Envaya
Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

JUAMA NI JUMUIYA YA KIJAMII (CBO) ILIANZISHWA 1998 NA KUSAJILIWA RASMI 23/9/2005.

  • REGISTRATION NUMBER: 383/2005
  • BANK ACCOUNT 031208000156 THE PEOPLES BANK OF ZANZIBAR

JUAMA ILIANZISHWA KAMA NI KIKUNDI CHA UHAMASISHAJI KUIMARISHA USAFI NA UPANDAJI MITI KUTOKANA NA MILIPUKO YA MARADHI YA KIPINDUPINDU NA MATUMBO PIA KUTOKANA NA ATHARI ZA UKATAJI WA MISITU OVYO KATIKA UKANDA WA PWANI YA MASHARIKI YA KISIWA HIKI CHA UNGUJA KWA VIJIJI KAMA VILE UROA;MARUMBI,DIKONI,PONGWE PWANI NA NDUDU

JUAMA INA OFISI YAKE KIJIJI CHA UROA WILAYA YA KATI, MKOA WA KUSINI UNGUJA

JUAMA INAFANYAKAZI ZA UIMARISHAJI MAZINGIRA IKIWA NI MKAKATI WA KUIMARISHA UCHUMI NA AFYA YA WANAJAMII.

BAADHI YA KAZI ZAKE KWA KUSHIRIKIANA NA JAMII NI

  • USAFISHAJI MAZINGIRA YA VIJIJI,
  • UHIFADHI WA FUKWE ZA BAHARI NA BAHARI;
  • UJENZI WA VYOO NA MAENEO YA KUHIFADHI TAKA NA KUHAMASISHA MATUMIZI YAKE
  • UHAMASISHAJI JAMII KATIKA MAMBO YA UTUNZAJI NA UHIFADHI MAZINGIRA
  • KUTOA ELIMU YA AFYA KWA WANAJAMII

JUAMA KWA KUSAIDIANA NA TAASISI ZENYE UJUZI ZAIDI HUSAIDIA

  • KUJENGA UWEZO WA KITAALAMU KWA VIKUNDI VYA MAZINGIRA,WAKULIMA, WANAWAKE WANAOJISHUGHULISHA NA KUJITAFUTIA KIPATO MFANO WANAOPANDA MWANI NA KUOTESHA MITI (MIVINJE,MIDIMU)
  • HARAKATI ZA ELIMU NA MAENDELEO KWA JUMLA.

BAADHI YA MAFANIKIO YA JUAMA NI KAMA IFUATAVYO:-

  • KUHAMASISHA NA KUTOA ELIMU KWA WANAJAMII WAPATAO 245 KUHUSIANA NA MAMBO YA AFYA NA MAZINGIRA
  • KUSHIRIKI MAONESHO MBALI MBALI YA KITAIFA MFANO YANAYOANADALIWA NA FOUNDATION OF CIVIL SOCIETY (FCS)
  • KUJENGA VYOO VIPYA (02) NA KUKARABATI VYOO VIKONGWE (6) NA KUHAMASISHA MATUMIZI YAKE KATIKA KIJIJI CHA UROA
  • KUJENGA MAENEO MAALUM YA KUHIFADHI TAKA (3) NA KUHAMASISHA WANAJAMII WAYATUMIE KIKAMILIFU
  • KUHASISHA WAKULIMA KUTUMIA TAKA ZILIZOOZA KUWA MBOLEA HIVYO KUIMARISHA KILIMO CHA KISASA
  • KUMASISHA UPANDAJI WA MIVINJE KWA WANAJAMII WAPATAO 32 WA UROA,MARUMBI NA PONGWE PWANI
  • KUTUNUKIWA CHETI CHA KITAIFA CHA UTUNZAJI MAZINGIRA/KUPANDA MITI 2006/07. PIA CHETI CHA USAFI WA MAZINGIRA 2008/09
  • KUANZA KUIMARISHA MAHUSIANO MEMA NA KUBADILISHANA UZOEFU NA VIKUNDI VINGINE VYA KIJAMII MFANO VYA JAMBIANI UNGUJA (JUMABEKO), NA HATA PEMBA
  • KUSHAJIHISHA KUUNDWA SACCOS (UROA SACCOS) YENYE WANACHAMA 140
  • KUSHAJIHISHA KUUNDWA KWA KAMATI YA ULINZI WA MSITI WA ASILI YENYE WAJUMBE WAPATAO 20 INAYOLINDA UHARIBIFU WA MSITU NA KUELEKEZA MATUMIZI SAHIHI YA MSITU WA UROA
  • KUSHAJIHISHA MATUMIZI BORA YA BAHARI NA UVUVI WA KISASA USIOHARIBU MAZINGIRA
  • KUJENGA USHAWISHI KWA SERIKALI HASA YA WILAYA NA MKOA ILI MAWEKEZAJI UTALII WACHUKUE JUHUDI ZA ZA MAKUSUDI KUHIFADHI MAZINGIRA