Christina Shusho Tena
![]() |
| Christina Shusho |
Amri ya kutotembea yawekwa Nigeria
Amri ya kutotoka nje wakati wowote ule imetangazwa katika jimbo la Adamawa, Nigeria, baada ya mashambulio kadha dhidi ya Wakristo.

Jeshi limeshika zamu mabarabarani, na taarifa kutoka mji mkuu wa jimbo, Yola, zinaeleza kuwa maduka na maofisi yote yamefungwa, na huduma za lazima tu ndio zinaruhusiwa.
Wafuasi wa kikundi cha Waisalmu wenye siasa kali, Boko Haram, wameshambulia kanisa, kituo cha jamii, na duka la msusi katika siku za karibuni, na kuuwa watu kama 29.
Sheria za dharura zilianzishwa katika majimbo kadha mengine ya kaskazini mwa Nigeria juma lilopita, ambako Boko Haram wamefanya mashambulio piya.
Kikundi hicho kimeuwa watu zaidi ya 500 katika muda wa mwaka.
BBC
Nyoni: Hakuna daktari aliyefukuzwa MNH
SERIKALI imesema haijawafukuza madaktari walio katika mafunzo ya vitendo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) waliogoma hivi karibuni na wala haina mpango wa kama huo.
Hayo yamesema na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni.
Katibu huyo amelazimika kutoa ufafanuzi huo kutokana na vyombo kadhaa vya habari kuripoti kuwa, madaktari 229 walio katika mafunzo ya vitendo katika hospitali ya Muhimbili wamefukuzwa kutokana na kufanya mgomo wa nchi nzima kwa lengo la kushinikiza serikali kuwalipa malimbikizo ya posho zao yanayofikia Sh milioni 176.
Aliongeza kusema kuwa, ingawa madaktari hao walikiuka maadili ya weledi kwa kufanya mgomo, hakuna daktari aliyerudishwa nyumbani wala kufutiwa mkataba kutokana na ukweli kuwa siku zote serikali inatumia busara na njia sahihi kutatua matatizo bila kumuumiza mtu.
“Hakuna daktari aliyefukuzwa, bali serikali inafanya utaratibu wa kuwaita makao makuu ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kupokea maelekezo ya mkataba mpya ili waweze kufanyakazi kwa kuzingatia kanuni na maadili na kurudisha nidhamu katika fani ya udaktari.
Wakati huo huo, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Haji Mponda amesema Taifa linakabiliwa na uhaba mkubwa wa madaktari na watenda kazi katika sekta ya afya hivyo serikali haikusudii kupunguza idadi yao.
Akizungumza na HABARILEO Jumapili kwa njia ya simu, Dk Mponda alisema baada ya mgomo huo kutokea serikali ilichukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha kuwa wagonjwa wanaendelea kupata huduma ili kuzuia madhara ambayo yangeweza kusababishwa na mgomo huo.
Alisema hatua mojawapo iliyochukuliwa na serikali ni kuchukua madaktari 50 waliokuwa katika orodha ya madaktari waliokuwa wakisubiri kupata nafasi ya kufanya mafunzo kwa vitendo na kuwajumuisha na madaktari wengine 25 ambao hawakujihusisha na mgomo huo.
“Kwa kuwa tulikuwa na akiba ya madaktari ambao walikuwa wanasubiri fursa ya kufanya mafunzo kwa vitendo tuliwaita na kuwapa fursa iliyoachwa na wenzao waliogoma. Tulifanya hivyo kuzuia athari za mgomo hivyo serikali haina mpango wa kufukuza wala kupunguza wafanyakazi wa seta ya afya.
Anafafanua kuwa lengo la kuwaita wizarani madaktari waliopo kwenye mafunzo kwa vitendo ni kuwapangia vituo vipya vya kazi na kuwapatia mkataba ambao utasaidia kuboresha nidhamu katika sekta ya afya.
Baadhi ya magazeti ya kila siku nchini (siyo HABARILEO), katika matoleo ya jana yalipamba kurasa zao za mbele kwa habari za kufukuzwa kwa madaktari 229 kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa madai ya kujihusisha na mgomo uliodumu kwa siku mbili wakishinikiza kulipwa malimbikizo ya posho.
Source: Habarileo
ATTENTION..! ATTENTION..! ATTENTION...!

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUFUNG
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUFUNGULIWA KESI: MWANASHERIA wa kujitegemea wa jinini Mwanza Stephen Magaigwa amekusudia kufikisha hati yake ya mashitaka kuwafungulia kesi Mwanasheria Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika Mahakama kuu Maalum ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na wanasheria hao kuruhusu makosa muhimu manne yanayokinzana yaliyomo katika katiba ya Jamhuri na ile ya Mapinduzi.
Mwanasheria Stephen Magaigwa.
Amesema kuwa Kupitia marekebisho ya katiba ya mwaka 1977 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Zanzibar ya mwaka 1984 tangu nchi hizi mbili zilipoungana kuna mambo walikubaliana kwamba haya ni ya Muungano lakini yamekiukwa kupitia marekebisho yaliyofanywa ya katiba ya Zanzibar.
"Baada ya kutumia taaluma yangu kifungu baada ya kifungu nimegundua kuwa marekebisho hayo yameingilia mambo ya Muungano na kuleta mkinzano au mkanganyiko katika shughuli za kila siku za utendaji wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania".
"Nilitegemea kuwa wanasheria wa serikali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wangechukuwa hatuwa maalum kurekebisha hali hii tangu awali kabla ya kuipeleka katika utekelezaji lakini walikaa kimya kama wataalamu wa sheria wasiojuwa kazi yao.
Mambo manne aliyogundua"
Mbele ya wandishi wa habari.
1.Haki za binadamu:- "Katika marekebisho ya katiba ya Zanzibar suala la Haki za Binadamu katiba hiyo imezua kwamba haliwezi kuja katika Mahakama ya Rufaa –Wakati Ukisoma katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jedwali la 1 unagundua kuwa suala la Mahakama ya Rufaa ni suala la Muungano"
"Lakini Haitoshi linapokuja suala la haki za binadamu nchi inayohusika ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania"
2.Ukisoma Marekebisho ya Katiba ya Zanzibar kifungu cha 2A Rais wa Zanzibar anaweza akaigawa Zanzibar katika mikoa, wilaya na maeneo mengine kadri atakavyojisikia – Lakini kifungu cha katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2(2) Suala la Mipaka ya nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni suala la Muungano hivyo Rais akitaka kuigawa sehemu ya Jamhuri ya Muungano (Tz bara na Tz visiwani) ni lazima awasiliane na Rais wa Zanzibar Lakini ya Zanzibar inasema anaweza kugawa bila kuwasiliana na Rais wa Tanzania, sasa tuna nchi moja ambayo imeungana kwenye mipaka lakini watu wawili wanaohusika kuigawa.
3.Majeshi ya Ulinzi:- "Katiba ya Jamhuri inasema kuwa nchi pekee ambayo imepewa mamlaka ya kuunda majeshi ya ulinzi au vikosi vya aina yeyote ile ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lakini Marekebisho ya kumi ya sheria namba 9 ya mwaka 2010 ya katiba ya Zanzibar yanasema sasa wanaweza kuunda vikosi kama KMKM na kadhalika … Swali ni nani Amri Jeshi Mkuu wa majeshi hayo? Kwani yanapoundwa lazima yawe na mtoa amri wake mkuu"
Katiba zinazokinzana.
4.Wakuu wa nchi wawili:- "Ukisoma katiba ya Zanzibar 26(1) na ile ya Muungano kifungu cha 33(2) utagundua kuwa sasa tuna wakuu wa nchi wawili, sasa tunapokuwa na wakuu wawili ile hali katika katiba hatua ruksa ya kuwa na ‘two head of state in one country’ hali hii inamaanisha nini?"
"Nimefungua kesi hii Mwanza kwa mujibu wa Kifungu cha katiba ya Jamhuri 126-127 na 128, hivyo shauri langu litakapo sajiliwa na kupatiwa hati ya Mashitaka, Rais atapewa taarifa kuteuwa majaji wa kusikiliza kesi hii maalum ya katiba kwenye mahakama maalum ya katiba"
Lengo kuu:- Nitaomba Mahakama hiyo iamuru katiba ya Zanzibar irekebishwe kuondoa kasoro hizo haraka iwezekanavyo ili kuleta sifa ya Muungano. IPC NA UTPC YAWAKUTANISHA WADAU WA HABARI IRINGA
MAZISHI YA ASKARI ALIYEUAWA NA JAMBAZI MWANZA
Ajali Ya Basi La Taqwa na Moro Best




PILIKAPILIKA ZA UJENZI WA MAKAZI MAPYA YA WAATHIRIKA WA MAFURIKO MABWEPANDE
![]() |
| Baadhi ya waahtirika wa mafuriko wakitembezwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, kuona maendeleo ya ujenzi wa mahema watakamohamia |
![]() |
| JKT wakiendelea kuenga mahema |
![]() |
| Baadhi ya Askari wa JKT, wakihudumiwa maji baada ya kupata mlo wa mchana |
![]() |
| Mfumo wa maji wa muda ukiwa umetengenezwa KUTOKA KWA MTAA KWA MTAA |












