ELIMISHA ni shirika lisilo la kiserikali,ambalo limeanzishwa na waandishi wa habari kwa lengo kusaidia jitihada za serikali katika kuiwezesha jamii kwa kuijengea uwezo ili kuondokana na umasikini,shughuli kubwa za ELIMISHA hufanyika vijijini,ambako kuna uhitaji mkubwa wa huduma mbalimbali za kijamii, na baadhi ya shughuli za ELIMISHA ni kutafiti na kuibua matatizo ya wananchi ili serikali na mashirika mengine yaweze kusaidia, kama unavyoweza kuona matukio mbalimbali katika picha za walengwa wanahitaji misaada.
Maoni (0)
Upande wa kulia ni mtendaji mkuu wa Shirika la ELIMISHA, Festo Sikagonamo akiwa na mmoja wa wazee walio wahi kuhudumiwa na Shirika.
Wanafunzi wakiwa katika picha ya pamoja na walimu wao baada ya kupata msaada wa vifaa vya shule, uliotolewa na Shirika la ELIMISHA kwa baadhi ya watoto yatima.
Katika kufikisha huduma za uhakika na ufanisi kwa walengwa ELIMISHA inasshirikisha jamii kuibua na kupanga vipaumbele kupitia mikutano, huu ni mmoja wa mikutano ya ELIMISHA.
wazee waliotoa mchango mkubwa kwa Taifa kupitia kilimo kwa sasa wanahitaji msaada