Envaya
Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

large.jpg

Mkurugenzi wa Africa Upendo group akiwa anasikiliza kwa makini vijana wakiwa katika mafunzo ya Ulinzi Salama katika Mtaa wa Makuburi -Kibangu.Aliyevaa tisheti ya kijani aliweza kuwakamata majambazi waliopora fedha kule buguruni zaidi ya milioni 28.Anaitwa Miraji Ramadhani Rashid.

large.jpg

Vijana wakijadiliana katika mazoezi waliyopewa.Wako katika mafunzo ya ujasiriamali na ICT

large.jpg

vijana wanajipa mazoezi katika mafunzo ya kujiamini.

large.jpg

Akina mama wakijadiliana jinsi ya kuendesha biashara zao kwa kutoa mifano mbalimbali katika Mafunzo ambayo yaliendeshwa na partners wetu ICTD Learning Centre na DOT

large.jpg

Vijana wakijadiliana mambo huku wakiwa katika mafunzo ya Computer na ujasiriamali.

large.jpg

Mkurugenzi wa Africa Upendo Group akiwa na Mwalimu Winfrida Mgina wakipeana mawazo kama wanawake jinsi ya kuwasaidia wasichana na akina mama ambao hawakubahatika kusoma na kujiendeleza.

Africa Upendo Group imeanzisha program inayojulikana kama SISI KWA SISI.Program hii ni kwa ajili ya wale wote ambao wangependa kujifunza kutumia Computer na kujua kuzungumza kiingereza rika lolote lile.Program hii ni bure haina gharama yoyote ni mtu kuchukua form pale ofisini kwetu na kwa kwa wale wote ambao wanaishi katika Jimbo la Ubungo tumependa kuanzia pale ofisi yetu ilipo kwanza ndipo tutakaposambaa pote Tanzania.Vijana wetu waalimu ni wengi na bado tunahitaji wengi wa kujitolea.Tumesambaza form kwa serikali ya mitaa kadhaa lakini bado tunaweza kupeleka mahali kama watahitaji.Tunamkaribisha mtu yoyote awe ni kijana au mzee waalimu wetu wanauwezo mkubwa wa kufundisha.Wengi ni vijana waliomaliza digree zao wapo katika ajira au bado wanasubiri kupata ajira.Tumeona nchi za jirani watu wakiingia humu kwetu kwa kasi kubwa kwa sababu ya lugha na ufahamu mzuri wa jinsi ya kutumia mitandao na ama computer wakati watu wengi hapa nchini hawajui namna ya kutumia ndio maana tumeliona hili na kuamua kuanzisha program hii.Tuna imani kubwa kuwa watu wenye mapenzi mema watatuunga mkono hata kutusaidia kubeba jukumu hili kubwa.Tunahitaji computer zaidi na waalimu wa kujitolea.Shime tushirikiane kutokomeza ujinga.Pia tunategemea kuungwa mkono zaidi na wadau wetu yaani Dar es Salaam Teknohama Business Incubator(DTBI) pamoja na COSTECH chini ya Eng.George Mulamula.Pia kama wapo wadau wengine tushirikiane tunahitaji pia NGO huko mikoani tushirikiane nao kutekeleza jambo hili.Karibuni

Vijana wa Africa Upendo Group wamekuwa wakikutana mara kwa mara kujadiliana maswala mbalimbali yanayohusu vijana.

kutokana na wimbi la vijana wengi ambao wanamaliza vyuo vikuu lakini kutokana na mashirika na serikali kung'ang'ania kuwa vijana hawa wawe na uzoefu katika kazi na kwa kuzingatia kuwa vijana hawa ndio kwanza wanatoka kwenye vyuo wamekuwa katika kuhangaika sana.

Katika asasi yetu ya Africa Upendo Group tumekuwa na kitengo maalum cha kuwasaidia vijana kama hawa kwa kuwapatia mafunzo mbalimbali na kwa pamoja kwa njia ya kujitolea tumeweza kuwa na mikutano ya mara kwa mara.Ili kubaini njia mbadala katika kuona kuwa vijana wanapokuwa bado wapo mashuleni na baada ya kutoka wanaweza kujiajiri wenyewe kwa kufanya mambo mbalimbali yakiwemo tafiti mbalimbali.Katika kuliona hili vijana hawa wametengeneza tovuti ambayo itajulikana kama www.ICT4TD.co.tz ambayo itakuwa na shughuli mbalimbali zikiwemo vijana wengi kujitolea kufundisha masomo mbalimbali kama lugha ya kijerumani,kifaransa,Kiingereza,masomo ya Teknohama watakuwa wanajitolea zaidi katika maswala yanayohusu jamii kama usafi na utunzaji wa mazingira,Makazi au kaya,vijana walioathiriwa au wako katika hatari ya kuambukizwa UKIMWI na madawa ya kulevya n.k kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali ikiwemo Envaya,DTBI,Restless,Global Exchange,VSO wizara ya habari utamaduni na maendeleo ya vijana .

Katika kutekeleza majukumu yao mbalimbali vijana wamekuwa na makongamano mbalimbali kama siku ya kujitolea duniani ambapo vijana waliweza kubadilishana uzoefu na mambo mbalimbali pia waliweza kuhudhuria mkutano ambao ulihudumiwa wa DTBI,na kwa pamoja walikutana na vijana kutoka chuo kikuu cha MIT kutoka Marekani na kubadilishana mawazo na wamekuwa wakifanya mambo mbalimbali ya mifano ya hayo.

Pia wameunda Stearing commitee ambayo itakuwa na majukumu mbalimbali kwa makundi mbalimbali.Ili kuboresha zaidi na kuhakikisha kuwa vijana wanapata taarifa za msingi kutoka nje na ndani ya nchi yao.Website hii imemalizika na iko katika hatua ya kuzinduliwa karibuni.

Hapa chini utaona moja ya kamati ambayo inashughulika na kuratibu makundi mbalimbali chini ya mwenyekiti wake Albert.Huyu ni kijana aliyemaliza mafunzo ya Teknohama kwenye chuo kikuu cha Dodoma na Moderator akiwa ni Neatness Msemo ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji katika Asasi hii.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

kwa kukuona picha nyingi zaidi bonyeza link hapo chini:

http://ict4td.webs.com/apps/photos/album?albumid=12923434

Dar es Salaam Flooding Community Survey

Mtaa wa mwongozo Lukas Sekelo
barabara,maji,miundo mbinu,fedha na makazi
nyumba yangu nusu imezolewa na maji
maisha ni ya shida sana kwani tunaishi juu ya mto hakun tena nafasi sehemu kubwa imechukuliwa na maji
maji hayafai kabisa
Before flooding: (No Response)Now: (No Response)

large.jpg

Samaki akiwa amekufa mda mfupi kwa kukosa hewa