Fungua
HakiElimu

HakiElimu

Dar Es Salaam , Tanzania

Maeneo ya ukurasa huu ni kwa Kiingereza. Hariri tafsiri
Haki Elimu HakiElimu

@lifeofmshaba @JohnKomakoma @piusmicky @Tanganyikan Tatizo ni usimamizi na udanganyifu uliokithiri kwa mtihani wa kushade tutegemee?

Haki Elimu HakiElimu

@lifeofmshaba @JohnKomakoma @piusmicky @Tanganyikan TATIZO NI JINSI GANI HIZO HESABU ZINAFANYIKA, KUSHADE CORRECT ANSWER, NI KIPIMO SAHIHI?

Haki Elimu HakiElimu

#Neshino will feature multiple-answer questions from which canditates are expected to shade correct answer using HB pencils( Daily News)

Haki Elimu HakiElimu

Makatibu na wakurugenzi wa Wizara ya Elimu kusimamia #neshino katika mikoa tofauti, lengo kudhibiti udanganyifu (Source Uhuru)

Haki Elimu HakiElimu

Naibu Waziri wa Elimu , Philipo Mulugo kusimamia mtihani wa #neshino katika mkoa wa Dar Es Salaam (Source Uhuru )

Haki Elimu HakiElimu

Waziri wa Elimu Dr. Shukuru Kawambwa kusimamia uchakuchuaji wa #neshino mkoa wa Pwani limeandika Uhuru

Haki Elimu HakiElimu

Mawaziri, wadau wa elimu na wasaidizi wao waandamizi wajitosa kusimamia mtihani wa darasa la saba. Lengo likiwa... http://t.co/b15hKl1e

Mtihani Mpya Darasa la Saba Haumchuji Anayejua Kusoma au Asiyejua - Walimu

Baadhi+ya+madarasa+ambayo+hutumika+kwa+m

Na Joachim Mushi, Thehabari.com

WAKATI wanafunzi wa darasa la Saba wakitarajia kuanza mitihani yao kesho baadhi ya walimu wa Sekondari wametoa angalizo kuwa mfumo mpya unaotarajiwa kutumika kwa usaishaji huenda ukapitisha (faulisha) wanafunzi wasio na sifa hivyo kuongeza idadi ya wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika kuingia sekondari.

Wakizungumza na Mtandao wa Thehabari.com hivi karibuni walisema mfumo huo wa usaishaji kwa kutumia mashine unaomtaka mwanafunzi kuweka kivuli kwenye jibu sahihi baada ya kuchagua ni rahisi kwa wanafunzi wasiokuwa na sifa kuibia kwa jirani yake kimazingira jambo ambalo ni hatari kulingana na mazingira ya vyumba vya mitihani.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kitopeni, Mjini Korogwe, Theodolph Karigita alisema mazingira ya vyumba vingi vya mitihani kwa shule za msingi ni rahisi kuibia kutokana na wanafunzi kusongamana kwenye vyumba vya mitihani, jambo ambalo kwa aina ya mtihani unaofanyika upo uwezekano wa kupata wanafunzi wasiokuwa na sifa kuingia kidato cha kwanza.


Baadhi+ya+madarasa+ambayo+hutumika+kwa+m
Mwalimu Karigita alisema kibaya zaidi kwa sasa hadi mtihani wa hisabati utafanyika kwa wanafunzi kuchangua yaani jibu sahihi kati ya A, B, C au D kabla ya kuweka kivuli kwenye jibu sahihi eneo, kitendo ambacho itakuwa rahisi kwa wasiojiweza kuangalia kwa mwanafunzi aliyejirani naye.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Boma ya Mjini Korogwe mkoani Tanga, Amir Nassoro alisema mtihani kama huo hauwezi kumpima mtoto kwamba anajua kusoma ama kuandika bali unaweza kujikuta unapitisha hata wale wasiokuwa na sifa kulingana na mazingira yetu. "Hivi unampimaje mtoto asiyejua kusoma na kuandika kwa kuchagua jibu sahihi au lisilokuwa sahihi...eneo kama hili hata asiyejua anaweza kubahatisha kwa kuandika A tu au B na hata C tu," alisema Nassoro.

Mwalimu Nassoro alitolea mfano kuwa mwaka 2010 alifanya utafiti mwepesi kwa kutunga mtihani wa kuchagua shuleni hapo na kuwapa wanafunzi kwa maelekezo kuwa baadhi waandike A tu na wengine B na vivyo hivyo kwa majibu mengine, lakini ilionekana wapo baadhi walifanikiwa kufanya vizuri bila ya kujua alichokichagua ni jibu sahihi.

"Katika mazingira kama hayo huwezi kumpima mwanafunzi wakati mtihani anaofanya haumchuji anayejua kusoma au asiyejua..." alisema mwalimu Nassoro.


Baadhi+ya+madarasa+ambayo+hutumika+kwa+m

*Habari hii imeandaliwa na Thehabari.com (www.thehabari.com) kwa kushirikiana na HakiElimu

 
Haki Elimu HakiElimu

Walimu watoa maoni yao kuhusu mtihani wa #neshino unaotarajia kufanyika kesho http://t.co/csSWNnAw pia fuatilia #neshino utume ujumbe wako

Haki Elimu HakiElimu

Ugatuaji (decentralization) wa Baraza la mithani Tanzania (NECTA) wapendekezwa na TAMONGSCO ili kumaliza wizi wa #neshino