Envaya

HakiElimu

Amakuru

Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations
Haki Elimu HakiElimu

Kuwepo namba za kudumu za utambulisho wa watahiniwa (PCIN - Permanent Candidates identification number) kumaliza wizi #neshino - TAMANGSCO

Haki Elimu HakiElimu

Kuundwa mamlaka huru ya kusimamia elimu na mafunzo (Tanzania education and training regulatory authority) kumaliza wizi #neshino -TAMONGSCO

Haki Elimu HakiElimu

Waliothibitishwa na tume huru kuhusika na udanganyifu/wizi wa #neshino wachukuliwe hatua kali za kinidhamu na kisheria- TOMANGSCO

Haki Elimu HakiElimu

Pendekezo la kwanza la TOMANGSCO kumaliza tatizo la wizi wa #neshino ni Kuundwa kwa tume huru ya kuchunguza udanganyifu wa mitihani

Haki Elimu HakiElimu

TAMONGSCO yatoa mapendekezo ya muda mfupi na mrefu kumaliza wizi wa #neshino wakisema ni saratani inayolitafuna Taifa ,fuatilia kuyafahamu

Haki Elimu HakiElimu

TAMANGSCO hatuko tayari kushirikiana na mmiliki yeyote wa shule ambaye anaendelea kumlinda mkuu wa shule aliyethibitika ktk wizi wa #neshino

Haki Elimu HakiElimu

Mkoa wa Arusha unaongoza kwa wizi wa #neshino shule binafsi kuwa asilimia 48 ya shule zote zilizotuhumiwa ikifuatiwa na mkoa wa Kagera (13%)

Haki Elimu HakiElimu

Jumla ya wanachama 31 wa TAMONGSCO ambapo asilimia 61 ni shule za msingi; wametuhumiwa katika swala hili la udanganyifu/wizi wa #neshino

Haki Elimu HakiElimu

Shirikisho la wamiliki na mameneja wa shule na vyuo visivyo vya serikali (TAMONGSCO) latoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu #neshino

Kila la heri darasa la saba kwenye mitihani yenu ya mwisho

DSC05098.jpg
 

Wanafunzi wa darasa la saba nchini kote kesho na keshokutwa wanatarajia kuanza mitihani ya kumaliza elimu yao ya msingi ambapo kwa mara ya kwanza tekinolojia mpya iitwayo Optical Mark Reader (OMR) itatumika.
Watahiniwa watatumia fomu maalum za OMR kujibia mtihani na majibu yao yatasahihishwa kwa kutumia kompyuta.  Masomo yatakayotahiniwa katika mtihani huo ni Kiswahili, English Language, Sayansi, Hisabati na Maarifa ya Jamii. 
Jumla ya wanafunzi 894,881 wamesajiliwa  kufanya mtihani huo ambapo wavulana ni 426,285 sawa na asilimia 47.64  na wasichana ni 468,596  sawa na asilimia 52.36. Aidha, kati ya  wanafunzi hao, wapo wanafunzi 874,379  watakaofanya mtihani huo kwa lugha ya Kiswahili na wanafunzi 20,502 watafanya kwa lugha ya Kiingereza ambayo ndiyo waliyoitumia kujifunzia.  Wanafunzi wasioona waliosajiliwa kufanya mtihani ni 92 wakiwemo wavulana 53 na wasichana 39.  Watahiniwa wenye uono hafifu ambao huhitaji maandishi makubwa ni 495, kati yao wavulana ni 238 na wasichana ni 257.
 
Mwaka jana, watahiniwa 1,010,619 waliandikishwa kufanya mtihani wa darasa la saba mwaka 2011 ambapo jumla ya watahiniwa 993,324 waliandikishwa kufanya mtihani kwa lugha ya Kiswahili na watahiniwa 17,295 waliandikishwa kufanya mtihani kwa lugha ya  Kingereza ambayo walikuwa wakiitumia katika kujifunzia.

DSC05116.JPG


HakiElimu inawaasa wanafunzi, walimu na wadau wote kuzingatia misingi bora katika kipindi chote cha mitihani ya kumaliza elimu ya msingi ikiwa ni daraja moja muhimu linalotakiwa kuwavusha wanafunzi kutoka elimu ya msingi na kuingia elimu ya sekondari.
Kila la heri wanafunzi wote katika mitihani yenu.