Envaya
Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Icyongereza. Edit translations
Wakihabima sasa imepata usajili rasmi toka wizara ya maendeleo ya jamii jinsia na watoto. Hii ni baada ya juhudi za uongozi na wanachama. Aidha msaada mkubwa wa ushauri toka kwa mratibu wa mashirika wa halmashauri ya mji Masasi, na usaidizi mkubwa toka LHRC dawati la wasaidizi wa kisheria na ofisi kuu vimewezesha zoezi hilo kufanikiwa. Shukrani nyingi ziende kwa kila mmoja.
Wakihabima imebahatika kuwa moja ya asasi zilizotoa waangalizi wa uchaguzi wa ubunge jimbo la Masasi uliokuwa umeahirishwa wakati wa uchaguzi mkuu Oktoba 20 kutokana na kufariki kwa mmoja ya wagombea Dr. Emmanuel Makaidi wa NLD. Kazi hii waliifanya kwa mwamvuli wa TACCEO chini ya kituo cha Sheria na haki za Binadamu LHRC. Walioshiriki walikuwa; Noel Mwembere, Tanmoza Fungafunga, Donald Simonje, Mwanaafa W. Malenga, Irene Liyumba, Frank Liweta, Monica Mzula, Damas Mlaponi, Mwinda Mkwamba, Maurice Ng'hitu, Edna Ngasiwa, Sekioni Joseph, Yakobo Yohana na Anjelina Saidia. Hawa waliungana na jopo laTACCEO/LHRC lililoongozwa na Dr. Geoffrey Chambua. Uchaguzi huo ulifanyika Disemba 20/2015 na mgombea wa CCM alipata ushindi.
Wakihabima imefanikiwa kuendesha kliniki ya msaada wa kisheria wilayani Masasi ambapo wanasheria 4 toka LHRC walikuja na kutoa ushauri na usaidizi wa kufuatilia mashauri yaliyokosa mwelekeo pia mafunzo yanayohusu masuala ya ndoa, mirathi, ardhi, haki za mtoto na sheria ya vijiji ya mwaka 1999. Kliniki hiyo ilifanyika kuanzia tarehe 9 hadi 13 Novemba2015 kwenye kata za Masasi mjini, Nanganga, Nanjota, Mbonde na Chiwale.