Injira
Indaba Africa

Indaba Africa

Mbeya, Tanzania

Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Icyongereza. Edit translations

MAVAZI YA UTANDAWAZI NA ATHARI ZAKE.................................

Nusu+uchi.JPG
MWANADADA aliyevaa kaptula fupi akiwa anaokolewa na wasamalia wema katika eneo la Mwanjelwa Jijini Mbeya baada ya wananchi kumzomea huku wengine wakithubutu kutaka kumpiga wakipinga vazi hilo ambalo mabinti wengi wanaamini kuwa ni vazi la kisasa........... kutoka Tanzania yetu

*MDAU HAWA NDIYO WASANII WETU BIFU HILI CHANZO NINI?

rei.jpg
Chuki, Husda huanzia mbali na husababishwa na kitu kidogo tu, sasa hatua waliyofikia wasanii hawa vipenzi vya mashabik wa Bongo Movie, ni 'hakunaga mjinga' baina yao bado kutoleana 'vimiguu vya Kuku' tu

Hamad Rashid aitunishia misuli CUF, asema yeye bado ni mbunge

MBUNGE wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed, amepinga uamuzi wa Baraza Kuu la Uongozi la Chama Cha Wananchi (CUF) kumvua uanachama, akisema ni batili na umekiuka amri ya Mahakama.
Wakati Hamad akitoa tamko hilo, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa amekilipua CUF, akisema uamuzi wake wa kumfukuza uanachama Hamad, haukuzingatia maslahi ya wapiga kura wa Jimbo la Wawi, bali matakwa ya wachache ndani ya chama hicho. Licha ya kuwepo zuio la mahakama, juzi Baraza Kuu la Uongozi la CUF, lilimvua uanachama Hamad Rashid na washirika wake watatu ambao ni Mjumbe wa Baraza Kuu (Tanga), Doyo Hassan Doyo, Mjumbe wa Baraza Kuu (Pemba), Shoka Khamis Juma na Juma Saanane ambaye ni Mjumbe wa Baraza Kuu Unguja. Hatua hiyo ilimfanya Hamad kuitisha mkutano na waandishi wa habari jana na kutoa tamko kuhusu uamuzi huo ambao aliuita kuwa ni batili kutokana na kukiuka amri ya Mahakama kuzuia mkutano. Alisema muda mfupi kabla ya tangazo la kufukuzwa kwao uanachama, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ilitoa amri ya kuzuia kuendelea kwa kikao cha Baraza kuu, lakini baraza hilo lilikaidi na kuwafukuza. Mbunge huyo alisema: “Niliwaomba wanipe muda wa kujitetea kama wao walivyochukua muda wa kunihukumu, wakakataa. Kikao kile kilikuwa na watu wazito kama Waziri wa Sheria wa Zanzibar, Jussa, Taslima na Makamu wa Rais wa Zanzibar, wote wakiwa wanasheria, lakini wameshindwa kufuata sheria.” Hamad Rashid alihoji, “Kiongozi wa Serikali kama Maalim Seif anakataa kutii amri halali ya mahakama? Akija kuwa rais itakuwaje? Nimeogopa sana?” Hata hivyo, Hamad na wenzake walisema wataendelea kupigania haki yao ndani ya CUF mpaka ipatikane."Tunaheshimu uamuzi wa Mahakama. Kwa amri hiyo uamuzi wa Baraza Kuu ni batili. Bado sisi ni wanachama halali..., bado mimi ni mbunge na tuna mashiko ya kuendelea kufanya kazi za chama,” alisisitiza. Alisema, “Jana (juzi) nilipata simu zaidi ya 15 za wanachama kutoka mikoani akiwemo aliyekuwa mbunge wa Chadema Jimbo la Tarime, Charles Mwera wakiniunga mkono." "Wana CUF mikoani wametangaza kutuunga mkono. Mwanza wameandaa maandamano, Tanga wamesema hadi leo jioni watakusanya kadi 2,000 kwa Dar es Salaam Temeke wameshakusanya kadi 600 na mikoa mingine mingi”. Alisema hukumu dhidi yao ilikuwa imeshaandaliwa hata kabla ya kusikilizwa na kwamba hata Kamati ya Nidhamu iliyowahoji haikuwa halali kikatiba. “Tumefanya mabadiliko ya Katiba ya chama mara mbili. Kifungu cha 81 cha Katiba ya chama kinaitaka Kamati ya Katiba iidhinishwe na Baraza Kuu, lakini wajumbe wote wa kamati ile wanakaimu nafasi zao. Makamu mwenyekiti wa chama huyo huyo ndiyo aliyeongoza kikao cha Kamati ya Nidhamu na huyo huyo ndiye aliyeongoza Baraza Kuu kutuhukumu,” alisema. Alisema Baraza Kuu halikutenda haki ya kusikiliza kila upande na kuongeza: “Kwa kuzingatia ‘natural justice’, Baraza Kuu limepoteza uwezo wa kusikiliza na halina sifa ya kutenda haki. Baraza hilo lenye wanasheria wengi, lakini halikutupa nafasi ya kutusikiliza.” Tuhuma dhidi yake Kuhusu tuhuma alizopewa kabla ya kufukuzwa, alisema Kitabu chake cha ‘Yaliyojiri’ alichokitunga mwishoni mwa mwaka jana ndicho kimesababisha yote.Katika kitabu hicho, Hamad ameweka barua aliyowaandikia viongozi wa chama hicho akiwaeleza mwenendo mbaya wa chama hicho. Hata hivyo, Hamad Rashid alisema uongozi wa chama hicho akiwemo mwenyekiti Profesa Ibrahim Lipumba, walimwonya asiendelee kukisambaza kitabu hicho naye akaacha. “Hivyo nimehukumiwa kwa kutoa kitabu hicho wakati tayari nilishaacha kukisambaza. Fedha iliyotumika kutufukuza ingetosha kabisa kugharimia matawi mikoani. Waulizeni nguvu waliyotumia kwenda Mwanza, kuzunguka Zanzibar, Lindi na Mtwara yote kuwaambia kuwa eti Hamad ni msaliti” alisema na kuongeza:, “Mimi kama nimetumia fedha basi ni Sh 500,000 tu, 250,000 kuimarisha tawi la Kosovo na nyingine tawi la Chechnya. Fedha za walipa kodi na michango ya wabunge yote imetumika kunishitaki mimi niliyejitolea kusema ukweli.” Kauli ya Tendwa Kwa upande wake Tendwa, alisema uamuzi huo wa kumfukuza Hamad Rashid ambaye ni mbunge wala kujali maslahi ya wapiga kura wa Wawi bali maslahi ya chama. Tendwa alisema hayo jana Ikulu jijini Dar es Salaam alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari baada ya kuhudhuria hafla ya kuwaapisha viongozi wapya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Alisema ni muhimu vyama vikaweka maslahi ya wapiga kura mbele kwa kuwa, ndiyo wanaomchagua mwakilishi wao na si chama kinachowachagulia. "Tunaweza tukabadilisha mifumo ya uchaguzi, chama kinapomfukuza mbunge ni lazima kimfikirie mpigakura atakuwa katika hali gani na pia suala la gharama lazima lifikiriwe,"alisema Tendwa. Msajili huyo mwenye dhamana na ustawi wa vyama vya siasa nchini, alisema ni muhimu mpigakura akapewa nafasi ya kufanya uamuzi huo kama anavyofanya wakati anapomchagua mbunge wake. "Busara inahitajika katika kufanya uamuzi huu ili isiwe ni tabia na desturi ambayo tunajiwekea,"alisema Tendwa. Mwenyekiti wa UDP na mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo alisema walichofanya CUF ni kukiuka sheria mama ya nchi ambayo ni Katiba. Alisema kwa mujibu wa Katiba, mbunge atakaa katika kiti chake kwa miaka mitano na utaratibu wa kumwondoa ni katika Uchaguzi Mkuu. "Katika nchi tuna sheria mama ambayo inatamka rais atatawala miaka mitano ukimwondoa hapo katikati unatafuta matatizo hivyo kwa mbunge,"alisema Cheyo. Alisema kitendo kilichofanya na CUF na NCCR ni kutafuta matatizo nchini na vurugu badala ya kujenga demokrasia. CUF: Hatuendeshwi na Mahakama Kwa upande wa uongozi wa CUF umetetea uamuzi wake wa kuwafukuza wanachama wake wanne na kuwaonya wengine 10, huku kikisema kimezingatia katiba yake. Chama hicho pia kimekanusha madai ya kupokea amri ya mahakama ya kuzuia mkutano huo, uliomalizika juzi kwa kuwafukuza wanachama wanne na kuwavua nyadhifa za uenyekiti na wanachama wanne. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara, Julius Mtatiro alisema: “CUF hatujapokea pingamizi la Mahakama kuzuia mkutano wa Baraza Kuu na kama amri hiyo ingekuwa sahihi kama tungeletewa juzi, (Jumatatu) na si siku ya mkutano.” Mtatiro alisema kimsingi, mahakama haina uwezo wa kuzuia mkutano wa chama cha siasa kama ulikwishaanza kwa kuwa chama hakiongozwi na mahakama. “Mahakama yoyote haina uwezo wa kuzuia mkutano wa chama cha siasa uliokwishaanza, chama hakiongozwi na mahakama bali kila chama kinaongozwa na katiba za vyama vyao ambazo zinatambuliwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Mtatiro. Katika mkutano huo, CUF kilitangaza kuwavua uenyekiti wanachama wake wanne katika Wilaya za Ilala, Temeke jijini Dar es Salaam na Nachingwea Mkoa wa Lindi. Waliovuliwa nyadhifa zao za uongozi ni waliokuwa wenyeviti katika Wilaya za Ilala, Don Waziri, na katibu wake Masaga Masaga, Temeke, Mohamed Albadawi na mwenyekiti wa Nachingwea, Haji Nanjase. Mtatiro alisema baraza lilipokea majina ya watuhumiwa 14 akiwamo Hamad Rashid na baada ya kuwahoji lilijiridhisha kwamba 12 kati yao walivunja katiba ya chama. Alifafanua kwamba, wajumbe wanne akiwamo Hamad Rashid wamefukuzwa uanachama na kuanzia sasa si mbunge kupitia chama hicho. “Kuanzia sasa Hamad Rashid si mwakilishi wa wananchi wa Wawi kupitia CUF, akitaka kuendelea kuwa Mbunge anapaswa kuwa mwakilishi kupitia mahakamani,”alisema Mtatiro. Mwanasheria Kwa upande wake ofisa mwandamizi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Harod Sungusia alisema tabia ya vyama vya siasa kuwafukuza uanachama wanachama wake, inatokana na matokeo ya mmomonyoko wa utawala wa sheria.Sungusia alisema hayo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa maoni kuhusu chama cha CUF kumfukuza uanachama mbunge huyo wa Wawi. Alisema vyama vya siasa vimekuwa vikifanya uamuzi kwa kujali maslai yao binafsi, ndio maana vimekuwa vikileta msuguano ndani vya vyama na kusababisha wengine kufukuzwa. “Kama wabunge wanatumia vizuri chombo chao cha kutunga sheria, wanaweza kuondoa matatizo haya kwa kutunga sheria ambazo zitawasaidia wananchi pamoja na kuwapa miongozo mizuri katika kazi zao ndani ya Bunge na nje ya Bunge,” alisema Sungusia.

Askofu Kilaini: Ndugai jibu hoja

Thursday, 05 January 2012 21:04
Waandishi Wetu Mwananchi ASKOFU Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Mhashamu Methodius Kilaini, amemshangaa Naibu Spika Job Ndugai kwa kile alichoeleza kuwa amekwepa kujibu hoja ya msingi ya Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye inayohusu nyongeza ya posho za wabunge, badala yake, ameshambulia kiongozi huyo kama mtu binafsi. "Sumaye kama mwanadamu anaweza akawa na upungufu mwingi, lakini alichokisema kuhusu posho tujihoji kina ukweli gani? Hilo ndilo la msingi. Alichotakiwa Ndugai ni kufafanua uhalali wa posho na sio kusema aliyetoa hoja hiyo, hana usafi wa kuhoji." Katika kuonesha kukerwa na kauli ya Ndugai, kiongozi huyo wa kiroho alikemea kauli za baadhi ya wanasiasa kutotaka kukosolewa hata pale wanapofanya makosa na kutaka watu waachwe waseme ukweli bila kuzibwa midomo wala kubezwa. "Watu waachwe waseme kweli wasibezwe. Kwamba naye (Sumaye) alijiongezea posho, hilo ni jambo lingine ambalo kama anataka (Ndugai), alianzishe mjadala watu wajadili. Lakini sasa tunazungumzia suala la posho za wabunge ambazo sote zinatukera,"alisema Kilaini. Kwa mujibu wa Askofu Kilaini, si sahihi mtu kujadili hoja aliyoanzisha mtu kwa kuangalia udhaifu wa mtoa hoja. "Hakuna hoja ya msingi katika kumshambulia mtu anayetoa hoja kwa kutumia udhaifu wake, kwani ukweli utaendelea kuwa ukweli na udhaifu wa mtu ni jambo lingine." Askofu Kilaini alisema: "Nataka watu wajue kwamba hakuna mtakatifu hapa, wote tuna udhaifu, lakini kama mwenzetu kasema ukweli tujadili hoja yake kwa moyo mkunjufu na sio kumpuuza kwa sababu tu eti aliyeongea ana upungufu fulani." Aliongeza; "Ndugai lazima asome alama za nyakati. Huu sio wakati wa kutetea posho kwani hakuna atakayemwelewa. Watanzania wa matabaka yote wamezipinga sasa yeye akianza kuzitetea atabaki peke yake." Wanasheria Kauli hiyo ya Askofu Kilaini, iliungwa mkono na baadhi ya wanasheria waliozungumzia hoja hiyo jana ambao kwa nyakati tofauti walisema kitendo cha Ndugai kuponda maoni ya Sumaye, kimeonyesha kuwa si mtu makini. Wakili wa kujitegemea, Lupia Augusto alihoji kama Ndungai alikuwepo bungeni wakati sheria ya kupandisha posho za viongozi wastaafu zilizomwezesha Sumaye kujiandalia uzee mwema, kwanini hakupinga. "Iweje aje na hoja hiyo leo?"alihoji. Augusto alisema tabia aliyoionyesha Ndugai inatakiwa kutafsiriwa kama hakujua majukumu ya ubunge wake wa kuhoji na badala yake, alijua itamnufaisha.Alifafanua kwamba kitendo alichokifanya Ndugai ni ishara kwamba maoni yake yamekumbatia kujinufaisha na sio kunufaisha wananchi. Alisema Ndugai ameanika udhaifu wake kwani hakuna rekodi zinazoonyesha kwamba alipinga hoja ya kupitisha posho ilipoletwa wakati Sumaye alipokuwa Waziri Mkuu.Augusto alisema kuna kila dalili kwamba kuna mambo mengi yanayofanywa kwa siri kwa maslahi ya wachache na kwamba wanapopingana ndipo mambo hayo hujitokeza wazi. “Wananchi wajiulize alifanya nini kupinga, maana hapa anaazisha malumbano yasiyokuwa na tija baada ya watu kupinga posho ambazo wabunge wamejipandishia bila kuweka uzalendo mbele,”alisema Awakera wananchi Baadhi ya wananchi nao wameeleza kukerwa na kauli ya Ndugai dhidi ya Sumaye na kwamba ni mbinu za kuwatisha viongozi wastaafu wasitetee maslai ya Umma. Mkazi wa Dar es Salaam, Kimazi Totera alisema Ndugai anatumia Bunge kama sehemu ya kutetea matakwa yake binafsi kwa kuziua kauli za viongozi wastaafu pale wanapotetea maslai ya Umma. Fatma Haji alisema Ndugai ana siri kubwa kutokana na kuyajua mazingira ya uongozi ya awamu ya tatu kwa kudai Sumaye alijiwekea sheria ya viongozi wa juu wastaafu kulipwa asilimia 80 ya mshahara. “Yeye kama kiongozi alikuwa wapi kupinga sheria ya viongozi hawa kulipwa kiwango hicho cha pesa ina maana naye ana chuki binafsi, tungemwelewa kama angesema mapema,”alisema Fatma. Alichosema Sumaye Jana alipotakiwa kuzungumzia hoja za Ndugai jana, Sumaye alisema," No comment," nataka kusoma na kuelewa vizuri alichokisema kwa hiyo unitafute kesho (leo)." Kilichoamsha hasira za Ndugai ni kauli ya Sumaye alioyoitoa kupitia kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha ITV, kwamba ongezeko la posho za wabunge linaweza kuchochea makundi mengine kudai kama Wanajeshi, Polisi, Mahakama na walimu nao kutaka nyongeza, hivyo kumweka Rais katika wakati mgumu kufanya uamuzi. “Mwanasiasa mzuri akifanya jambo akiona limewaudhi wananchi anatakiwa aliache, lakini pia kwenye hili huu mkanganyiko wa Spika na Katibu wake na huu ukimya wa Ikulu ni tatizo, tungependa waseme ili umma ujue hali ikoje,” alisema Sumaye. Alisema hatua ya Bunge kujipandishia posho ya kikao kutoka 70,000 hadi 200,000 kwa siku haliingii akilini na kwamba, inakiuka utaratibu uliowekwa na serikali katika kulipa gharama kwa maofisa wake ikiwa ni pamoja na gharama hizo za fedha za kujikimu. “Siyo kwamba napinga posho, wabunge wanastahili posho, lakini kwa kweli kujiongezea kutoka 70,000 hadi 200,000 siyo sahihi,” alisema Sumaye. Alisema wakati yeye alipoteuliwa na Rais Benjamin Mkapa kwa awamu ya pili kushika wadhifa wa Waziri Mkuu, aligoma kwa sababu alikuwa amekwaruzana na wabunge kuhusu nyongeza ya posho. “Nilimwambia wabunge watanikataa kwa sababu nimegombana nao sana juu ya suala la posho lakini akasema lazima uwe na mimi ndipo nikakubali, lazima hili suala liangaliwe mara mbilimbili…, leo wabunge mmejiongezea kesho jeshi, polisi na walimu nao watataka, tutafanyaje tusifanye mambo ambayo yatamuweka Rais pabaya,” alisema Sumaye. Alisema posho ni jambo ambalo kwa sasa limekuwa tatizo kwa serikali na kwamba imefika wakati ofisi za serikali zimehamia hotelini, lengo likiwa ni watumishi wa umma kutafuta mwanya wa kulipana posho. “Ndiyo maana watu wa TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania) wanakusanya fedha nyingi lakini ni fedha kidogo sana zinakwenda kwenye huduma za jamii, nadhani hili ni tatizo na ni utawala mbaya kabisa, lazima kuwepo mabadiliko kama kweli tunataka kuisafisha nchi yetu,” alisema Sumaye Habari hii imeandaliwa na Daniel Rutoryo, Keneth Goliama, Freddy Azzah

Ni Kusanyiko La Magezi-gezi? Wakufunzi Wa Wakufunzi!

002.jpg
00016.jpg
008.jpg
Ndugu zangu, Moyo wangu ulidunda, mara ile nilipopokea na kusoma mwaliko wa kujumuika na kusanyiko la wanahabari waliobobea na wenye majina makubwa. Ni kwenye mafunzo ya wakufunzi wa wanahabari. Kaka yangu Kajubi Mukajanga anasema; Wahaya wanamwita mtu anayejifanya anayejua jua sana mambo kwa jina la ' Lugezi-gezi'- Kwamba yeye anajua kila kitu!" Nami nilidhani ningefika Morogoro na kukutana na watu wenye hulka ya 'lugezi-gezi'- wajuaji wa kila kitu. Kwamba nisingekuwa na kipya cha kuwaambia. HAPANA! Kusanyiko hili la Morogoro limeniondoa mashaka hayo. Kila mmoja anaonekana kuwa na utayari wa kujifunza kutoka kwa mwenziye. Kuna utani mwingi pia. Tunacheka sana. Tunajifunza. kutoka mjengwa blog Naam, kusanyiko la Morogoro lina waandishi wenye uzoefu wa miaka mingi kwenye tasnia ya habari. Kuna majina kama Kajubi Mukajanga, Fili Karashani, Aboubakar Karsan, Nyaronyo Kicheere, Allan Lawa, Ally Saleh, Said Dogoli, Deo Mfugale, Moses Mataba, Mnaku Mbani.... orodha kamili inakuja. Maggid Mjengwa, Morogoro. Ijumaa, Januari 6, 2012.

Mafunzo Kwa Wakufunzi: Fili Karashani Na Kajubi Mukajanga

00020.jpg
00019.jpg
Ni mafunzo yanayofanyika Morogoro na yaliyoandaliwa na Union of Tanzania Press Clubs. Pichani juu ni waendesha mafunzo na wanahabari waliobobea hapa nchini; Fili Karashani picha ya juu na Kajubi Mukajanga ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania, MCT.

Chadema faults govt on policies

Wilbroad-Slaa.jpg
Chadema Secretary General, Dr Wilbroad Slaa (right) stresses a point during a press conference in Dar es Salaam on Thursday. Left is Kigoma North MP, Mr Zitto Kabwe. (Photo by Yusuf Badi)
Opposition Party – Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) – has faulted government policies, saying they have failed to tackle the country’s economic woes.
This was said by the party’s Secretary General, Dr Willbrod Slaa, at a press conference at Chadema’s headquarters in Dar es Salaam on Thursday.
“The government lacks innovation when it comes to solving Tanzania’s economic problems. Rather than looking for solutions, they have, instead politicized all problems.
“We are tired of hearing the government giving simple answers to sensitive issues. Take, for instance, the problem of sugar shortage in Kagera Region, the ruling party has focused on letting the local government officials distribute it leading to corruption,” he stated.
Dr Slaa said that his party thought that the best way of tackling economic problems was through increase in production.
The Secretary General also cited the ‘Kilimo Kwanza’ programme which focuses on increasing the country’s food production and also create employment which he claimed has failed.
“Imagine about 5,000 students graduated in agricultural courses last year but they are still jobless, yet we want to promote agriculture,” he said.
Dr Slaa claimed that the government would slash about 50 per cent of employment opportunities this year, a report he declared he had.
He said that Chadema would continue criticizing the government in a bid to push for development.
“We will continue speaking out. If students at universities strike, the government should look at the root of the crisis rather than causing more problems,” he noted.
Dr Slaa also said his party was not satisfied with the way the government was handling the disputes between pastoralists and farmers and the land rows between big agriculture investors and small scale farmers.
He urged the police to stop interfering in their peaceful demonstrations as they were the main cause of violence.
“It is our constitutional right to demonstrate. It should be noted that on most occasions, it is only when the police interfere that violence erupts,” said Dr Slaa.
Before the beginning of the press conference, the party’s members and audience had a moment of silence to remember the people who died in last year’s protests in Arusha.
By JULIUS BWAHAMA, Tanzania Daily News

MME WA MARIAH CAREY HALI MBAYA

2.jpg
1.png
Mariah Carey announced on her Twitter page that her husband Nick Cannon suffered mild kidney failure during a family vacation in Aspen, Colorado yesterday and had to be rushed to the hospital... She writes: This is us in the hospital - role reversal; Last year it was me attached to the machines (after having dembabies) and Nick was there with me through it, and now here we are. We're trying to be as festive as possible under the circumstances but please keep Nick in your thoughts because this is very painful. They tried to kick me out of the hospital but here I am pon de bed with Mr. C. We're doing OK but we're "straaaaaanded in Aspen". #DramaticDivaPlace (I know, we could be in a lot worse places) but the truth is as long as we're together, we're OK. I'm not trying to make light out of the situation because it's a serious moment that's very tough on all of us so please keep us and our family in your prayers. LYM.

brC8ge5zCbg

Oklahoma Mother Kills Intruder Breaking Into Her Home While on Phone With 911

The mother shot the 24 yr old intruder the second he stepped inside her home, and police call the shooting justified. Watch video...

IIySXm6UrY8