 3 = 600,000
6.2. Posho ya Mhasibu/Mtunza Hazina Miezi Mitatu @ 150,000 x 3= 450,000
6.3. Gharama za mawasiliano kila mwezi Miezi 3@ 20,000 x 3 60,000
6.4. Ghaarama za shajala kwa mwezi @20,000 x 3 60,000
6.5. Gharama za pango (Ofisi) kwa Mwezi @50,000 x 3 150,000
6.6. Ununuzi wa pikipiki 1@ 2,450,000 2,450,000
6.7. Ununuzi wa Printer 1@ 500,000 x 1= 500,000
6.8. Kuweka Internet ( Zain Mordem) 1 @ 100,000 100,000
6.9. Ununuzi wa wino wa printer 1 Catridge Hp 12A @ 60,000 165,000
6.10. Ununuzi wa scaner Machine 1@330,000 x 1 330,000
Jumla ya gharama za matumizi Utawala 4,865,000
Mafanikio au Matunda ya Mradi
- Matukio mbalimbali ya unyanyasaji kijinsia dhidi ya wanawake yameripotiwa na hatu zinachukuliwa kwa wahusika kama sehemu ya mikakati ya mabaraza ya kata na Halmsahuri za Wilaya husika kupambana na tatizo hilo.
- Wanawake kuwa na ujasiri katika kueleza changamoto walizokutana nazo dhidi ya vitendo vya unyanyasaji kjinsia.
-Wanawake wametambua wapi wapeleke kesi zao dhidi ya vitendo vya unyanyasaji kijinsia na sasa wameanza kuripoti vitendo wanavyotendewa vya unyanyasaji.
- Kuwekwa kwa mpango maalumu wa kuiomba serikali utunge sheriaitakayotoa adhabu kali kwa wanaume na wanawake wanaotekeleza familia zao. ( Mapendekezo ya wadau wa mradi)
- Baadhi ya Serikali za Vijiji zilikuwa haziendeshi mikutano ya robo mwaka, sasa wameanza katika Kata ya Kagongo.
- Uongozi wa Kituo cha afya Nguruka, umetambua umhimu wa utekelezaji wa sera kwa vitendo na sasa unahamasisha jamii kupanga uzazi na kutambua umhimu wa wanawake wajawazito kuhudhulia kliniki.
-Vyombo vya habari sasa vimeanza kualika watendaji wa asasi yetu katika mijadala ya moja kwa moja katika studio zao zilizoko kigoma na kushiriki kutoa elimu kwa njia ya radio, Kama vile kipindi cha darubini, na Asubuhi njema. ( RFA na radio kwizera) haya ni mabadiriko makubwa.
-Ubora wa lengo mahsusi la mradi.
-mabango yalibandikwa katika maeneo mbalimbali yameongeza uelewa zaidi hata kwa wale ambao hawakushiriki moja kwa moja kwa mradi.
-Jinsi asasi yetu ilivyowashirikisha waandishi wa habari katika mradi wetu.
Mambo Mliyojifunza
Maelezo |
---|
Katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo wa mradi huu, tumepata mawazo makuu mapya yafuatayo kama sehemu ya uzoefu: 1. Sera nyingi zinazoandaliwa na serikali hazifiki/kuwafikia wadau wa maendeleo haswa ngazi ya Kata na Vijiji. 2. Katika kutekeleza mradi huu, tumejifunza kuwa ndoa nyingi ziko katika mazingira magumu kutokana na hali ya mfume dume kuendelea kushamiri katika maeneo yote ya tulikotekeleza mradi huu. 3.Viongozi wengi wa mabaraza ya Kata hawajui wajibu wao. |
Mabaraza ya Kata yaliyo mengi yanaendesha shughuli za utoaji haki kwa uzoefu na hayana mwongozo wa sheria mbalimbali. |
Ipo haja ya asasi za kirai kusaidia kuwajengea uwezo jamii haswa wale walioko katika famili kufundishwa juu ya kuwa na maadili mema, haswa katika kipindi cha malezi ya mtoto ili kuwa na taifa lenye viongozi na jamii bora siku zijazo. |
Tumejifunza kuwa vyombo vya habari ni mhimu sana katika kushirikishwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali na hivyo itasaidia jamii kubwa zaidi kushiriki katika mijadala kwa njia ya radio, hatimaye jamii itakuwa na mabadiliko makubwa kijamii, kielimu, kiutamaduni na kiuchumi. |
Utegemezi wa vyombo vya usafiri kwa asasi za kiraia unaweza kuchangia kuchelewa kufikia malengo waliyojipangia. |
Mfumo wa mahusiano ya viongozi wa vyama vya siasa ngazi ya Kata hadi Vijiji unachangia kuzorotesha masuala ya utekelezaji wa sera haswa ya maendeleoa ya wanawake na jinsia. hivyo tumejifunza kwamba ipo haja ya asasi za kiraia kutoa elimu kwa viongozi wa vyama vya siasa toka ngazi ya Wilaya hadi Kijiji ili watambue umhimu wa siasa katika kutekeleza sera mbalimbali za Serikali. |
Changamoto
Changamoto | Namna mlivyokabiliana nazo |
---|---|
Kwa ujumla hakuna changamoto zilizojitokeza na kusababisha kutofikia malengo. hata hivyo changamoto kubwa ilikuwa kwenye bajeti yetu haswa kwenye upande wa nauli za washiriki wa mkutano ngazi ya Kata. Kwenye bajeti tulijikuta kifungu cha nauli hakiupo. | Tulifanya majadiliano na Watendaji wa Kata ili waweze kutusaidia kutumia Madarasa ya Shule za Msingi/Sekondari bila gharama ili gharama za kulipia ukumbi zitumike kulipia nauli. Isipokuwa kwa upande wa kasulu tulipunguza gharama ya matumizi ya ununuzi wa petroli na kulipia ukumbi. |
Malalamiko ya washiriki juu ya kiwango cha nauli kilicholipwa cha Tsh 5000, wakati wa mikutano ya Kata kuwa kidogo. |
Mahusiano
Wadau | Namna mlivyoshirikiana nayo |
---|---|
Serikali za Mitaa: - Watendaji wa Kata | Kabla ya mradi kufanyika, shirika letu lilifanya mawasiliano na Watendaji wa kata kwa kupeleka barua za utambulisho wa mradi, katika barua hizo, tulieleza lengo la mradi, kiasi cha fedha kilichotolewa na FCS, aina na idadi ya walengwa wa mradi. Aidha Uongozi wa shirika letu, Watendaji wa Kata, kwa kusirikiana na watendaji wa Vijiji tulifanikiwa kuwapata washiriki wa mikutano ya mabaraza ya Kata na washiriki wa jukwaa la utetezi na Ushawishi juu ya haki za wanawake na jinsia. |
Vyombo vya habari -Radio Kwizera-Kigoma -Radio Free Africa - Star TV -ITV -Magazeti Uhuru, Jambo leo. | Vyombo hivi vya habari, tulivishirikisha ili wahusika ( waandishi wa habari) nao wachangie hoja katika mijadala, kutokana na uzoefu walionao. aidha lengo lingine la kuwashirikisha ilikuwa kusaidia kufikisha ujumbe kwa jamii ( kwa kiwango kikubwa). Kupitia vyombo, hiv |
Dini. Roman Katoliki -FPCT Anglican -Islamu | Hawa walishirikishwa ili kusaidia kuleta ufanisi wa kutekelezwa kwa sera ya maendeleo ya wanawake na jinsia. Pia wao wanasikilizwa na watu wengi kulingana na hadhi yao. Walishiriki katika shughuli zote za utekelezaji wa mradi huu kwa robo hii ya kwanza. |
Vyama vya siasa. CCM CHADEMA CUF NCCR | Viongozi wa vyama walishirikishwa kwa kuhudhulia mikutano ya Mabaraza ya Kata. na kuruhusiwa kuchangia mada mbalimbali.Lakini tuliwashirikisha ili waweze kupata ujumbe wa sera, kwani wanawake wengi wanapojitokeza kugombea nafasi za uongozi (Kisiasa) baadhi ya viongozi wa vyama huwakwamisha wanawake katika kiny'nganyiro cha kura za maoni. na hivyo kufanya sera hii isitekelezeke. |
Idara ya Afya: Mabwana Afya Wakuu wa vituoa vya afya.Zahanati | hawa tuliwashirikisha ili waweze kuitambua sera kwa kuhdudhuria mikutano ya Kata, iliyoendeshwa kwa muda wa siku mbili kila kata. lengo lilikuwa ni kuwawezesha kuijua sera na kisha kuitekeleza kwa vitendo kwa kutoa huduma bora kwa Haswa mama wajawazito na watoto. |
Mipango ya Baadae
Shughuli Zilizopangwa | Mwezi wa 1 | Mwezi wa 2 | Mwezi wa 3 |
---|---|---|---|
Kuunda Kikosi cha wafuatiliaji wa masuala ya unyanyasaji wa wanawake vijijini ( Gender Violance Monitoring Group) na kuripoti na pia kutafuta mfumo bora wa kuripoti matukio hayo | xxxx | ||
kuendesha jukwaa la utetezi na ushawishi ambapo wahanga wa matukio ya unyanyasaji wataalikwa kutoa changamoto walizopitia na mikakati ya pamoja kuandaliwa. | xxxx | ||
Kufanya ufuataliaji na tahimini kwa kutemebelea Kila kata angalau mara moja kwa mwezi | xx | xx | xx |
gharama za utawala: Posho,Mawasiliano na shajala. | xxx | xx | xxxx |
Walengwa Waliofikiwa
Walengwa wa moja kwa moja | Walengwa wasio wa moja kwa moja | ||
---|---|---|---|
Wajane na Wagane | Wanawake | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) |
Wanaume | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Jumla | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Watu wanaoishi na VVU/UKIMWI | Wanawake | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) |
Wanaume | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Jumla | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Wazee | Wanawake | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) |
Wanaume | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Jumla | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Watoto Yatima | Wanawake | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) |
Wanaume | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Jumla | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Watoto | Wanawake | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) |
Wanaume | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Jumla | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Watu wenye Ulemavu | Wanawake | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) |
Wanaume | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Jumla | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Vijana | Wanawake | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) |
Wanaume | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Jumla | (Hakuna jibu) | (Hakuna jibu) | |
Watu wengine | Wanawake | 79 | 31200 |
Wanaume | 146 | 36800 | |
Jumla | 225 | 68000 |
Matukio Mliyoyahudhuria
Aina ya Tukio | Lini | Mambo uliyojifunza | Hatua zilizochukuliwa |
---|---|---|---|
mafunzo ya usimamizi wa ruzuku | Agosti | Umuhimu/Usimamizi wa fedha - udhibiti wa fedha - Utenganishi wa majukumu Madaraka na mipaka yake - Uandaaji na uhifadhi wa kumbukumbu za mahesabu - Uandaaji w taarifa ya fedha-foundation. | kutekeleza mafunzo hayo kwa vitendo, kwa kuandaa vitabu vya kumbukumbu za fedha, na nyaraka nyingine kama voucher, fomu ya kuombea fedha, na mikataba ya wawezeshaji . kuweka kumbukumbu vizuri |
Uandishi wa taarifa | kufuata hadidu za rejea za somo hili na kuzitekeleza kwa vitendo wakati wa uandishi wa taarifa zetu za shirika. |
Viambatanisho
Afisa Mipango na Mratibu Miradi wa shirika la Tanzania Women Social Economic Development and Human Rights Organization Bwana William Daudi amesema kwamba, shirika lake kwa sasa linatarajia kuendesha mradi wa kuongeza nguvu katika utekelezaji wa Sera ya maendeleo ya wanawake na jinsia ya mwaka 2000. akizungumza katika kikao cha Kamati kuu Mapema wiki jana, alisema kwamba shirika lake litatekeleza mradi wenye thamani ya shilingi arobaini na nne milioni na laki nane na hamsini elfu ( 44,850,000) ambapo kata sita zilizoko katika Wilaya ya Kigoma na kasulu zitanufaika. Ruzuku hiyo inatolewa na shirika la Foundation for Civil Society.
Aidha baada ya Taarifa hiyo, mratibu huyo kwa sasa yuko Dar es Salaam kuhudhulia kikao cha HUMAN RIGHTS AND BUSINESS NETWORK ambacho kinafanyika katika Hotel ya Peackock Hotel mjini Dar es Salaam. Aidha alieleza kwamba kikao hicho kitashughulikia masula ya kutiwa sahihi kwa katiba ya mtandao huo. pili kupitia joint proposal na mpango mkakati. aidha washiriki pia watapata mafunzo juu ya mbinu za kufanya fundaraising. Kikao hicho kitahudhuliwa na mashirika kumi (10) wanaanzilishi, na wataalamu toka Ulaya na kutoka MDF-ESA toka Arusha. Kikao hicho kitafanyika kwa muda was siku nne (4) ambapo kitaanza tarehe 17 hadi 20 january 2011.
Imetolewa na idara ya habari na Mahusiano
Kigoma Makao Makuu.