Injira
ASASI YA UKOMBOZI WA VIJANA TANZANIA ( AUVITA)

ASASI YA UKOMBOZI WA VIJANA TANZANIA ( AUVITA)

Bunda, Tanzania

Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Icyongereza. Edit translations
    UGONJWA WA MAFUA YA KUKU
Ugonjwa huu umekuwa ni hatari sna hasa kutokana na usumbufu wake wa kimatibabu pale unapoingi katika shamba la mkulima mfugaji wa kuku, hapa nakuletea maelezo mafupi kuhusu ugojwa huu.
 
Ni ugonjwa unaoitwa infectious coryza huenezwa na bacteria. anaeitwa (hemophilus paragallinarum).
Ugonjwa huu hushambulia  kuku aina zote. Na usipo kuwa makini kwenye usafi wa banda na vyombo , kuruhusu watu kuingia ovyo bandani au kuku wa jirani kuja kuingia kwenye banda lako; ugonjwa huu unaweza shambulia kuku wako kwa kila wiki.
 
*DALILI ZA UGONJWA HUU*  =
 
_Kuvimba uso chini na nyuma ya macho.
_Kupumua kwa shida na kukoroma
_Kutoka makamasi puani,
_ Mdomoni kuwa na hali ya mterezo
_Macho kuvimba
_Kushindwa kula.
_Kupiga chafya , macho kuonekana kama yanatoka machozi
 
*JINSI UGONJWA UNAVYOENEA:*
 
_Ugonjwa huu huenea kutokana kuku mmoja kwenda kwa kuku mwingine, au kutoka banda moja kwenda banda lingine.
 
_Chanzo cha maambukizi ni maji na chakula kilicho chafuliwa na kinyesi cha kuku Mgonjwa.
_Ugonjwa huu uneea na kuambukizwa kwa mfumo wa hewa  pale kuku wanapopiga chafya.
 
*UNASHAURIWA*
 
Pindi ugonjwa unapo ingia bandani kwako wale kuku watakao onesha dalili za ugonjwa huu , watenge kisha wape tiba kuku wako wote; unatakiwa kuwatenga kwa ajili ya kupunguza maambukizi bandani.
 
*DALILI ZA MZOGA UKIUPASUA*
Usaha mweupe hadi njano huonekana kwenye macho na ndani ya pua
 
*MATIBABU*
 
Zipo dawa nyingi za kutibu ugonjwa huu  antibiotic/ sulfa. Hizi ni baadhi tu.
 
Fluban
Ganadexil
Tylodox
Teramycin.nk
 
Ushauri:Tumia fluban kwa Kuku wanaooneshadalili za mafua  bila  vifo.
 
Tumia  Ganadexil/tylodox kwa Kuku wenye mafua  ambao tayali kuna vifo vimetokea.

large.jpg

Tumeamua kujikita katika shughuli za kilimo hususani kilimo cha bustani na ufugaji wa kuku. Ni dhamira yetu kuhakikisha kuwa jamii inapata lishe bora na salama kwa afya, ni fahari kwetu kuona kuwa vijana wanaelimika na kuchagua mfumo wa maisha kiuchimi kupitia rasilimali zinazo wazunguka kama nyezo ya kuwainua kiuchumi, jamii inahitaji nyama ya kuku na mazao mengine ya kuku kama Mayai na mbolea ya kinyesi cha kuku. Mazao haya ya kuku ni frusa kwa vijana kwani wakielimishwa na wakawa tiari kuwekeza katika sekta ya ufugaji kupitia Ndege jamii ya kuku watakuwa wamekubali kutatua Matatizo yaliyopo katika jamii yatokanayo na uhaba wa mazao ya kuku. Sisi kama ASASI ya AUVITA tumejidhatiti kwa dhati kuwekeza kwa vijana wa Tanzania ili kuwawezesha kukabiliana na uhaba wa ukosefu wa ajira. Takwimu zonaonesha kuwa idadi ya watu inazidi kuongezeka kila leo na watu Hawa wanahitaji kula na wenyejukumu la kuwalisha ni sisi vijana kwa kuwekeza katika sekta ya kilimo. Hivyo tukiwa kama vijana tunatoa rai kwa watanzania vijana kuwekeza katika sekta ya kilimo ili kujikwamua kiuchumi na kukidhi nahitaji ya Chakula. Pichani ni kuku wa Kienyeji walioboreshwa kwenye asili ya India.

TANZANIA NA UZALENDO WETU TUMEKOSEA WAPI?

Uzalendo ni kitendo cha mtu kuipenda nchi yake, rasilimali zilizomo na watu wake kwa moyo wa dhati kwa kuilinda, kuithamini wakati wote na mahali popote.

Uzalendo katika nchi ndio chanzo cha maendeleo na usawa kwa watu wote nchini. Uzalendo unaleta haki, uzalendo unajenga misingi ya kujaliana, uzalendo ndio chachu ya matumizi ya rasilimali za nchi kwa usawa, uzalendo unatujengea undugu na amani, uzalendo unajenga na kudumisha upendo, uzalendo unajenga na kudumisha ushirikiano, uzalendo unajenga misingi ya uwajibikaji kwa wanajamii, uzalendo huondoa unyonyaji na matabaka katika jamii.

Uzalendo ni upendo na dhana ya hiari ya mtu binafsi uzalendo hujengwa kutoka moyoni mwa mtu, wakati mwingine uzalendo hujegwa na wanajamii kipitia misingi ya maisha wanayoyaishi na itikadi ya kisiasa  miongoni mwa wanajamii. Hivyo mtu anaweza kuzaliwa akiwa mzalendo au  itikadi ya kisiasa na misingi ya maisha katika jamii inaweza kumjenga mtu katika hali ya uzalendo.

Uzalendo unagawanywa katika aina mbili; a) uzalendo wa kihistoria ambao unatokana na maisha ya watu waliotangulia katika jamii. b) uzalendo wa kiutu. Huu ni uzalendo ambao huchukulia binadamu kama alivyo. Mfano katika Biblia maandiko yanasema mpende jirani yako kama nafsi yako.

Katika taifa letu dhana ya uzalendo imepotea miongoni mwa wanajamii. Historia inaonesha Tanzania imepitia vipindi mbalimbali; kipindi cha kabla ya ukoloni, wakati wa ukoloni, wakati wa kupigania uhuru na  wakati baada ya uhuru. Kila kipindi kilijengwa na misingi yake ya uzalendo.

Kipindi kabla ya ukoloni historia inaonesha kuwa mababu zetu waliishi katika misingi ya umoja mshikamano na undugu, walifanya kazi kwa kushilikiana waliishi kama wamoja, rasilimali ziliwanufaisha wote watu wote walikuwa na haki sawa katika utumiaji wa rasilimali. Kipindi hiki kilitawaliwa sana na uzalendo wa  kiutu.

Kipindi cha ukoloni. Historia inaonesha kuwa kipindi hiki wakoloni walitumia kila mbinu kuuvunja na kuundoa kabisa uzalendo miongoni mwa wanajamii. Walitujengea mioyo ya chuki, walituondolea umoja, walitujengea ubaguzi, walitugawa ili watutawale. Yote haya waliyafanya kwa manufaa yao binafsi ya kuzinyonya rasilimali za waafrika, walitumia Ardhi yetu kujinufaisha , walitumia  udhaifu wetu kutufarakanisha, walitujengea matabaka katika jamii. walichonacho walikuwa nacho na wasiokuwa nacho waliendelea kukosa, elimu ilitolewa kwa misingi ya ubaguzi katika jamii, rasilimali za nchi zilitumika kuwanufaisha wachache wenye vyeo na madaraka tu. Hakika wakoloni walifanikiwa kutufarakanisha waafrika na kutuondolea uzalendo wetu.

Wakati wa kupigania uhuru. Hiki ni kipindi ambacho  waafrika wenyewe tulianza kujijengea  mioyo ya uzalendo tulioupoteza kupitia ukoloni, tulijijenga pamoja kushirikiana na kupambana dhidi ya ukoloni. Kipindi hiki mioyo ya uzalendo ilijegwa upya katika jamii ya watanzania. Baba wa Taifa alitumia juhudi zake kupitia Chama cha TANU kutuunganisha pamoja , tuwe wamoja , kutujengea upendo na baadae kushirikiana kudai uhuru wetu tukiwa kitu kimoja na wamoja.

Waasisi wetu walitumia juhudi zao kuujenga uzalendo na upendo katika jamii wakaiacha mizizi kwa mategemeo kwamba kizazi kilichofuata kingeendeleza hali ile.

Tanzania ya sasa si ile ya waasisi wetu, uzalendo tuliojengewa hatunao tena, umoja na mshikamano vimepotea sasa kila mtu akwenda kivyake nchi inapoteza mwelekeo , umasikini unakua kiuhalisia lakini unapungua kitakwimu, matabaka yanazidi kuongezeka makuadi wa kupoteza uzalendo wetu wanaongezeka kila siku, rasilimali sasa zinawanufaisha  watu baadhi. Kwa mioyo migumu waliyo nayo sasa hata madaraka wanarithishana ili tu kujilinda.  Taifa linahitaji jitihada za kila mmoja wetu kuhakikisha kuwa tunautetea na kuuendeleza uzalendo wetu kwa maendeleo yetu . matabaka tuyaonayo leo ni matokeo ya kukosekana kwa uzalendo miongoni mwetu, misingi ya utu, ummoja, undugu sasa tumeipoteza kila mtu anafanya ajualo. Mabadiliko yanaletwa na mimi na wewe tumia nafasi yako vizuri kujenga usawa, utu, uwajibikaji, undugu katika jamii kwa maendeleo ya Taifa letu.

 

 

 

 

TUNAIENZIJE SIKU YA MAZINGIRA?Umepanda mti leo?

Leo ni siku ya mazingira duniani ambayo inatukumbusha kuwa uhai wetu inalindwa na mazingira yetu, hivyo tukiwa kama wadau katika sekta ya mazingira tunawakalibisha wadua na wahifadhi mazingira ili kuu tetea uhai wetu kwani kuishi kwetu kunategemea mazingira yetu.

Nikweli kabisa kuwa hatunabudi kuyalinda na kuyahifadhi mazingira yetu na kuienzi siku hii kwa fulaha kwani inatupa matumaini mapya ya kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia ya nchi yanayo itikisa Dunia.

Mazingira yetu ni uhai wetu tuyalinde yatulinde. kama hatutaona umuhimu wa kuyalinda mazingira basi tunamtizamo wa kuyakatisha maisha yetu, Pamoja na uhifadhi wa mazingira tunayaweka mazingira ya uhai wa viumbe wengine katika hali safi yaani uhifadhi wetu wa mazingira unayaboresha si tu maisha ya binadamu bali na viumbe wengine.

Siku hii iwe chachu ya kutujengea misingi bora ya kuyaheshimu maeneo yaliyotengwa sehemu mbalimbali nchini kwa kuendelezwa kimazingira na kuyaheshimu maeneo haya, serikali hainabudi kushughulikia suala la mgawanyo wa maeneo yatuzungukayo kulingana na matumizi na kuzisimamia sheria kikamilifu.

Pia jamii ifahamu kuwa uhifadhi wa mazingira ni jukumu la kila mtu na inatupasa kushiriki wote kakamilifu juu ya suala zima la kuyahifadhi mazingira yetu.

Uhai wetu ni mazingira yetu tuyalinde yatulinde

 

MAANDIKO YA MWALIMU J. K. NYERER.

Kwa vijana kitabu hiki kinatufaa sana katika kutujengea misingi bora  ya uongozi na maadali memea naomba tukisome.

1: Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania (1994) - Mwl Nyerere

Download: http://dl.dropbox.com/u/52629254/dot...JK_Nyerere.pdf

2: Uongozi wetu na Hatma ya Tanzania - (Toleo la Kizazi Kipya)

Download: http://dl.dropbox.com/u/52629254/dot...wanakijiji.pdf

Ndugu Simba Mramba .

Mwanzilishi wa Asasi ya Ukombozi wa Vijana Tanzania (AUVITA) na ndiye mwenyekiti wa sasasi hiyo. Anawakaribisha vijana katika ukombozi mpya. Sikuzote huamini kuwa hamuna lisilowezekana Duniani na maisha ya mtu hupangwa na mtu mwenyewe, kwa ushirikiano na vijana kwa kuwapatia elimu mbalimbali maisha ya vijana yatabadilika na kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira.

Anasema kuwa.

Ni dhahili kabisa jamii ya watanzania  inahitaji elimu mbadala tofauti na ya darasani ambayo itawajengea wanajiamii hususani vijana misingi ya kujiami, kupata utashi wa kuhoji,kudadisi na kujua nini kinaendelea katika jamii. vijana wanatakiwa kuwa mfano wa kuigwa katika jamii washiriki katika shughuri za uzalishaji na maendeleo ya jamii zao kila mmoja, wafanye kazi kwa tija na kuwajibika popote walipo, waondoe mawazo mgando ya utegemezi na wajiajiri wenyewe kupitia rasilimali zinazo wazunguka, waondoe mtazamo hasi na wajenge fikra chanya juu ya maisha yao.

"umasikini si janga kama tetemeko la aridhi, njaa na mafuriko bali husababishwa na binadamu mwenyewe na anaweza kuuondoa mwenyewe kwa kutambua wajibu wake na kuwajibika" Simba Mramba.

"Ni bora ufanyekitu kwenyejamii ambacho sikumoja jamii itakukumbuka na kuishi kwako kutaonesha thamani katika jimii kuliko kuishi kusahaulika" Simba Mramba.